..Nashukuru kwa jibu hili.
..lakini bado najiuliza ni wapi Mbowe amekosea mpaka kusababisha hali ya hewa kuchafuka ndani ya Chadema?
..Au wewe ungekuwa Mbowe ungefanya jambo gani tofauti ili kui-contain hali iliyojitokeza?
..Mbowe ameshafanya press kadhaa lakini sina uhakika kama ameweza kuwashawishi waliomtupa mkono.
Cc
Nguruvi3,
Fundi Mchundo,
Tindo
Baada ya kumsikiliza Lema Jana, kosa kubwa la Mbowe nikutaka kuwasaliti wenzake na kuwatupa nje ya chama, alikua anafanya kuwazunguka lakini bahati mbaya wamemgundua mapema.
Hebu waza kwa nini Mbowe ampigie simu Bob Wangwe agombee Kanda ya Serengeti na amuunge mkono Ili amshinde Heche?.
Heche alikua na kosa gani lakufikiria kumtupa nje ya ulingo wa siasa?.
Mbowe alienda Mbeya akawambia wana Mbeya wakipata hata viti 20 vya uwenyekiti vinatosha, hivi CDM Niyakusema viti 20 vinatosha kweli Mbeya?.
Mimi ningekua Mbowe ningeomba msamaha kwa wenzangu ambao tunasukuma nao gurudumu. Na kuamua kukaa pembeni na kukisaport chama nikiwa mjumbe tu wa kamati kuu.
Hii ingeleta heshima kubwa kwake, kwa sababu haya yote yanayotokea alie yasababisha kwa kiasi kikubwa ni Mbowe mwenyewe.
Ukizingatia pia majira na nyakati za sasa vijana wengi wa miaka ya 90/2000 na watu wa makamo wenye miaka 45 kushuka chini wanahitaji aggressive politics baada yakuona siasa za kiiplomasia zimeshindwa na mtu anaeziweza hizi kwa kiasi kikubwa ni Lissu/Heche/Lema.
Jambo lingine kwenye Press zote Mbowe alizofanya anajitetea tu na kujibu tuhuma anazopewa, hakuna mahala ambapo Mbowe anasema akiogezewa miaka Mingine mitano atafanya nini!.
Hata wafuasi wa Mbowe ukiwauliza Mwenyekiti atafanya nini jipya akipewa miaka migine mitano?.
Jambo gani mwenyekiti ambalo hakufanya miaka 21 iliyopita ambacho anahitaji akitimize sasa?.
Hakuna anaejibu kuanzia Mbowe mwenyewe mpaka wafuasi wake. Kwahio hilo linawapa watu wengi mashaka .
Jambo lingine tujiulize kwa nini Mbowe haonekani kukemea rushwa hadharani kama wafanyavyo wenzake?.
Kwa nini walirekodi kikao cha kamati kuu wakati wanamuhoji Lissu kuhusu tuhuma zake za watu kupewa rushwa, na jambo ambalo lilikua halijawahi kutokea huko nyuma?.
Kwa nini Mbowe hakuwataka Msigwa, Lema, Heche kwenye uongozi wake unaokuja hasa wawe wenyeviti wa Kanda?.
Kwa nini Mbowe alikua radhi kuwapoteza hao wakina msigwa lakini yupo radhi kuwa retain Mdee na wenzake?.
Mwisho wasiku nyakati haziko upande wa mwenyekiti na ushahidi wa mazingira unaonyesha ana agenda nyingine iliyo nyuma ya pazia ambayo nikutomtengenezea Samia mazingira magumu ya siasa.
Mwisho, tunaomba Mwenyekiti apumzike, tusingependa ashindwe kwenye sanduku la kura kwa sababu itaharibu Legacy yake ya Miaka 21.