Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
He is very Briliant, Talented and Charismatic zaidi ya GentamycinLissu huwa hachoshi kumsikiliza Mungu tuachie Lissu atukomboe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
He is very Briliant, Talented and Charismatic zaidi ya GentamycinLissu huwa hachoshi kumsikiliza Mungu tuachie Lissu atukomboe.
Vikao ndio vinateka masanduku ya kura na kuuwa wagombea?TAL ni mwanaharakati! Anachosema vifanyike kwenye chama ,hakuna vikao ndani ya chama?
Chama kisipofanya,atalaumu nani na atakifanyia nini?
Lissu Hana Cha kupoteza mkuu, hajawahi kuwa mwenyekiti, mbowe ndo atajutaAnayetarajia kujuta ni Lissu.
Well saidLissu Hana Cha kupoteza mkuu, hajawahi kuwa mwenyekiti, mbowe ndo atajuta
Politics starts at grassroots, unatakiwa uwe maarufu huko kwanza kabla ya kwenda national.Kumbuka hata hao veteran politician, walianza wakiwa hawana influence ktk jamii, hivo ni jambo jema kuwapa nafasi watu wapya.
Wewe umekariri tu Lissu ni mwanaharakati hata ukiambiwa utoe definition ya harakati hujui, wewe ni mccm unawashwa nini na Chadema?TAL ni mwanaharakati! Anachosema vifanyike kwenye chama ,hakuna vikao ndani ya chama?
Chama kisipofanya,atalaumu nani na atakifanyia nini?
TAL atapoteza Umakamu mwenyekiti na Uwenyekiti!Lissu Hana Cha kupoteza mkuu, hajawahi kuwa mwenyekiti, mbowe ndo atajuta
TLS ilipoteza uelekeo kwa kuchaguliwa kuwa Rais!Wewe umekariri tu Lissu ni mwanaharakati hata ukiambiwa utoe definition ya harakati hujui, wewe ni mccm unawashwa nini na Chadema?
Kama mchangiaji wa jukwaa la siasa embu kuwa.Hata wewe akili zako zinakutosha kuosha vinyeo vya vizee vya kizungu
..kwa vile amekuwa makamu na hajaomba Haina shida, uwenyekiti hawezi poteza maana hajawahi kuwa naoTAL atapoteza Umakamu mwenyekiti na Uwenyekiti!
..kwa vile amekuwa makamu na hajaomba Haina shida, uwenyekiti hawezi poteza maana hajawahi kuwa naoTAL atapoteza Umakamu mwenyekiti na Uwenyekiti!
Trust me! TAL anakosa bara na pwani!..kwa vile amekuwa makamu na hajaomba Haina shida, uwenyekiti hawezi poteza maana hajawahi kuwa nao
Tuondolee upuuzi wako wa kukariri unajua alihudumu kwa muda gani kabla Magufuli hajatuma watu kumpiga risasi. Jaribu kuficha ujinga wako kwa kutaka kujadili mambo yanayokuzidi upeo wako wa utambuzi.TLS ilipoteza uelekeo kwa kuchaguliwa kuwa Rais!
Sasa hasara ile anataka kuipeleka chadema!
Wewe na maccm wenzako ndiyo watu wa hovyo unafikiri kumshambulia Lissu ndiyo mnamsaidia Sultan Mbowe kushinda ?Kama mchangiaji wa jukwaa la siasa embu kuwa.
Sina shida kuambiwa nimeandika ujinga hata kama hakuna justification ya kejeli.
Huko kujifanya unawajua watu ni kujitangaza ni mtu wa hovyo.
All the best on your wishful thinking.Sasa huo u-veteran unasaidia nini kama haumuwezeshi muhusika kuwashawishi Wananchi wamchague? Pengine wewe ndo huelewi dhana ya POSITIVE DISCRIMINATION.
Mtu yeyote anayelitakia mema taifa hili, atatamani kuwepo na upinzani imara, na huo upinzani imara unahitaji uwe na watu wenye haiba kama ya Tundu Lissu.
Chadema ikisuasua, watakaoathirika ni walalahoi. CCM sababu haitakuwa tena na cha kuhofia, haitahitaji wapiga debe kama wewe, bali watagawana vyeo kwa kuzingatia ukwasi, undugu na urafiki. Nyinyi wengine labda itakoee zali la mtende kuota jangwani.
Tunaweza kuitetea CCM , ila tusiombee mabaya vyama vinavyokosoa mwenendo wa uendeshaji wa taifa letu.
Mhe Lissu kama alivyoahidi kuhutubia Taifa Leo siku ya tarehe 01.01.2025 majira haya ya mchana,
Mhe Lissu ni mkweli na tayari amenafanya hivyo msikilize.
