Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Anatapatapa sasa ameshindwa kuwa win watz! Hatuhitajj mdahalo sisi bali tunataka utuambie umefanya nini na utafanya nini tukikupa kura zetu! Hatuko kwenye mashindano ya mdahalo!
Sio kwamba hutaki mdaalo ni kwamba unajua uwezo duni alio nao mgombea wenu.
 
Nimekuelewa!

Anachoongea Lissu umekipa rangi ya hadaa! Kuwa ana wahadaa raia wenye elimu ndogo na hana hoja ya msingi. Pia ukaweka ziada inambidi apewe ukweli wake Magufuli ni rais wa hii nchi. Vilevile ukaweka ziada kuwa kufanya mdahalo kwa Lissu ni kufurahisha sintofahamu zake za kichwani.

Lakini mazingira haya yametokea na yanatokea. Tumeshuhudia na imeshuhudiwa vijembe vikirushwa pande zote mbili, kwa Lissu Chadema na kwa Magufuli CCM. Si hivyo tu, bali mpaka wagombea Urais wenyewe wanarushiana vijembe.

Kwa hayo uliyoyaorodhesha kuhusu Lissu ni tunu kwa CCM. Kwa nini msiitumie hii fursa ya dhahabu ya mdahalo kumharibu na kuharibu carrier yake moja kwa moja kuliko ile ya kujibizana na mtu mwenye mental issues kwenye majukwaa?! Naamini hili likitendeka hamtampa tena sikio za kuhangaika naye kwenye vijembe. Kwani umma utakuwa umeshashuhudia.

Nafikiri ni muda wa muafaka wa Magufuli kumuonyesha fahari ni nani kwenye hili zizi. Njia pekee na sahihi ya kuwathibitishia hata kwa wale wenye elimu ndogo kuwa Lissu ana wahadaa ni mdahalo. Na si kitu kikubwa! Ni mdahalo tu!

Ruhusuni mdahalo.
 
Wanataka debate ili wazungu wa Ulaya Wawaone na wajue kuwa pesa wanazowapa zinafanyiwa kazi.

Huwa nawaambia kuwa utendaji wa Magufuli ni mdahalo tosha kabisa.
 
Huyo mjamaa amekulia porini afu anajiona lugha ya kingereza ni kijijini kwao

Kufanya mjadala na mropkaji wa matusi nani atakubali?
Aende ubeligiji akafanye mjadala na robert
Lugha tu na Mzee kupangilia logical sequence ni issues msaidizi wake humprey aligonga zero HKL high school
 
Ni sawa na kusema raisi Magufuli aingie kwenye dimbwi na kucheza vita ya kurushiana matope just for the sake of entertaining Lissu niche crowd of supporters.

Tundu Lissu hana shida ya mdhahalo na wala hana hoja za msingi as yet zaidi ya porojo zisizo na kichwa wala muhimu, shida yake ni kujiweka on per na Magufuli and that line of reasoning is destroying is mental state.

Akuanza leo wala jana hiyo obsession ya kujilinganisha na Magufuli ata alipochaguliwa raisi wa ‘Tanganyika Law Society’ Lissu alikuwa analazimisha kwa nafasi yake akutanishwe na Magufuli na kila anachofanya Magu anapinga to the point of annoying the National security maana mambo mengine ni sentive kama ilivyokuwa kwenye renegotiation ya mikataba.

Deep down Tundu Lissu is just jealous of Magufuli presidency’s.

There is no point of entertaining such a person let his jealous yearn to be considered on equal per with Magu be the cause of his worsening mental state.
 
Pamoja. Naheshimu mawazo yako.
 
Tatizo unaandika kwa mihemko ya Kisiasa, hivi huoni DSM baada ya uboreshaji wa miundombinu ya Barabara foleni imepungua kwa kiwango kikubwa na watu wanafika kwa wakati maeneo yao ya kazi.
 
Sio kwamba hutaki mdaalo ni kwamba unajua uwezo duni alio nao mgombea wenu.
Kwahiyo unataka kusema Lowassa ambaye nae hakutaka mdahalo ile 2015 ni kutokana na uwezo mdogo alionao? na vp wapiga waliyompigia kura hawakuliona hilo?
 
Anatapatapa sasa ameshindwa kuwa win watz! Hatuhitajj mdahalo sisi bali tunataka utuambie umefanya nini na utafanya nini tukikupa kura zetu! Hatuko kwenye mashindano ya mdahalo!
hili utaliuliza kwenye mdahalo wala usijali
 
..jpm anaogopa mdahalo, kwa sababu ana uwezo mdogo sana wa kujenga hoja.

..hata huu utitiri wa wasanii ktk kampeni zake lengo ni kumlinda Jpm asizungumze kwa muda mrefu akatoa boko.

..hana uwezo wa kuzungumza moja kwa moja na wananchi akawashawishi, badala yake anatumia wasanii kuwahadaa.
 
Mi natamani kweli ufanyike mdahalo na sio lazima awepo Magufuli kama Magufuli hataki sio lazima hata 2015 yeye pamoja na Lowassa hawakutaka mdahalo na haikuwa issue. Mdahalo wagombea wengine wapo mdahalo unaweza kufanyika na tukaona huo uwezo wa Lissu.
 
