Pre GE2025 Tundu Lissu: BAWACHA kama mnataka fursa za uongozi Bungeni au Udiwani mchagueni Celestine Malley-Simba

Pre GE2025 Tundu Lissu: BAWACHA kama mnataka fursa za uongozi Bungeni au Udiwani mchagueni Celestine Malley-Simba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii haijakaa vizuri. Makamu Mwenyekiti anampigia debe wazi wazi mmoja wa wagombea? Akiwa Mwenyekiti si ndio itakuwa balaa! Na hawa ambao wametangaza loyalty kwa mgombea, wataweza kweli kum hold accountable akikosea? Sio ishara nzuri.

Amandla...
Well! huyu alisema ana afadhali kuliko Mwenyekiti. Lema kasema kuhusu yake na ya Msigwa.
Mbowe kazuia uchaguzi wa Rose Mayemba.
 
..hapa Lissu amekosea, unless hao wagombea wengine wanafanya kampeni za wazi kwa niaba ya Mbowe.
Mkuu, aliyeanzisha ni Mbowe. Godbless Lema kazungumzia jinsi '' Mwenyekiti' alivyomzunguka.
Msigwa alilalamika jinsi '' maagizo kutoka juu'' yalivyomuumiza
Rose Mayemba hadi leo kawekwa kampuni

FAM ana operate kwa remote! akiwatumia akina Kigaila ndio maana hakuweza kufanya lolote kuhusu COVID
 
Katika mahojiano yake, Heche amekataa kutoa yale aliyoona kama siri za vikao vya CDM.

Amandla...
JokaKuu
 
..kuna kitu Freeman Mbowe na timu yake wamekikosa, au wamekosea, na kupelekea " "hali ya hewa" ndani ya Chadema kuchafuka kiasi hiki.
Mkuu, tupo jamvini muda mrefu. Kama utakumbuka nimekuwa nam criticise Mbowe kwa miaka 10 iliyopita.
Si kwasababu nyingine bali michezo yake kwa kutumia '' Mbowe machinery''

This time around , Mbowe Machinery zimeshindwa kufanya kazi.

Ukitaka kujua hilo, TAL kwa muda mrefu amekana kugombea Uenyekiti akachukua Fomu ya umakamu. Dakika za mwisho akabadili uelekeo.Hii ilikuwa deliberately ili kukwepa ''Mbowe Machinery ''

So FAM amekutwa 'flat footed '' ndio maana tunaona kama amekosea!
 
Mkuu, aliyeanzisha ni Mbowe. Godbless Lema kazungumzia jinsi '' Mwenyekiti' alivyomzunguka.
Msigwa alilalamika jinsi '' maagizo kutoka juu'' yalivyomuumiza
Rose Mayemba hadi leo kawekwa kampuni

FAM ana operate kwa remote! akiwatumia akina Kigaila ndio maana hakuweza kufanya lolote kuhusu COVID
It does not make sense. Mbowe kaamka siku moja tu akaamua kuwa hawapendi Lissu, Msigwa, Heche na Lema? Ni lazima kuna kitu alisikia kikamfanya akose imani nao.
Msigwa alipommwagia sifa JPM, Mbowe hakumfanya kitu. Msigwa alipotofautiana wazi na wenzake ( ikiwa pamoja na Lissu), Mbowe hakumchukulia hatua.
Kuna mtu mmoja wa CCM alisema kuwa mazungumzo na Msigwa yalianza mapema tu. Bila shaka Mbowe alipata fununu. Na alipotimkia CCM ndio ikawa uthibitisho wa hisia zake. Lissu na Rose ni watu wa karibu sana na Msigwa. Kwa nini Mbowe asiwatilie shaka kuwa wamekuwa corrupted. Kuwa zile kelele za pesa za Abduli alizokuwa anapiga Lissu ilikuwa ni njia ya kuwaficha wanaonufaika ( Msigwa na pengine Rose).
Suala la Covid sio la Kigaila. Na Mbowe alichukua hatua zinazostahili dhidi yao. Lakini bado mnataka kumuangushia jumba bovu.

