Hakuna anaejali upuuzi wa Chadeka just a useless bunch.
Naona unanikaribisha ukumbini kwako kiaina, lakini siyo leo, shasema hivyo tayari.
Nimenyanyua hako kamstari kako kamoja kwa mksudi kabisa; lakini usinipange kuwa nipo huko CHADEMA, kama nisivyopenda kukupanga wewe kuwa upo huko kwenye chama kilichooza, lakini bado unakishabikia sijui kwa sababu zipi hasa!
Mara zote siku hizi nasema hivi kuhusu hii CCM yako ilivyo sasa: niko radhi chama chochote kile cha upinzani, kikiweza kuwaondoa hawa wanao tufanya kuwa mateka wao, nitawaunga mkono. CCM kimekuwa ndiyo adui mkubwa wa nchi yetu sasa hivi. Sioni adui mwingine yeyote zaidi ya CCM anayetukabili sasa hivi.
Tendo tu, la kutuzuia tusiwaondoe madarakani kwa njia yoyote ile, ni tendo tosha kabisa la kuwaona hawa kuwa maadui wa nchi yetu
Sasa wewe hapa, unapokuja na kuwabeza CHADEMA, pamoja na mapungufu yao; lakini ndio pekee kwa sasa, angalao wanaoweza kufurukuta na kuwasumbua hawa CCM; halafu wewe unakuja na kujiona ni bora ya kuwa na hao wanaotuteka?
Ndiyo, naelewa wazi kabisa, kwamba huko ndani ya CCM hiyo mbovu, wamo ambao wanaumia kama sisi wengine tulio nje ya hicho chama, lakini hawaezi kufurukuta, na kuleta mageuzi yoyote ndani ya chama chao. Tuwasaidie, kwa njia yoyote ile, hata kama ni kuwatia moyo CHADEMA waweze kulegeza mkono wa hao wabaya waliomo ndani ya CCM na kuwapa nafasi wanaoshindwa kufurukuta huko huko.
Inawezekana kabisa bado sikuelewi unacho maanisha hasa ni nini, kwa maana nakuona kama unajichanganya tu mwenyewe katika maandishi yako juu ya jambo hili.
Utaniwia radhi kwa makosa ya uandishi, kwa sababu nakwenda mbio tu, kwenye majibu kama haya ambayo sina akili tulivu ya kuyajengea hoja.