Usiondoke Jf kwa habari na madili mbalimbali
View: https://www.youtube.com/watch?v=ozQqkisoXJ4
==============================================
Kuhusu Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, Tundu Lissu amesema:
"Kiuhalisia kama sio kisheria, nchi yetu sasa iko kwenye utawala wa kiimla usiokubali ushindani wa kiuchaguzi wa wazi wazi. Kama baada ya chaguzi hizo mbili (2019 na 2020) kuhusu aina ya utawala wa kiimla tulionao mashaka hayo yameondolewa na Uchaguzi wa mitaa na vijiji wa mwaka huu"
"Kuanzia sasa hakuwezi kuwa na ubishi miongoni mwetu kuwa bila kupigania na kubadilisha mfumo mzima uliopo wa kikatiba, kisheria na kitaasisi wa mfumo mzima wa Uchaguzi, hakutakuwa tena na uwezekano wa kuwa na Uchaguzi ulio wa wazi na haki"
- Lissu ameishauri kamati kuu kuwepo na mabalozi wa nchi rafiki kama watazamaji na waangalizi wa uchaguzi wao wa ndani ya chama:
"Sambamba na viongozi wa kidini, kamati kuu vile vile iwaalike wawakilishi wa kibalozi wa nchi rafiki ili nao washiriki kama watazamaji wa uchaguzi wetu. Hiyo pia itaongeza uzito wa uchaguzi wetu ikiwemo kuongeza macho dhidi ya wale wote wanaopanga uchaguzi huo"
- Kuhusu ukomo wa madaraka kwa wabunge na madiwani wa viti maalum ndani ya CHADEMA, Lissu amesema:
"Kama hoja kuu ya kupinga ukomo wa madaraka kwenye vyama ni kwamba uongozi wa vyama vya siasa ni kazi ya kujitolea wanaopalilia hoja hii wamenyamaza kimya kuhusu pendekezo langu la kuwa na ukomo wa madaraka katika ubunge na udiwani wa viti maalum ambazo zote sio kazi za kujitolea"
"Kwa uzoefu wetu wenyewe, badala ya viti hivi kuwa fursa ya kuwajengea uwezo na uzoefu wa kuwa wabunge na madiwani, utaratibu wa viti maalum sasa umekuwa ni utaratibu wa wanawake wachache kujijengea himaya za kimalkia ndani ya vyama vyao kwa kutumia fursa na mafao ya ubunge au udiwani ili kujihakikishia wanaendelea kuwa wabunge"
“Mimi nimependekeza kurudisha ukomo wa madaraka katika mfumo wa uongozi wa chama chetu, na katika uwakilishi wa wanawake bungeni na katika halmashauri za serikali za mitaa.
- Lissu pia ameonesha kushangazwa na watu ndani ya CHADEMA wanaopinga hoja ya ukomo wa madaraka:
Hili ni jambo la pili linalohitaji kufanyiwa kazi ili tuweze kujiweka sawa kitaasisi. Katika hili ni lazima nikiri kwamba nimeshangazwa sana na mapokeo ya baadhi ya viongozi wa juu wa chama chetu.
Sikuwahi kufikiri kwamba, kwenye suala la ukomo wa madaraka ya kisiasa, kuna baadhi yetu ndani ya chama ambao, kwa kujielewa au la, bado wanatamani kuirudisha nchi yetu nyuma kikatiba kwa zaidi ya miaka arobaini.”
Hoja kubwa ambayo imetolewa na wanaopinga ukomo wa madaraka ndani ya chama ni kwamba utaratibu huu haufai kwa vyama vya siasa, hasa vya upinzani, ambako uongozi wake hauna malipo na unahitaji kiwango cha hali ya juu cha kujitolea katika ujenzi wa chama.
Hoja hii inatakiwa kuangaliwa kwa tahadhari kubwa. Kwanza, kama lengo la ukomo wa madaraka ni kudhibiti ving’ang’anizi wa madaraka na kuhakikisha utaratibu wa kuachiana madaraka kwa njia za kikatiba,ukomo wa madaraka unawahusu viongozi wote wa kisiasa bila kujali wanajitolea au wanalipwa mishahara.”
"Huu ulikuwa ni mwaka wa George Sanga mfungwa mwingine wa kisiasa ambaye amemaliza miaka 4 na amemaliza mwaka wa 5 ndani ya gereza la Njombe akiwa ni mhanga wa siasa za kiuchaguzi za John Pombe Magufuli na kazi inayoendelea na Samia Suluhu Hassan."
- Kuhusu kuachiliwa kwa George Sanga, Tundu Lissu amesema:
"Kuna wale ambao kwa sababu ya maslahi na vijimanufaa fulani fulani wamejisahau na kuanza kumsifia na kumsafisha utawala wa kiimla wa Samia Suluhu Hassan"
- Kuhusu Maridhiano kati ya CHADEMA na Samia, Lissu alisema:
"Kama maridhiano na Samia yalikuwa na manufaa makubwa kama tunavyoambiwa sasa, tuwaambie nini wajane na watoto wa Marehemu Medi George Juma Mohamed, Steven Chalamila na Modestus au tuwaambie nini wazazi na ndugu zao Deus Soka, Emanuel Mbise, Jacob Mlay, Shadrack Chaula na John Kipanya"
"Au maaan ya maridhiano ilikuwa ni kupeana michongo ya pesa tu?"
Magufuli alitaka kuongezewa muda wapi, sana sana wapiga zumari wote wakutaka aongezewe muda hawakurudi bungeni.Yani Magufuli alivyotaka kuongezewa muda FAM na genge lake walipiga kelele sana, ila Yeye FAM hataki pawe na ukomo wa madaraka kwenye chama.
Hii ni demokrasia gani? Demokrasia inaanzia kwa vyama vya upinzani kuonyesha mfano. CHADEMA inapoteza muelekeo, sijui kama wakitangaza maandamano tena kama kuna watu wenye akili zao watatokea.
Ni vizuri kama Watanzania tumeyajua haya ndani ya muda huu. Tushajua sasa FAM na genge lake sio watu wa kuwaamini tena, siku hizi hata akina MMM na Bonge wa Mayai wamepoteza mvuto kwa haraka sana.