Amandla....
 
Hoja ni kwamba Makamu anafanya kampeni wazi. Nimekujibu kwamba Mwenyekiti ndiye muasisi wa kampeni za ''wazi'' akitumia remote zake za sekretariati
Na kwa kufanya hivyo ana stifle competition. Kila mmoja anajua katika vyama vya siasa vyote vinakuwa na preferred candidate. Hata Lissu aliposhindana na Nyalandu ilijulikana kuwa yeye ndio preferred candidate. Mimi sikatai Makamu kumpendelea mmoja wa wagombeaji. Ninachokataa ni kuonyesha kabisa kuwa akishinda ni kutokana na endorsement yake. Huyu mama akishinda priority yake itakuwa kujikomba kwa Lissu na sio Bawacha. Trumpian 101.

True! kwamba hata TAL akishinda, viongozi wanaweza kutokuwa 'loyal'' wakawa ''submissive''
 
Mbowe kaamka siku moja tu akaamua kuwa hawapendi Lissu, Msigwa, Heche na Lema? Ni lazima kuna kitu alisikia kikamfanya akose imani nao.
Inaonekana kulikuwa na ''internal rift''. Swali kwanini?
Msigwa alipommwagia sifa JPM, Mbowe hakumfanya kitu. Msigwa alipotofautiana wazi na wenzake ( ikiwa pamoja na Lissu), Mbowe hakumchukulia hatua.Kuna mtu mmoja wa CCM alisema kuwa mazungumzo na Msigwa yalianza mapema tu.
Hii inaonyesha kufeli kwa leadership! Mwenyekiti aliachia hali hiyo ambayo sasa inamrudi
Bila shaka Mbowe alipata fununu.
Kama alipata fununu alitakiwa afanye jambo!
Lissu na Rose ni watu wa karibu sana na Msigwa. Kwa nini Mbowe asiwatilie shaka kuwa wamekuwa corrupted. Kuwa zile kelele za pesa za Abduli alizokuwa anapiga Lissu ilikuwa ni njia ya kuwaficha wanaonufaika ( Msigwa na pengine Rose).Suala la Covid sio la Kigaila. Na Mbowe alichukua hatua zinazostahili dhidi yao. Lakini bado mnataka kumuangushia jumba bovu.
Kwanini Rose Mayemba na Si Ezekiel Wenje ambaye ni rafiki wa Mtoto wa Ikulu!
Amandla....
 
Inaonekana kulikuwa na ''internal rift''. Swali kwanini?

Hii inaonyesha kufeli kwa leadership! Mwenyekiti aliachia hali hiyo ambayo sasa inamrudi

Kama alipata fununu alitakiwa afanye jambo!

Kwanini Rose Mayemba na Si Ezekiel Wenje ambaye ni rafiki wa Mtoto wa Ikulu!
Msigwa ni tofauti na Abduli. Ni tofauti hata na Covid-19. Msigwa anafanya juhudi za waziwazi kubomoa CDM. Kitu ambacho Covid-19 hawafanyi. Na sijamsikia Abduli akifanya hivyo hadharani. Rose kuwa mshiriki wake wa karibu kumemponza. Na inaelekea bado yuko karibu nae. Aidha, according to Wenje uhusiano wake na Abduli sio wa muda mrefu. Anadai walikutana kwenye tafrija ndio waka Bond.

Kuhusu ku act, sio rahisi kama unavyosema. Hasa inapokuwa watu kama Lissu na wenzake. Hamna ambae angeamini kuwa walitaka kufanya mapinduzi. Njia bora zaidi ilikuwa ni kuwabana mpaka ama watoke wenyewe au warudishe ndani makucha yao. Ni lazima anakumbuka yaliyo wakuta walipotaka kuwashughulikia Zitto na wenzake.

Kwenye hili inaweza kuonekana kuwa ameshindwa, lakini in the wrong run watu watamuelewa.

Amandla...
 
