Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)


..usiseme hujui waliomshambulia.

..hivi hujui chain of command ya aliyeondoa walinzi wa area D ili kuwapisha magaidi wakamshambulie Tundu Lissu?

..kweli hujui nani mwenye mamlaka ya kuondoa walinzi wale? Na mamlaka yake ni nidhamu huijui?
 
Ccm kumbukeni mwaka 2015 mliomba mdahalo baada ya kuona mgombea wa ukawa ni dhaifu,,Sasa mnaombwa mdahalo mnaanza kujinyata nyata inamaana Rais wetu anaogopa mdahalo wa kuelezea ilani na sera ya chama chake?mdahalo ni sehemu ya kufanya kampeni hofu ya nini?rais ni msomi tena degree tatu na amefanya presentation kibao ana uzoefu na pia kwa miaka 20 amekuwa waziri alikuwa anajibu maswali bungeni,akikataa mdahalo ataonesha ni dhaifu anastahili tumtumbue atakuwa na cheti feki,, haiwezekani PHD mzima uogope mdahalo.
 
Lissu anatafta kiki, ni kama anatafta umaarufu kupitia magufuli, na alivyo anaongea bila break au kutumia akili magufuli asiingie mtegon, maana kubishana na kichaa hua ni ngum sana
 
Siyo kweli kuwa ukichagua upinzani hupelekwei maendeleo kwenye jimbo lako, tatizo ni kuwa wabunge wa upinzani huwa hawapeleki mada zinazohusu majimbo yao bungeni bali wao huwa ni wanaharakati wa kupinga kila kitu cha serikali tu. Mpaka serikali ipitie mlango wa nyuma mikoani ndipo mambo ya majimbo husika yanapofika serikalini

Umewahi kumsikiliza Mbowe hapa?

 
Kwani kinachohofiwa kwenye mdahalo ni nini? Mbona mnahangaika hivi? Mnaelewa hapo kuwa mtu wenu hamuwezi Lissu kwa hoja, sasa mnajaribu kufunikafunika.

Usiseme mtu wenu, mtaje raisi alie madarakani ambae ni John Magufuli.

Na ndie mgombea wa sasa wa CCM.
 
..usiseme hujui waliomshambulia.

..hivi hujui chain of command ya aliyeondoa walinzi wa area D ili kuwapisha magaidi wakamshambulie Tundu Lissu?

..kweli hujui nani mwenye mamlaka ya kuondoa walinzi wale? Na mamlaka yake ni nidhamu hujui?

Usilazimishe mimi kuamini unachokiamini wewe.

Kila mtu ana haki na wajibu wa kutafakari shutuma za Tundu Lissu dhidi ya serikali.
 
Uraisi ni cheo cha heshima, mwenye cheo hicho hawezi kupoteza muda kufanya mdahalo na wapuuzi waropokaji
 
Inawezekana na wewe hujui kiingereza; unaweza kujua kuasiliana kwa kiingiereza bila kukijua vizuri kama Lissu na Magufuli walivyo.

Nimebahatika kusomea kwenye nchi inayoongea Kiingereza, naishi kwenye nchi inayoongea Kiingereza na mke na watoto wangu hawajui Kiswahili zaidi ya Kiingereza...
 
Magufuli hahitaji kuongea ongea, magufuli siyo debe shinda (amejaa)! Magufuli ni maneno machache saana na ni mwingi wa vitendo.
Sote tumeona au kusikia - Lissu bado ana siasa za viongozi wa zamani! Siasa za maneno jukwaani na mvinyo! Kazi za kuonyesha hana na watu wake wanakufa kwa umasikini.
 
Usilazimishe mimi kuamini unachokiamini wewe.

Kila mtu ana haki na wajibu wa kutafakari shutuma za Tundu Lissu dhidi ya serikali.

..sasa wewe shutuma za kuwa walinzi waliondolewa area D umezichukuliaje?

..umeridhika na majibu ya serikali kuhusu shutuma hizo?

..umeridhika na jinsi jeshi la Polisi lilivyoshughulikia uchunguzi wa shambulizi lile?
 
Lissu ameshakutana na viongozi wa dunia ya kwanza na kuhojiwa na vyombo vyao vya habari ije kuwa Magufuli.
mu ignore tuu kama Magu anacheza mapanga na wakina Chege kweri anamuita Lissu muhuni? hawa marobot ya Lumumba wahanga wakukosa akiri kweri
 
Mkuu huyo uliyemnukuu unadhan haielwei hayo uliyoandika? Ni basi tu anaongozwa na mahaba jumlisha na unafiki.
 
Kwani kinachohofiwa kwenye mdahalo ni nini? Mbona mnahangaika hivi? Mnaelewa hapo kuwa mtu wenu hamuwezi Lissu kwa hoja, sasa mnajaribu kufunikafunika.
Mnachong'ang'ania kwenye mdahalo ni kipi hasa? Mmeona watanzania hawaelewi sera zenu mnaforce mdahalo. Magufuli yupo busy na kuongoza nchi na kufanya kampeni kwa wakati mmoja
 
Nimebahatika kusomea kwenye nchi inayoongea Kiingereza, naishi kwenye nchi inayoongea Kiingereza na mke na watoto wangu hawajui Kiswahili zaidi ya Kiingereza...
Unaweza kuwa na familia inayoongea kiingereza wakati mwenyewe unababaisha ila mnaelewana kimawasiliano tu! Nimeshakutana na familia nyingi za aina ambayo mke anakuwa ni face ya familia kwa sababu mwanamme hajui lugha vizuri. Binafsi watoto wangu wote hawajui kiswahili sawaswa ingawa mke wangu ni mtanzania ambaye siyo kabila langu na wala sijui lugha yao lakini siwezi kutumia leverage ya watoto wangu au mke wangu kujua lugha zao. Mimi nazungumzia lugha ya kiingereza kwa sababu ya nature ya kazi yangu, siyo kwa sababu ya mazingira ya familia yangu.
 
..usiseme hujui waliomshambulia.

..hivi hujui chain of command ya aliyeondoa walinzi wa area D ili kuwapisha magaidi wakamshambulie Tundu Lissu?

..kweli hujui nani mwenye mamlaka ya kuondoa walinzi wale? Na mamlaka yake ni nidhamu hujui?
Ikifika angle hii hua wanajitoa ufahamu, kuna mmoja hapo juu anadai baada ya shutuma nyingi za kuituhumu serikali, eti serikali nayo ikaacha kufuatilia. Ni kama vile imesusa wakati ni wajibu wao kuchunguza na kutoa ripoti ya uchunguzi na wahusika wawajibishwe!!
 
Kama umeshindwa kujua lengo haswa la Magufuli kuinadi ilani makini ya ccm hata huo mdahalo hautakusaidia kitu comrade
 

..wanawajua waliotaka kumuua Tundu Lissu.

..wangekuwa hawawajui wangewatafuta, maana kuna uwezekano wakashambulia na mwingine.

..lakini kwasababu wanawajua, na wanajua walitumwa kumuua Tundu Lissu na siyo mtu mwingine, basi ndio maana unaona wametulia tu.
 
Lissu kama kweli anataka mdahalo asubiri mgombea wa 2020 apatikane ndipo ajiandae.

Magufuli ni mtekelezaji wa ilani tangu 2015 hayupo katika hadhi sawa na Lissu kwa sasa.

Mwenye jukumu la kutekeleza malengo ya chama kwa vitendo hawezi kuwekwa jukwaa moja na yule mwenye ndoto za urais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…