Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Upuuzi halafu mtoa mada unasoma?, Ridiculous. tulieni dawa iwaingie
Dawa gani? Angetoa ata hint basi anaufahamu wa maswala mbali mbali mara ohoo sijui diplomasia imeporomoka wakati hakuna ushahidi Tanzania kujitoa kwenye international treaty zozote, regional blocks na wala kuvunja bilateral agreements.

Mara sijui ataongeza abc bila ya kuelezea source of funds ni upuuzi mwisho, sasa aina maana kwa sababu kuna watu wanameza porojo zake; raisi nae aka entertain upuuzi wake.

Yeye anachotaka ni audience tu kufurahisha his ego yupo on per with Magu; mengine unajua atakayoongea sijui kufungia magazeti, kumuulizia Azoray Gwanda na Saanane, sijui kufungia mikutano ya upinzani. Maswala na matukio ambayo for the most part misingi yake ni decentralised decision ambazo Magufuli ahusiki nayo on daily basis.

Other than that we unadhani Tundu Lissu ana hoja gani za msingi kuhusu maswala ya uchumi, ulinzi na maendeleo ya nchi kiasi kwamba apewe audience na raisi? Si anataka tu akutane nae apige makelele yake ya ovyo tu.
 
Na sie wananchi pia wanafki au hatulipi uzito hili suala la mdahalo,yani tunaangalia kwanza mgombea tunayemshabikia kama anataka mdahalo ndio sie tunajifanya kutaka mdahalo ila mgombea akiwa hataki na sie tunasema hakuna umuhimu wa mdahalo.
 
Mdahalo ni kitu chengine kabisa,mi sidhani kama Lissu anauweza mdahalo na ndio maana anamg'ang'ania Magufuli.
 
Wacha kuropoka kama bata!! Nakutajia vitu viwili ambavyo Tanzania amejitoa. Moja ni Open Government Partnership, yaani uendeshaji Serikali kwa uwazi Tanzania ilijitoa mwaka 2016. Pili ni Mahakama ya Africa yenye makao yake Mkuu Arusha, Tanzania ilijitoa mwaka jana kwenye clause inayoruhusu mwananvmwananchi kuishtaki Serikali.
 
Tofautisha kati ya kuwa UN member ambapo nchi zinakubaliana treaties matokeo yake wanajikuta wanapokea international regulations na directives wanazopitisha kwenye mikutano yao na kutakiwa kutekeleza au kusimamia ivyo ndio unavyokuwa sehemu ya international community; similarly ndio inavyokuwa kwenye regional blocks inategemea treaties zipi mmekubaliana na hakuna sehemu kwenye makubaliano ya aina hiyo Tanzania imejitoa.

Hayo mambo unayoongelea ni voluntary international/community initiatives kujiunga au kujitoa ni swala la utashi tu.

Kuwa sehemu ya international community maana yake una share some sort of agenda na nchi nyingine mnakutana na ku discuss maendeleo yenu. Kuwa mwanachama wa taasisi ambazo ni voluntary kama ICC, open government, Mahakama ya Africa ni utashi.

Hiyo mahakama ya Africa ingekuwa sehemu ya AU block treaty na kuna regulations zake kama sehemu ya judicial system, serikali isingeweza jitoa. Mpaka kujitoa maana yake ni voluntary initiatives tu kama zinavuka mipaka hakuna shida kujitoa.

Mbona US, UK, Russia, China na wababe wengine wamejitoa uanachama ICC baada ya kuona kuna watu wao wanaweza itwa ni mambo ya kawaida hayo duniani kama hakuna international treaty inayolazimisha uwepo wa kila mtu.
 
Umeongea vizuri nami ndiyo ninavyoelewa. Sasa jiulize kwa nini amejiondoa kwenye hizo voluntary? Je watangulizi wake walikosea?

Na je unapata dalili gani kwa mtu anayejitoa kwenye mikataba mizuri kama ya uwazi?
Ina maana hata hiyo ambayo ni compulsory amejitoa tu!!
 
Sijui what was behind the scene mpaka kujitoa; nonetheless kwenye kujitoa huko hakuna madhara yoyote ya dipmolatic relation kama Lissu anavyolisha watu matango pori.

Mahusiano yetu kimataifa bado yapo vizuri sana, unataka Magu akabishane na mtu anae ongopa hatuko vizuri na zile story za Lissu za ubabaishaji huko sasa ndio kumuendekeza Lissu.
 
Mkuu kama na wee uko upande wa huyu kibaraka wa mabeberu nakupa pole,huyu hataboi,magufuli atamtwanga mapema sana,ajandae kusafiri kwenda kwa mabeberu wenzake
Thubutu; hatokubali kufanya mdahalo na lissu hata kwa lugha ya kisukuma ambayo hata lissu haijui-Lissu kiufupi ni alisoma na kuelimika kwelikweli tofauti na kina siye
 
Ccm sijui kwa nini wana wasiwasi na kukataa
ni vp jmn si mgombea wenu yuko vizuri jmn.?there's nothing to fear
Ni fursa
 
Lissu yuko smart than you think. Wewe endelea kutumika Serikali kwa kuwa ndiyo inakupa mkate wako na wanao. Lissu angekuwa mbabaishaji si mgetulia muache wananchi wawape kura ! Lissu yuko knowledgeable sana, refer speech yake ya ZANZIBAR na Muungano wa Tanzania. I can assure you huyu wa kwenu Magu anajuwa kukariri takwimu feki za kilometres na samaki wa baharini.
 
Thubutu; hatokubali kufanya mdahalo na lissu hata kwa lugha ya kisukuma ambayo hata lissu haijui-Lissu kiufupi ni alisoma na kuelimika kwelikweli tofauti na kina siye
Lisu alisoma na kuelimika kweli lakin hana AKILI
 
Mkuu kichuguu..

Unafahamu muundo serikali za mitaa pamoja na majukumu yake?

Kuna hivi vyeo vya DED, DCunavielewa kweli?
 
Sasa mtu anasomaje na kuelimika Alafu hana akili?
Kumbe ulikuwa hujui kwamba ivo ni vitu viwili tofauti......ikitokea vile vyoooooote ulivyofundishwa/karirishwa vikiondolewa kichwani, kitakachobaki ndio AKILI, aliyebuni mambo ya elimu yeye alikuwa ana AKILI sio ELIMU, sijui umenielewa mkuu John7371
 
Mkuu kichuguu..

Unafahamu muundo serikali za mitaa pamoja na majukumu yake?

Kuna hivi vyeo vya DED, DCunavielewa kweli?
Ninavielewa ndiyo; DC ni mwakilishi wa Rais Wilayani na DED ni mwakilishi wa Waziri Mkuu wilyani. Kama nimekosea makubali kusahihishwa
 
Atafukuzwa chamani kwa utovu wa nidhamu,
 
Really?!!

Hii si fake ID?!!!

Mmh....Hapana aisee wamemdukua....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…