Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)



Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"

=====

LISSU IRINGA: MDAHALO NA MAGUFULI, MIKOPO ELIMU YA JUU NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Tundu Lissu ametoa wito kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. John Magufuli, kuwa tayari kushiriki mdahalo utakaowakutanisha wagombea hao wawili ili waeleze na kuhojiwa kuhusu maono na mipango yao ya namna ya kutekeleza agenda zinazohusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania, ikiwa ni sehemu ya wapiga kura kuwapima na kuwajua vyema washindani hao wakubwa katika nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.

Mhe. Lissu amesema kuwa ushiriki wa midahalo kwa wagombea urais ni mojawapo ya kipimo muhimu kinachotumika kimataifa kujua uwezo wa wagombea urais na kwa hapa nchini, takriban wiki mbili tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu, Agosti 26, mwaka huu, haina shaka yoyote kuwa ushindani katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uko kati ya Mgombea wa Chadema na Mgombea wa CCM, ambapo amesisitiza wito huo kwa kuviomba vyombo vya habari vikubwa hususan vituo vya luninga, kuandaa mdahalo huo.

“Natoa rai kwa mgombea mwenzangu wa CCM, tukutane kwenye mdahalo. Ufanyike kwa lugha yoyote ile na uendeshwe na wataalam tutakaokubaliana. Ili tuwaeleze na tuhojiwe hadharani na kujibu hadharani mipango na maono yetu. Naamini mwenzagu ambaye ameshakuwa Rais kwa miaka mitano hatakuwa na hofu ya kushindana na mimi ambaye sijawahi kuwa Rais. Tukutane pamoja. Tuache haya mambo ya kuogopana na kuchengana. Nina imani hatakimbia mdahalo. Akiogopa tutahoji majigambo ya usomi wake,” amesema Mhe. Lissu.

Aidha, Mhe. Lissu amesema Serikali atakayoiunda chini ya chama Chadema, itaondoa mara moja masharti ya kibaguzi na utaratibu mbovu wa kisheria unaotumika katika mfumo wa sasa wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambao umegeuka kuwa adha kubwa kwa wanafunzi na wazazi na badala yake, kanuni pekee itakayosimamia upatikanaji wa mikopo hiyo ni uhitaji wa mhusika.

Akisisitiza hoja hiyo, Mhe. Lissu amesema kuwa mfumo wa urejeshaji riba ya mikopo hiyo unaotumika sasa nao pia uko kinyume na utaratibu wa kisheria uliokuwa mwongozo kwa wanafunzi na wazazi kuingia makubaliano ya kukopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB), ambapo Serikali imeingiza utaratibu mwingine kuwataka wanufaika kulipa riba ya asilimia 15 badala ya asilimia 3 ya awali, akiahidi kuwa Serikali ya Chadema itaufutilia mbali kwa sababu unawafilisi kiuchumi wanufaikaji wa mikopo hiyo.

Akihutubia mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Mji wa Iringa na viunga vyake, uliofanyika leo katika Uwanja wa Mwembetogwa, Mhe. Lissu amesema mfumo unaotumika sasa umewekewa utaratibu ambao unawaumiza na kuwabagua wanafunzi na wazazzi hata wenye uhitaji wa mikopo hiyo ili waweze kujielimisha elimu ya juu kwa kadri ya uwezo wao.

Aidha, Mhe. Lissu akizungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote bila kubagua hali wala hadhi ya mtu, amesema kuwa kila mmoja katika wakati usiotarajiwa anaweza kuhitaji msaada wa kuhifadhiwa iwe kwa matibabu, ulemavu usiotarajiwa, umri wa uzeeni, kupoteza ajira au uhitaji wowote ule, hivyo Serikali atakayoiunda, akichaguliwa Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu utakaohakikisha kila Mtanzania anapata hifadhi kadri ya ya mahitaji, ikiwemo bima ya afya, badala ya sasa wanaohudumiwa walioko kwenye ajira rasmi pekee.

“Iringa ni mahali sahihi kabisa kuzungumzia agenda ya hali ya elimu yetu na hususan elimu ya juu. Kuna tatizo katika mfumo wetu wa utoaji elimu nchini. Mtakumbuka wakati ule nilipokuja wakati wa kutafuta udhamini nilizungumza hili. Tunapaswa kuubadili ili uweze kuwapatia watoto wetu maarifa na uwezo wa kufikiria kutatua matatizo yao na kuajiriwa mahali popote duniani. Kwa sababu hilo nililisema wakati ule na mlinielewa, leo nataka nizungumzie hili la elimu ya juu na hususan elimu ya juu, chuo kikuu. Wale wa makamo yangu wanajua kuwa wakati wetu elimu tuliyosoma ililipwa na umma wa Watanzania. Katika zama za CCM wanaita ya kisasa, ili motto wako asome Chuo Kikuu lazima umlipie au akopeshwe na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, mikopo hiyo na utaratibu wa utoaji wake na urejeshaji wake, imegeuka kuwa adha kubwa mno kwa wazazi na wanafunzi wenyewe.

