Tundu Lissu bado unayo nafasi ya kurekebisha hotuba yako! Usiongelee Macro issues kupita kiasi!

Mambo ya kurekabishwa na Rais ajae wa Upinzani au wa CCM (siyo Magufuli) yaliyoharibiwa na Awamu hii ni mengi sana hayawezi kuorodheshwa kwenye hotuba moja. Mengi unayotaja hapa Serkali ina taratibu nzuri sana za kufuata lakini uongozi wa Awamu hii iluamua kuachana na hizo taratibu na kufuata mawazo ya mtu asiye na uzoefu. Hata mengi yamepuuzwa ingawa yapo kikatiba ikiwa ni pamoja na Katiba yenyewe kusiginwa kumjenga mtu asiye na uwezo aonekane anafaa kwa sababu ni wa Chama chetu tawala. Mfano utaratibu wa Serkali kila mfanyakazi wake lazima apate nyongeza ya mshahara kila mwaka na kila miaka mitatu afikiriwe kupandishwa cheo/ngazi lakini haya hayakufanyika licha ya kilio cha kila mara cha wafanyakazi. Zanzibar sasa huu ni mwaka wa nne wazee wote wanalipwa pensheni haijalishi kama walikuwa watumishi, wakulima, wavuvi au wazururaji huku bara sera ya wazee iko toka Awamu ya Tatu lakini hali ya wazee bado mbaya sana ingawa kuna Wizara ya Wazee na wafanyakazi lukuki wakilipwa mishahara minono. Ni kweli wafanyakazi wengi walitumbuliwa pamoja na taaluma zao lakini hili lilifanyika ili kuwapatia ajira watu fulani wengi wao wakiwa hawana taaluma wala uzoefu wa kazi. Vyeti feki wengine hawakuguswa na wanaendelea na kazi hsdi leo.
 
We msomi hutujui sisi WaSwahili wengi ambao ni wapiga kura. Macro issues hatuzielewe - chambua chambua - mfano tu angesema tu "nitadeal na vyeti feki kwa wanasiasa" yaani tungeshangilia sana na mpaka hapo angeshapata hata kura milioni moja!

There's plenty of time kwa hayo yote kusemwa....

Itoshe tu kuelewa kuwa "sisi waswahili" tumemsikia Tundu Lissu kaweka "NIA" ya kuwania Urais wa Tanzania na kwa kweli ndivyo watu wanavyoelewa katika hatua hii ya mwanzo....

Na "hawa waswahili" they know exactly kuwa, kampeni za kila mgombea nafasi ya uongozi hazijaanza. Zikianza tutawategea masikio kiwasikiliza....
 
Lissu hana usomi wowote ana Masters ya Law wakati ambapo Rais Magufuli ana PHD ya Chemistry na ni mmoja wapo wa wanakemia mkubwa Tanzania ambao wamepata nafasi ya kupractice yale waliyo yasoma kinadharaia.

Lissu ana akili za kitoto sana, kwani hata kwenye arguments zake anaonyesha namna gani ana chuki kubwa sana zidi ya Rais Magufuli personally. Kisa cha yeye kumchukia Rais Magufuli ni uwezo wake wa kushinda kila kitu. Kila kitu Lissu na wenzake walichopanga kumzuru Rais Magufuli kimeshindikana kwa kishindo kikubwa sana, kwani alifikiri kuwa yeye ndiyo mjua sheria babu kubwa kuliko watanzania wote wengine. Kwa bahati mbaya au nzuri amejikuta kuwa yeye ni loser, kwani kuna majembe ya kitanzania ambayo yanajua sheria zaidi yake. Kwenye mambo haya yanayo husu sheria yeye anaonekana kuwa ni amateur, ni mtoto wa shule bado.

Tatizo letu hapa ni kuwa kwa vile watanzania wengi wanao tawala media ni wababaishaji, na wao kwa elimu yao ndogo na kutojiamini kwao, wanamwona Lissu kwa kelele zake kama mtu aliyebobea sana kwenye maswala haya wakati kumbe ni boya tu linalo elea majini. Lissu hajui kitu na wala hajui sheria vizuri. Amejaa mbwembwe tu.

Kwa vile tunamijitu yenye ukosefu wa mawazo mapana ya hiyo inayo miliki media, haina shughuli nyingine zaidi ya kumpa sifa Lissu ambazo hastahili. Lissu ana akili na uzoefu gani wa kushindana na mtu kama Prof. Kabudi? Kwa sisi tuliobahatika kwenda shule za uhakika na uzoefu wa maisha mengine zaidi ya yale Tanzania, tunamwona yeye kama kikaragosi tu asiye jua maisha ulimwenguni jinsi yalivyo. Hotuba yake hii ni ya kitoto sana mpaka nyie wafuasi wake mnaona kuna wajibu wa kujaribu kumrekebisha.

