Pre GE2025 Tundu Lissu: Bilioni 54 za kununua pikipiki "SSH 2025" zimetoka wapi?

Pre GE2025 Tundu Lissu: Bilioni 54 za kununua pikipiki "SSH 2025" zimetoka wapi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hebu tuangalie halafu tusaidiane



Pikipiki zimeandikwa SSH2025 na zina picha yake, hatujaanza kampeni, mama ameanza kampeni zaidi ya mwaka na nusu kabla ya uchaguzi. Kama ameanza yeye na sisi tuanze, amefungulia mlango.

Kila kata ya mkoa wa Singida imepewa pikipiki kulingana na idadi ya vijiji vyake, mkoa mzima wa Singida zimeletwa pikipiki 700, na Tanzania nzima kila mkoa kapeleka pikipiki 700, na Tanzania bara iko mikoa 26, hivyo fanya pikipiki 700*26 ni 18,200. Ukienda mjini kuafuta pikipiki moja inauzwa milioni 3 mpyaa. Zidisha pikipiki 18,200*3,000,000 ni shilingi bilioni 54,600,000,000.

Bilioni 54 katika nchi ambayo watoto wanakaa chini hawana madawati, mahospitali hayana madawa, hakuna maji ya kunywa, barabara ni mbovu ila kuna pikipiki za kugawa bure za Rais za Tsh. 54,600,000,000

Nyie mnajua maana sizungumzi vitu ambavyo hamvijui, Magufuli si alifanya kampeni, aligawa pikipiki? Kikwete si alifanya kampeni, aligawa pikipiki? Mkapa aligawa pikipiki?

Huyu anatuletea pikipiki, siyo za CCM, zingekuwa za CCM zingeandikwa Chagua CCM etc etc. Hizi zimeandikwa SSH2025, ni za kwake na siyo za Serikali.

Hizo hela amezitoa wapi huyo anayetaka tumuite mama? kumbuka ameuza bandari zetu kwa warabu, ameuza hifadhi ya misitu yetu hekta 9,900,000 kwa waarabu, kiwanja cha ndege cha KIA kauza kwa waarabu, kule umasaini kafukuza wamasai wamepelekwa Handeni ili auze kwa waarabu.

Hii bilioni 54 ametoa wapi kama siyo hii biashara haramu anayofanya na mali za nchi yetu? CCM tuambie huyu mwenyekiti wenu anayetaka tumuite mama ametoa wapi hizi pikipiki hizi 18,200. Ana hela wapi, ana biashara gani?

Mwalimu Nyerere kabla hajafa aliuza " Hivi Ikulu kuna Biashara gani" Samia Suluhu Hassan, Ikulu kuna biashara gani za kukupatia wewe Tsh 54,600,000,000 za kugawa pikipiki Tanzania nzima?


Pia soma: Kuelekea 2025 - Lissu: Wasijifiche nyuma ya msikiti, waje hadharani tuyaseme matendo yao maovu
 
Hebu tuangalie halafu tusaidiane

View attachment 3018313
Hivi kwamfano TAL ndio angegawa pikipiki hata 50 tu zikiwa na jina lake na 2025 hii serikali,sisiemu,yuvisisiemu na tume ya uchaguzi,msajili wa vyama vya siasa,ule umoja wa vyama shikizi,wachungaji na mashekhe siwangeanza kusema ametoa wapi pesa na ameanzaje kufanya kampeni kabla ya muda?🤣🤣🤣 bado tunaenda na mfumo chama na serikali kushika hatamu
 
Ila ikumbukwe Kikwete kwenye wakati wa uchaguzi ule wa Uraisi wake awamu ya ngwee ya mwisho alipo tumia familia yake Riz akiongoza kampeni ilimsumbua sana!!!

Mama Samia kuwa makini
Kumbuka Hilo
 
Unamaanisha amegawa pikipiki kwa kila mtanzania?
Unapo ambiwa deni la taifa trioni kadhaa
Inamaana Kila Mtzd alipata fungu wakati wa mkopo?
Hizo pikipiki wamepewa Machawa
Katazame zinayo piga misele hovyo ndio utajuwa Kila Mtzd Zina muhusu
 
Mimi sio chawa wa huyo mama.

Wanachotia huruma hawa sakapoko (chawa) wa huyo mama hawajui wanasomwa na hakina nani.

JF ni uwanja wa vigogo wa serikali na chama. Hii ndio sehemu ya kuonyesha uwezo wao hawajui tu.
 
Ingekuwa mimi ndio UVCCM ningemtwanga huyo Lissu kwa hoja atie akili
Hebu anza kwa kuwapa hizo mbinu za "kumtwanga huyo Lissu..." Ni hoja zipi hasa unazodhani wanaweza kuzitumia?

Huoni kuwa huyo ambaye wangemkingia kifua kwa hoja hizo ndiye kawaondolea hizo hoja kwa matendo yake yaliyo wazi kwa kila mtu?
 
Back
Top Bottom