Habari ya wakati huu wadau wa jukwaa hili pendwa.naombeni moderators msiunganishe thread hii na nyingine tafadhari. Jana nilibahatika kuhudhuria kwenye mkutano wa mgombea wa kiti cha urais kupitia Chadema mh. Tundu A. Lissu. Alianza kuhutubia kwa kuomba ufanyike mdaharo kati yake na mgombea wa nafasi ya uraisi kupitia ccm. Nanukuu kauli yake;

“Natoa rai kwa mgombea mwenzangu wa CCM, tukutane kwenye mdahalo. Ufanyike kwa lugha yoyote ile na uendeshwe na wataalam tutakaokubaliana. Ili tuwaeleze na tuhojiwe hadharani na kujibu hadharani mipango na maono yetu. Naamini mwenzagu ambaye ameshakuwa Rais kwa miaka mitano hatakuwa na hofu ya kushindana na mimi ambaye sijawahi kuwa Rais. Tukutane pamoja. Tuache haya mambo ya kuogopana na kuchengana. Nina imani hatakimbia mdahalo. Akiogopa tutahoji majigambo ya usomi wake”.

Neno ‘MDAHALO’ sio geni. Midahalo baina ya wagombea wa nafasi ya urais imekuwa ni jambo la kawaida sana duniani katika kipindi cha kampeni. Nchi zaidi ya 60 duniani wamekuwa na huu utaratibu, pia makundi mbalimbali ya kijamii yamekuwa yakishinikiza midahalo baina ya wagombea. Midahalo huwasaidia sana wapiga kura kuwa informed na kuwafanya wagombea kufocus na policy issues ambazo zipo kwenye ilani zao zaidi kuliko personal issuees. Lakini pia midahalo huchochea uvumilivu wa kisiasa (political torelance). Pia midahalo huwafanya wagombea kujikita kwenye issue za muhimu ambazo muda mwingine wameshindwa kuzieleza vizuri majukwaani wakati wa kampeni. Nakumbuka nchini marekani, mgombea wa chama cha Republican bwana Bob Dole mwaka 1996 alipohojiwa umuhimu wa mdahalo alisema “They force us to think”. Lakini pia hata Bill Clinton rais wa marekani 1993-2001 alisema
I am convinced that the debates I went through…..actually helped me to be a better president”.

nikirudi kwenye Hoja ya lissu. hoja hii imepokelewa katika mitazamo tofauti tofauti katika mitandao ya kijamii na hata katika mijadala kwenye makundi ya watu. Wapo wanaipokea hoja hii kwa mikono miwili wakiamini kwamba mdahalo ni muhimu sana kwa wagombea katika nafasi ya uraisi, lakini pia kuna baadhi ya watu wameonekana wakipinga hoja hii kwa,madai kwamba magufuri ni mtendaji na sio msemaji hivyo yeye anajikita kwenye kazi tu na sio porojo. Wengine wamesema Wananchi wanataka sera zinazo telelezeka sio mdahalo, Sera za majukuani ni zaidi ya mdahalo. Wengine wameenda mbali zaidi wakisema magufuri sio level ya kushindana kwenye mdahalo na lissu labda kibajaji au msukuma. Katika post ya polepole kwenye mtandao wa tweeter amesema



Kutokana na hoja hizi nimeona ni vema tueleweshane hapa kwakujenga hoja za msingi bila kutumia lugha za matusi kwakujibu maswali haya

  • Je kwanini baadhi ya watu wanakataa mdahalo?ni athari zipi hujitokeza endapo taifa likiwa linapuuza midahalo?
  • Je hawa wanaopinga mdahalo hawana uelewa kuhusu umuhimu wa midahalo au wanaongozwa na hisia zaidi kuliko akili?
  • Je kuna mtu anaweza kuwa mtendaji bila kuwa mzungumzaji/ mjenga hoja?
  • Mheshimiwa Raisi ananafasi kubwa sana ya kuwin kwenye huu mdahalo kwasababu kuna mengi ameyafanya. Je hamuoni kama kuzuia mdahalo , mnamfanya asiyaeleze vema aliyoyafanya na wananchi wapate nafasi ya kuuliza maswali ili kujuzwa zaidi?
nawasilisha
 
Kwahiyo unataka kusema Lowassa ambaye nae hakutaka mdahalo ile 2015 ni kutokana na uwezo mdogo alionao? na vp wapiga waliyompigia kura hawakuliona hilo?
alifanyiwa interview na Zuhura Yunus wa BBC akaomba po! akasema unanioneaaa
 
Hii ni nzuri sana. Angalau sasa tuwe na issues ambazo tunaweza kupima/kulinganisha sera za vyama! Natamani sana media ingeweza kutusaidia wananchi kwa kutengeneza kitu kama matrix hivi......kwa mfano kwenye elimu (ccm wanasemaje, CDM, ACT?), kwenye mifuko ya jamii ? Kwenye afya? Etc.
 
Ila mdahalo hapana, watamtia aibu tu mgombea wetu......halafu msimu huu nimezimiss pushups ! Kulikoni?
 
Ukweli ni huu hapa...

Magufuli ni Rais JMT...ni raia namba moja wa Tanzania huwezi kumkalisha meza moja ya mdahalo na Wahuni.

Lisu kwanini asiombe mdahalo na wenzake wanaoitaka Ofisi kuu kwa mara ya kwanza? Aombe mdahalo na Membe, Sipunda na Lipumba!! Period
 
Wananchi wenyewe hawaoni umuhimu wa mdahalo,na ndio maana 2015 wagombea wa urais wa hivyo vyama(ccm na chadema) wote walikataa mdahalo na hakukuwa na tabu na wao ndio walishika nafasi ya kwanza na ya pili na kuwaacha mbali hata wale wagombea waliyoshiriki mdahalo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…