Mimi katika uhai wangu sita mwona Lissu anakuwa Rais wa Tanzania. Na nina uhakika mkubwa hata kuwa Rais wa watanzania hata mara moja. Kwanza akirudi maisha yake yenyewe yako hatarini. Yeye na dereva wake ni mashahidi wakubwa sana wa kesi yake ya kupigwa risasi. Kwa vile ni mashahidi namba one watanzania walio husika na shambulio lake wata mmaliza tu, mwache aje.

Sababu nyingine za kuwafanya watanzania kummaliza kwanza ni;
uongo wake alioutoa na ambao anaendelea kuutoa kuhusu nchi yetu na wananchi kwa ujumla,
jingine ni kwamba amelishutumu kulidhalilisha sana jeshi letu la polisi na mahakama kwa ujumla na Bunge letu tukufu na Speaker wetu hawakuachwa salama kwenye tuhumabzake na mwisho ni chuki zake binafsi kwa Rais wetu mpendwa Magufuli na kadhalika na kadhalika.
Kwa sababu hizo hawezi kuwa Rais wa watanzania ng'o!

Siku atakayo tua tu nchini atakamatwa na kutiwa kizimbani kwa makaosa ya usaliti wa Taifa letu na utoro wa kesi aliyo nayo. Sidhani kama mahakama itampa ruhusa kutoka kwa dhamana, sijui. Na uchaguzi nafikiri safari hii atausikia kwenye bomba. Ni mtu hoppless sana.

Ndiyo maana amehangaika sana mpaka kwenda kuwa consult Amnesty International kuwaomba wamsaidie kuipa pressure serikali yetu ili Rais Magufuli ampe garantii ya maisha yake nchini. Kama yeye kwa matendo yake anajiona ni mtu safi kwanini ahofie kurudi? Anajua kuwa ametenda mabaya ndiyo maana anajitahidi kupata huruma ya wanachi na mataifa mengine.

Kwa mimi namwona Lissu ni marehemu tayari. Ni mtu ambaye amesha kufa. Lissu amekufa kifo cha kujiua mwenyewe kisiasa na kimaadili. Ni mtu ambaye ni juha na hopless. Anafanya mambo kwa kubahatisha huku akijua kuwa karata zote haziko upande wake.

Sidhani kama kuna kitu kikubwa ambacho atawaambia watanzania na wakamsikiliza. Ni makachero wake tu kama wewe mleta mada ndiyo labda mtasikiliza na nyie mmko wachache sana. Ni nini hasa alicho kuwa ncho Lissu? Domonla kupayuka? Kutengeneza arguments zenye substance hajui. Arguments zake ni kama za mtoto ambaye yuko kwenye shule ya chekechea. Ana arguments za kuzomeana kama watoto wadogo wanavyo fanyina wenyewe kwa wenyewe. Sasa inategemea mtu kama huyu ataweza liongoza Dola? Thubutuuuu!

Mimi sijawahi kusikia mtu mwenye level ya Masters kwenye international Arena anatoa utumbo wa kuwahutubia Audience kwamba Rais Magufuli hajui kiingereza, utafikiri yeye ndiyo anakijua kiingereza vizuri kuliko wengine wote. Kwa uelewa wangu mtu ambaye ameishi na kusoma Amerika kama yeye nafikiri kiingereza chake kingekuwa zaidi ya kile anacho kikoga nacho, kiingereza chake ni cha kuokoteza. Lisuu anakiingereza cha kufikiri na sio cha kutoka tumboni. Kwa mwana sheria kama yeye alitakiwa azungunze kiingereza ambacho kina miminika kama maji ya mto na sio kama matone ya maji ya bomba.

Kiingereza chake kina Eeh eeh nyingi! Nakumbuka ile Interview yake kwenye Hard Talk wakati yule mtangazaji alivyo mwuuliza swali naye kubabaika katika kujibu kwa kutafuta maneno ya kusema mpaka yule mtangazaji alipo mwambia aseme haraka maana mda unaenda. Akajikuta anaongea mambo ambayo ni irrelevant kulingana na swali. Alijitia aibu kubwa sana. Na aliwatia wana sheria aibu kubwa.

