Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Tundu Lissu azungumza na Wananchi na Wanachama wa CHADEMA - Januari 01, 2025

Kumbuka hata hao veteran politician, walianza wakiwa hawana influence ktk jamii, hivo ni jambo jema kuwapa nafasi watu wapya.
Politics starts at grassroots, unatakiwa uwe maarufu huko kwanza kabla ya kwenda national.

CDM viti maalum wake inateua, wakati CCM ni nafasi za kugombea.

Sasa kama unateua hakikisha unaweka watu ambao wameshakomaa au kama ni kuchanganya wamawalimu bungeni.

Siasa ni rahisi sana Tanzania
 
Uchaguzi huu,lazima usimamiwe na Vyombo vya usalama,ili kulinda raia na Mali zao!
TAL kuwa mpole!
 
TLS ilipoteza uelekeo kwa kuchaguliwa kuwa Rais!
Sasa hasara ile anataka kuipeleka chadema!
Tuondolee upuuzi wako wa kukariri unajua alihudumu kwa muda gani kabla Magufuli hajatuma watu kumpiga risasi. Jaribu kuficha ujinga wako kwa kutaka kujadili mambo yanayokuzidi upeo wako wa utambuzi.
 
Yani Magufuli alivyotaka kuongezewa muda FAM na genge lake walipiga kelele sana, ila Yeye FAM hataki pawe na ukomo wa madaraka kwenye chama.

Hii ni demokrasia gani? Demokrasia inaanzia kwa vyama vya upinzani kuonyesha mfano. CHADEMA inapoteza muelekeo, sijui kama wakitangaza maandamano tena kama kuna watu wenye akili zao watatokea.

Ni vizuri kama Watanzania tumeyajua haya ndani ya muda huu. Tushajua sasa FAM na genge lake sio watu wa kuwaamini tena, siku hizi hata akina MMM na Bonge wa Mayai wamepoteza mvuto kwa haraka sana.
 
Kama mchangiaji wa jukwaa la siasa embu kuwa.

Sina shida kuambiwa nimeandika ujinga hata kama hakuna justification ya kejeli.

Huko kujifanya unawajua watu ni kujitangaza ni mtu wa hovyo.
Wewe na maccm wenzako ndiyo watu wa hovyo unafikiri kumshambulia Lissu ndiyo mnamsaidia Sultan Mbowe kushinda ?
 
Sasa huo u-veteran unasaidia nini kama haumuwezeshi muhusika kuwashawishi Wananchi wamchague? Pengine wewe ndo huelewi dhana ya POSITIVE DISCRIMINATION.

Mtu yeyote anayelitakia mema taifa hili, atatamani kuwepo na upinzani imara, na huo upinzani imara unahitaji uwe na watu wenye haiba kama ya Tundu Lissu.

Chadema ikisuasua, watakaoathirika ni walalahoi. CCM sababu haitakuwa tena na cha kuhofia, haitahitaji wapiga debe kama wewe, bali watagawana vyeo kwa kuzingatia ukwasi, undugu na urafiki. Nyinyi wengine labda itakoee zali la mtende kuota jangwani.

Tunaweza kuitetea CCM , ila tusiombee mabaya vyama vinavyokosoa mwenendo wa uendeshaji wa taifa letu.
All the best on your wishful thinking.

Uhalisia bado kwa uongozi wa juu hata ndani ya CDM, let alone being a president (daah) I can imagine hasa kwa nchi yenye civil services mbovu kama ya Tanzania.
 
Mhe Lissu kama alivyoahidi kuhutubia Taifa Leo siku ya tarehe 01.01.2025 majira haya ya mchana,

Mhe Lissu ni mkweli na tayari amenafanya hivyo msikilize.

Usiondoke Jf kwa habari na madili mbalimbali



View: https://www.youtube.com/watch?v=ozQqkisoXJ4

==============================================

Kuhusu Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, Tundu Lissu amesema:

"Kiuhalisia kama sio kisheria, nchi yetu sasa iko kwenye utawala wa kiimla usiokubali ushindani wa kiuchaguzi wa wazi wazi. Kama baada ya chaguzi hizo mbili (2019 na 2020) kuhusu aina ya utawala wa kiimla tulionao mashaka hayo yameondolewa na Uchaguzi wa mitaa na vijiji wa mwaka huu"

"Kuanzia sasa hakuwezi kuwa na ubishi miongoni mwetu kuwa bila kupigania na kubadilisha mfumo mzima uliopo wa kikatiba, kisheria na kitaasisi wa mfumo mzima wa Uchaguzi, hakutakuwa tena na uwezekano wa kuwa na Uchaguzi ulio wa wazi na haki"



  • Lissu ameishauri kamati kuu kuwepo na mabalozi wa nchi rafiki kama watazamaji na waangalizi wa uchaguzi wao wa ndani ya chama:

"Sambamba na viongozi wa kidini, kamati kuu vile vile iwaalike wawakilishi wa kibalozi wa nchi rafiki ili nao washiriki kama watazamaji wa uchaguzi wetu. Hiyo pia itaongeza uzito wa uchaguzi wetu ikiwemo kuongeza macho dhidi ya wale wote wanaopanga uchaguzi huo"


