Pre GE2025 Tundu Lissu: BAWACHA kama mnataka fursa za uongozi Bungeni au Udiwani mchagueni Celestine Malley-Simba

Pre GE2025 Tundu Lissu: BAWACHA kama mnataka fursa za uongozi Bungeni au Udiwani mchagueni Celestine Malley-Simba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mbangaizaji wa Taifa

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
493
Reaction score
844
Anaandika Tundu AM LISSU.

====
" Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa BAWACHA kama wewe unataka au mwanamke mwenzako anayefaa nae apate fursa za uongozi bungeni au kwenye udiwani miaka ijayo, nakushauri upige kura ya mabadiliko kwenye Uchaguzi wa BAWACHA kesho na Uchaguzi Mkuu wa chama tarehe 21 Januari.

Ni kura ya mabadiliko pekee itakayoondoa umalkia katika ubunge na udiwani wa viti maalum katika chama chetu.

Ni kura ya mabadiliko pekee itakayohakikisha wanawake wengine wengi nao wanapata fursa za kuwa wabunge na madiwani wa viti maalum.

Celestine Malley-Simba ameweka msimamo wake wazi kwamba atapiga kura ya mabadiliko tarehe 21 Januari.

"Na mimi rasmi natangaza kumuunga mkono"

Lakini mimi sio mpiga kura kesho, na wala viti maalum havinifaidishi mimi binafsi ila wewe uliye mpiga kura wa BAWACHA kesho na viti maalum vya ubunge na udiwani vinakuhusu, nenda kaunge mkono mabadiliko ndani ya chama chetu.

Piga kura yako kwa Celestine Malley-Simba kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa "

Pia soma
> Uchaguzi 2025 - Lissu: Tutaweka ukomo Ubunge Viti Maalum isiwe kikundi cha wale wale miaka yote

IMG-20250115-WA0007.jpg


IMG-20250103-WA0235(2).jpg

===​
Baada ya Deogratias Mahinyila kutangaza hadharani anamuunga mkono Tundu Lissu huku na yeye akiomba achaguliwe kwenye Uenyekiti wa BAVICHA ili wasaidiane na Lissu na Heche katika Ujenzi wa Chama na Wajumbe wakakubaliana nae na kumchagua kwa kura nyingi,

Sasa ni zamu ya Uenyekiti wa BAWACHA Taifa na tayari Mgombea makini wa nafasi hiyo Ni Celestine Simba ameshatangaza pia kumuunga mkono Tundu Lissu na John Heche.

Hiki ndicho alichokiandika Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ajae baada ya Celestine Simba kutangaza kumuunga mkono yeye na John Heche.

Mungu mwenye Nguvu atasimama awamu hii CHADEMA

Pia soma Uchaguzi 2025 - Spika wa Bunge la Wananchi Selestine Simba atangaza kumuunga mkono Lissu huku akitangaza kugombea Uenyekiti BAWACHA Taifa ili kujenga CHADEMA mpya
 
Back
Top Bottom