Sisi wana harakati tutazitumia arguments zake zote alizozitoa ili kuwaonyesha watanzania kiasi gani alivyo kuwa msaliti hatari kwa Taifa letu wakati wa kampeni, kama CHADEMA wataamua kumweka yeye kuwa mgombea wao wa Urais. Tuna silaha kali sana za kumpiga Tundu Lissu kwenye kampen. Tutakuwa kila mara tunawapeperushia watanzania ili wazisikilize na kuona maovu yake.

Hiyo ndiyo maana yangu ya kusema kuwa yeye ni marehemu. Kisiasa hatafanya kitu nchini. Tuta mdhihaki na kumkejeli mpaka ataiona hii nchi chungu na kurudi huko huko kwa mabeberu wake.

Kwanza angejua alivyo kuwa limbukeni asinge enda ishi kwenye nchi kama Belgium. Belgium ni nchi gani ya mtu kama yeye kuishi Ulaya? Belgium ni nchi moja wapo masikini katika bara la Ulaya. Maisha ya Belgium hata yale ya baadhi ya nchi za Afrika zinaishinda. Kwa vile yeye haijui Europe vizuri kwake anaona sawa tu. Na ndiyo maana wanashindwa hata kumtengenezea viatu ambavyo yeye anaweza kuvivaa, mpaka aende Germany!

TUNDU LISSU AMEKWISHA KAZI!!!!!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Du! Unaweza kuja kuwa mkimbizi hivi hivi!
 
Tumefikia hatua ya mwananchi mwenyewe anamfundisha mwanasiasa mambo ya kuongea ili aweze kudanganyika vizuri.

Kuna watu walikuwa na matumaini makubwa sana kwa Magufuli aliposhinda urais ila sasa wanakiri walikosea,sasa sijui wengine wanaona kwa Lissu kuna kipi ambacho anaweza kufanya kwa yale yaliyomshinda Magufuli.
 
Wewe ndiye unaweza ukawa Rais mzuri. Kumbe unaelewa!
 
Mleta mada uko sahihi, speech ya Lissu ilikuwa nyepesi sana.
Huwezi kuikita speech ya kuombea uraisi kwenye mambo ya siasa, katiba haki za binadamu na kuneglect uchumi au issurs zinazowahusu wananchi kuweka mkono kinywani
Lissu hajazungumzia ajira za vijana wetu, maslahinya wafanyakazi, suala la ulipaji madeni HESLB linavyoumiza watu, Mazao ya wakulima, korosho, mbaazi, kahawa, pamba etc.
Huwezi kuzungumzia uraisi bila kuzungumzia hali ya ufisadi, maslahi ya waliovunjiwa nyumba kinyume cha sheria

Next time Lissu ajipange, Speech yake ya juzi haina substance ni nyepesi kuliko unyoya
 
Good!
 
TAL ana masters - Jiwe ana Phd. Nani msomi?
Kuwa na PhD wakati hujawahi ku publish hata journal article moja iliyohakikiwa unakuwa huna tofauti na diploma.. kwa hiyo jiwe hana tofauti na mealimu wa sekondari maana hana publication inayoeleweka kwenye jarida.. hata la uswahilini.. unaiitaje hiyo ni PhD? Wenye PhD wako Google Scholar.. ukigusa tu masayansi tele tele yanamwagika.. tafuta jina la jiwe kama utaona kitu..
 
Mambo mazuri kuyaaongezea. Pia akiongezea na
Kwa kweli mamnbo mazuri hayo. Pia akitia msisitizo namna atakavyokuza uchumi( economic growth), hasa kama fedha yetu na mikopo itaelekezwa katika maswala yatakayokuza uchumi, kama:
1) Human capital development: elimu yenye mitaala ya kuwapa vijana stadi za kuzalisha mali, kujiajiri na kadhalika. Sio elimu ya degree za nadharia peke yake. Pia huduma nyingine nyeti kama afya bure kwa vijana ili wakuwe wakiwa bomba waweze kuchangia uchumi. Elimu na afya kwa wanawake ambao no asilimia 50 ya population, ili tuupate vema mchango wango wao katka uchumi. Haya wasomi wa CHADEMA nyambulisheni hili ili liingie katika hotuba.
2) infrastructure zinazolenga kuchochea ukuaji wa uchumi: kama ni reli au barabara zitachocchea uchumi kwa namna gani, na kwa kiasi gani. Sio barabara na viwanja ambavyo havina mantiki bali kuserve watu wachache.
3) chagua kero kuu kama 10 zilizokukwaza sana, uruke na hadi ya kuzitatua ukitoa na muda kamili.
"Macro" issues ni vizuri kuzitaja, lakini hawa wapiga kura wa kawaida hawayaoni sana hayo, japo ilikuwa ninhotuba makini sana.
Kila la kheri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…