  • Kuhusu ukomo wa madaraka kwa wabunge na madiwani wa viti maalum ndani ya CHADEMA, Lissu amesema:

"Kama hoja kuu ya kupinga ukomo wa madaraka kwenye vyama ni kwamba uongozi wa vyama vya siasa ni kazi ya kujitolea wanaopalilia hoja hii wamenyamaza kimya kuhusu pendekezo langu la kuwa na ukomo wa madaraka katika ubunge na udiwani wa viti maalum ambazo zote sio kazi za kujitolea"

"Kwa uzoefu wetu wenyewe, badala ya viti hivi kuwa fursa ya kuwajengea uwezo na uzoefu wa kuwa wabunge na madiwani, utaratibu wa viti maalum sasa umekuwa ni utaratibu wa wanawake wachache kujijengea himaya za kimalkia ndani ya vyama vyao kwa kutumia fursa na mafao ya ubunge au udiwani ili kujihakikishia wanaendelea kuwa wabunge"



  • Lissu pia ameonesha kushangazwa na watu ndani ya CHADEMA wanaopinga hoja ya ukomo wa madaraka:
“Mimi nimependekeza kurudisha ukomo wa madaraka katika mfumo wa uongozi wa chama chetu, na katika uwakilishi wa wanawake bungeni na katika halmashauri za serikali za mitaa.

Hili ni jambo la pili linalohitaji kufanyiwa kazi ili tuweze kujiweka sawa kitaasisi. Katika hili ni lazima nikiri kwamba nimeshangazwa sana na mapokeo ya baadhi ya viongozi wa juu wa chama chetu.

Sikuwahi kufikiri kwamba, kwenye suala la ukomo wa madaraka ya kisiasa, kuna baadhi yetu ndani ya chama ambao, kwa kujielewa au la, bado wanatamani kuirudisha nchi yetu nyuma kikatiba kwa zaidi ya miaka arobaini.”

Hoja kubwa ambayo imetolewa na wanaopinga ukomo wa madaraka ndani ya chama ni kwamba utaratibu huu haufai kwa vyama vya siasa, hasa vya upinzani, ambako uongozi wake hauna malipo na unahitaji kiwango cha hali ya juu cha kujitolea katika ujenzi wa chama.

Hoja hii inatakiwa kuangaliwa kwa tahadhari kubwa. Kwanza, kama lengo la ukomo wa madaraka ni kudhibiti ving’ang’anizi wa madaraka na kuhakikisha utaratibu wa kuachiana madaraka kwa njia za kikatiba,ukomo wa madaraka unawahusu viongozi wote wa kisiasa bila kujali wanajitolea au wanalipwa mishahara.”


  • Kuhusu kuachiliwa kwa George Sanga, Tundu Lissu amesema:
"Huu ulikuwa ni mwaka wa George Sanga mfungwa mwingine wa kisiasa ambaye amemaliza miaka 4 na amemaliza mwaka wa 5 ndani ya gereza la Njombe akiwa ni mhanga wa siasa za kiuchaguzi za John Pombe Magufuli na kazi inayoendelea na Samia Suluhu Hassan."

  • Kuhusu Maridhiano kati ya CHADEMA na Samia, Lissu alisema:
"Kuna wale ambao kwa sababu ya maslahi na vijimanufaa fulani fulani wamejisahau na kuanza kumsifia na kumsafisha utawala wa kiimla wa Samia Suluhu Hassan"

"Kama maridhiano na Samia yalikuwa na manufaa makubwa kama tunavyoambiwa sasa, tuwaambie nini wajane na watoto wa Marehemu Medi George Juma Mohamed, Steven Chalamila na Modestus au tuwaambie nini wazazi na ndugu zao Deus Soka, Emanuel Mbise, Jacob Mlay, Shadrack Chaula na John Kipanya"

"Au maaan ya maridhiano ilikuwa ni kupeana michongo ya pesa tu?"

Akili kubwa huyu Chiba
 
Yani Magufuli alivyotaka kuongezewa muda FAM na genge lake walipiga kelele sana, ila Yeye FAM hataki pawe na ukomo wa madaraka kwenye chama.

Hii ni demokrasia gani? Demokrasia inaanzia kwa vyama vya upinzani kuonyesha mfano. CHADEMA inapoteza muelekeo, sijui kama wakitangaza maandamano tena kama kuna watu wenye akili zao watatokea.

Ni vizuri kama Watanzania tumeyajua haya ndani ya muda huu. Tushajua sasa FAM na genge lake sio watu wa kuwaamini tena, siku hizi hata akina MMM na Bonge wa Mayai wamepoteza mvuto kwa haraka sana.
Magufuli alitaka kuongezewa muda wapi, sana sana wapiga zumari wote wakutaka aongezewe muda hawakurudi bungeni.

Acheni hii tabia ya kujiongopea wenyewe na kuishi kwa kuamini uongo wenu.

Lini Magufuli kawai kusema alikuwa na mpango wa kuvunja katiba zaidi ya hadithi tu.

Usijiongopee
 
Back
Top Bottom