Hii haijakaa vizuri. Makamu Mwenyekiti anampigia debe wazi wazi mmoja wa wagombea? Akiwa Mwenyekiti si ndio itakuwa balaa! Na hawa ambao wametangaza loyalty kwa mgombea, wataweza kweli kum hold accountable akikosea? Sio ishara nzuri.

Amandla...
Hizi ni kampeni kila mmoja anaruhusiwa kunadi anayemtaka hata kama yeye ni mgombea
 
Hizi ni kampeni kila mmoja anaruhusiwa kunadi anayemtaka hata kama yeye ni mgombea
Nimesema wapi kuwa mtu anakatazwa? Ninachokisema ni kuwa kufanya hivyo hakutoi picha nzuri hasa kwa mtu anayegombea nafasi ya juu kabisa katika chama. Tuseme yule anayemnadi ashindwe na yeye ashinde. Si aliyemshinda mtu wake ataweza kuhofia kuwa hatapata ushirikiano kwa sababu yeye sio chaguo lake? Au kama kweli itagundulika kuwa hatoshi katika hiyo nafasi ataweza kujitetea kuwa anafanyiwa figisu kwa sababu hapendwi.

Amandla...
 
Msigwa ni tofauti na Abduli. Ni tofauti hata na Covid-19. Msigwa anafanya juhudi za waziwazi kubomoa CDM. Kitu ambacho Covid-19 hawafanyi. Na sijamsikia Abduli akifanya hivyo hadharani. Rose kuwa mshiriki wake wa karibu kumemponza. Na inaelekea bado yuko karibu nae. Aidha, according to Wenje uhusiano wake na Abduli sio wa muda mrefu. Anadai walikutana kwenye tafrija ndio waka Bond.

Kuhusu ku act, sio rahisi kama unavyosema. Hasa inapokuwa watu kama Lissu na wenzake. Hamna ambae angeamini kuwa walitaka kufanya mapinduzi. Njia bora zaidi ilikuwa ni kuwabana mpaka ama watoke wenyewe au warudishe ndani makucha yao. Ni lazima anakumbuka yaliyo wakuta walipotaka kuwashughulikia Zitto na wenzake.

Kwenye hili inaweza kuonekana kuwa ameshindwa, lakini in the wrong run watu watamuelewa.

Amandla...

..hudhani kwamba ukaribu wa covid19 na Mwenyekiti katika shughuli binafsi unakidhalilisha chama?

..mgogoro wa Mbowe na Msigwa chanzo chake ni nini? Je, Msigwa amekwenda Ccm kwasababu ya kuhongwa, au kukerwa na tabia za Freeman Mbowe?
 
Hakidhalilishi chama. Halima ni protege wa Mbowe na pengine alimtegemea awe Mwenyekiti wa kwanza wa kike. Kwa sababu hiyo Halima hawezi hata siku moja akawa adui wa Mbowe. Na tukiwa wawazi kosa la Covid-19 ni kukaidi maagizo ya chama chao na kuipa legitimacy Bunge la JMT. Katika muda wote huu hawajawahi kusimama jukwaani kukihujumu chama kama wanavyofanya Msigwa na Peneza. Kwa vile sijui nini kiliwafanya wafikie uamuzi ule, I reserve my judgement.

Kwa kweli sijui wamekosana kwenye nini. Lema ana hint kuwa walitofautiana kwenye maneno. Lakini nadhani ni deeper kuliko hicho. Msigwa ni mshari na anajiamini mno. Inawezekana katika moja ya vikao vyao alimshutumu Mbowe kuwa amelambishwa asali. Hata sijui. Ila nahisi Lissu amehusika.

..hudhani kama mbowe anapaswa kulinda taswira ya chama kwa kujiweka mbali na halima na wenzake?

..pia kuchangamana na halima wakati kuna kesi mahakama huoni kama kunajenga mashaka kuhusu jinsi kinamama hao walivyofika bungeni?
 
Anaandika Tundu AM LISSU.

