Uchaguzi 2020 Tundu Lissu awataka wanachama kutoshangilia kwa hofu ya mapingamizi, afikiria kuweka pingamizi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu awataka wanachama kutoshangilia kwa hofu ya mapingamizi, afikiria kuweka pingamizi

Mpinzani kuwekewa pingamizi au kuenguliwa wala sio habari, bali mgombea wa ccm hasa rais, hiyo ni ajabu ya karne.
Hata ingelikuwa mpinzani ndiye mwenye dola still tangelikuwa haya haya tu.

Uniteue kuwa judge kisha nije nikujudge vibaya, probability ni 0.0008
 
Kwa hiyo leo atahangaikia urais, wale wa majimbo wasahau maana attention yote anataka iwe kwenye Urais.

Hiyo ndiyo counter attack ya CCM. Wanakusubirisha huku, kule wanakula vichwa.
 
Mbona hofu nyingi sana!
Kwa sababu hakutegemea kufika hapo. Alijua atakatwa akawa anapiga mabomu ya maangamizi, lakini mambo yamegeuka ni mgombea uraisi kwa tiketi ya Chadema na mabomu yamebakia machache na vita ni siku 90. Kwa hiyo ajipange kama gentleman anayewania uraisi na sio Mau Mau terrorist fighter.
 
Kwahiyo kwa unavo elewa muda huu nchi haina Rais?

Mapicha picha yana kazi gani, ni kama tunalazimishana kumkubali mtu.

Hii siyo mara ya kwanza kushangaa mambo haya, hata events za nje, unaona wametundika picha, tena unaona kabisa walihangaika pa kuiweka? WHY?

Hata kwa aesthetic and design reasons tu, ukiachilia mbali sababu za kisheria, hiyo picha haipendezi hapo. Imeziba hata maneno muhimu!
 
Lissu hakatai mapingamizi, ndio maana alirudi nchini licha yakua anajua mangapi yanayomsubiri.

Anachohitaji nihayo mapingamizi yafuate Sheria pasipo kumuonea wala kumpendelea

Unafikiri hata yakiwa ya haki atakuambia ni ya haki? Hawa jamaa wapo vizuri kwahadaa mashabiki wao, kila siku wao wapo sahihi kila wafanyalo serikali ndiyo huwaonea.

Mfano leo kuna sehemu walisema walikuwa hawajahakiki majimboni ndiyo maana wakasubirishwa? Hapana hakusema, ila alikuwa analijua hili.

Ila akakuambia anasubirishwa kwasababu wanataka kumkata! Hapo unatengenezwa ili utete usichokijua.

Hawa wanasiasa waache tu, wote sio CCM sio Chadema!

Hakuna cha kuwa mwana CCM, hata kesho tukimkabidhi Lissu nchi CHADEMA watakuwa na favour fulani tofauti na vyama vingine. This is natural..only what you can do is to reduce.
 
Unaongozwa na hisia zaidi, ndio maana unajenga hoja za kutetea uovu kwa kisingizio kuwa hata wengine wangefanya kama ww. Udhaifu wako usihamishie kwa wengine.
Hahaha! Kuna uhalisia wa kuandika na maisha halisi.

Wewe unaongelea kilichotakiwa kufanywa jambo ambalo sipingani nalo kabisa.

Lakini, reality huwezi kulifanya wewe mwenyewe.
 
Nimeangalia picha hii nimestaajabu sana. Ni sahihi picha ya Rais, na ambaye pia ni mgombea wa uchaguzi, kuwekwa pale ukutani? Hivi Taasisi kama Tume ya Uchaguzi si wanatakiwa wawe neutral, kabla, wakati na baada ya uchaguzi?

View attachment 1548084
Siyo kosa. Nchi bado inaongozwa na rais. Tunahitajii kufanya mabadiliko ya katiba ili kuondoa kero ndogondogo kama hizi.
 
Siyo kosa. Nchi bado inaongozwa na rais.tunahitajii kufanya mabadiliko ya katiba ili kuondoa kero ndogondogo kama hizi.

Katiba haiwezi kuongelea vitu kama hivyo. Kuna wakati busara na common sense inahitaji kutumika. Wahenga wana msemo, ‘just because you can do it, it doesn’t mean that you should’.
 
Back
Top Bottom