====
" Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa BAWACHA kama wewe unataka au mwanamke mwenzako anayefaa nae apate fursa za uongozi bungeni au kwenye udiwani miaka ijayo, nakushauri upige kura ya mabadiliko kwenye Uchaguzi wa BAWACHA kesho na Uchaguzi Mkuu wa chama tarehe 21 Januari.

Ni kura ya mabadiliko pekee itakayoondoa umalkia katika ubunge na udiwani wa viti maalum katika chama chetu.

Ni kura ya mabadiliko pekee itakayohakikisha wanawake wengine wengi nao wanapata fursa za kuwa wabunge na madiwani wa viti maalum.

Celestine Malley-Simba ameweka msimamo wake wazi kwamba atapiga kura ya mabadiliko tarehe 21 Januari.

"Na mimi rasmi natangaza kumuunga mkono"

Lakini mimi sio mpiga kura kesho, na wala viti maalum havinifaidishi mimi binafsi ila wewe uliye mpiga kura wa BAWACHA kesho na viti maalum vya ubunge na udiwani vinakuhusu, nenda kaunge mkono mabadiliko ndani ya chama chetu.

Piga kura yako kwa Celestine Malley-Simba kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa "

Pia soma
> Uchaguzi 2025 - Lissu: Tutaweka ukomo Ubunge Viti Maalum isiwe kikundi cha wale wale miaka yote
Baada ya Deogratias Mahinyila kutangaza hadharani anamuunga mkono Tundu Lissu huku na yeye akiomba achaguliwe kwenye Uenyekiti wa BAVICHA ili wasaidiane na Lissu na Heche katika Ujenzi wa Chama na Wajumbe wakakubaliana nae na kumchagua kwa kura nyingi,

Sasa ni zamu ya Uenyekiti wa BAWACHA Taifa na tayari Mgombea makini wa nafasi hiyo Ni Celestine Simba ameshatangaza pia kumuunga mkono Tundu Lissu na John Heche.

Hiki ndicho alichokiandika Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ajae baada ya Celestine Simba kutangaza kumuunga mkono yeye na John Heche.

Mungu mwenye Nguvu atasimama awamu hii CHADEMA

Pia soma Uchaguzi 2025 - Spika wa Bunge la Wananchi Selestine Simba atangaza kumuunga mkono Lissu huku akitangaza kugombea Uenyekiti BAWACHA Taifa ili kujenga CHADEMA mpya
Asante Lissu
 
..hudhani kama mbowe anapaswa kulinda taswira ya chama kwa kujiweka mbali na halima na wenzake?

..pia kuchangamana na halima wakati kuna kesi mahakama huoni kama kunajenga mashaka kuhusu jinsi kinamama hao walivyofika bungeni?
Hapana. Inabidi tukubali kuwa Mbowe na wenzake ni binadamu kama sisi. Hivi Halima angekuwa mwanae tungemtaka ajitenge nae?

Hata hao ambao wake zao ni sehemu ya Covid-19 tunawaonea tu. Kuwa wamoja katika ndoa sio lazima muwe na mtazamo unao fanana!

James Carville ni strategist mkubwa wa Democrats lakini mke wake ni Republican dam dam. Ndivyo inavyopaswa kuwa.

Amandla...
 
Mkuu JokaKuu,
Hivi unadhani Lissu na Lema hawawasiliani na Msigwa? Hawatembeleani? Msigwa ni mtu aliyehusika sana katika kumfikisha Lissu Nairobi. Itakuwa un realistic na unfair. Lakini baada ya kusema hayo, unamkumbuka yule mwandishi wa habari aliyemwambia Mbowe kuwa alipata document ya kikao cha Kamati Kuu ya CDM kutoka kwa kada mkubwa wa CCM. Mbowe alipombana akakiri kuwa huyo kada ni Msigwa. Mbowe akamuuliza Msigwa ni rafiki wa nani? Kwa hali hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa mmoja wa marafiki wa Msigwa wana share nae document za CDM. Sasa hapo nini ni kibaya zaidi kati ya ku share document za chama na adui wa chama na kumualika Halima katika sherehe ya ufunguzi wa Kanisa?

Amandla...
 
Back
Top Bottom