“Kumekuwa na masharti ya kibaguzi katika utoaji wa mikopo ya hiyo. Wanafunzi waliosoma shule za binafsi wamekuwa wakiambiwa hawastahili kupata mikopo. Wanafunzi wengine wengi wameshindwa kuendelea na masomo yao. Serikali ya Chadema, nitakayoiunda mkinichagua Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu unaohakikisha kila mtoto anastahili kupata mkopo bila kujali alisoma wapi. Kanuni pekee itakayotuongoza ni, je anahitaji mkopo? Tutahakikisha pia wanufaikaji wote wanatendewa haki kwa kurejea kwenye sheria ya mwanzo iliyokuwa inaelekeza makato ya riba ya asilimia 3 badala ya sasa ambapo imefanywa kuwa asilimia 15 hali inayowafilisi kiuchumi,” amesema Mhe. Lissu.

Akitumia mkutano huo pia kuomba kura zake na kuwaombea kura wagombea ubunge na udiwani kwa tiketi ya Chadema katika Mkoa wa Iringa, Mhe. Lissu amezungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote, ambapo amesema kuwa mfumo uliopo sasa pamoja na kuwatenga watu wengine wasiokuwa kwenye ajira rasmi, pia umeshindwa kuwahudumia hata wahusika baada ya kutumiwa vibaya kwa matumizi yasiyokuwa na tija kwa wachangiaji, ambapo amesema fedha nyingi zimefujwa kiasi cha mifuko hiyo kushindwa kujiendesha na hatimae kufilisika.

Ameongeza kuwa tatizo la hifadhi ya jamii si uwingi au uchache wake, bali ni matumizi mabaya ya rasilimali zake, hivyo ameahidi kuwa Serikali atakayoiunda baada ya kuchaguliwa mwezi Oktoba, itahakikisha utaratibu mpya wa hifadhi ya jamii unawahusisha watu wote kwa ajili ya maendeleo yao na kuhakikisha inaendeshwa katika namna inayozingatia matumizi sahihi yenye tija kwa wahusika ambao watakuwa na uhuru wa kuamua.

“Tunazungumzia mfumo wa hifadhi ya jamii utakaoweza kuwahudumia watu wote, wastaafu wetu, wazee, wasiojiweza, bima ya afya. Tutahakikisha kila asiyejiweza anatunzwa na hifadhi ya jamii. Sisi wote hapa tutazeeka, tunaweza kuwa walemavu, tunaweza kupoteza ajira, tutaugua, tutahitaji kuhifadhiwa. Shida hapa kwetu si wingi wa mifuko, bali mifuko hiyo imefujwa. Walipoifilisi wakaleta masuala ya fao la kujitoa na ile kanuni mpya ya kikotoo, maana mifuko hiyo haina fedha tena,” amesema Mhe. Lissu.

Mhe. Lissu amesema kuwa utekelezaji wa mipango hiyo utahitaji vyanzo vya uhakika vya fedha, ambapo ametaja mapato yatakayotokana na uuzaji wa gesi asilia, ambayo uendelezaji wake ulianza wakati wa Serikali ya awamu ya nne, ulioibainisha Tanzania kuwa mojawapo ya nchi zenye utajiri mkubwa wa rasilimali hiyo, kabla haujatelekezwa katika awamu ya tano, itakuwa ni mojawapo ya vyanzo vya fedha ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu ya uhakika na Watanzania wote wanapewa haki ya hifadhi ya jamii.

Mhe. Lissu ametumia mikutano yake mitatu katika maeneo ya Migoli (Isimani), Ifunda (Kalenga) na Iringa mjini, kunadi agenda mbalimbali zilizomo katika Ilani ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, inayozungumzia masuala yote katika muktadha wa Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.

Imetolewa leo, Jumapili, Septemba 13, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Hatutaki mdahalo na mtu ambaye kila anapopata nafasi anatoa matusi kama hajalelewa vile...
 
Magufuli ni nyampara wa Barabara yeye anachoweza ni kukari makilometa na vijiji tu,mdahalo hawezi,

Alijichanganya Ndugai siku moja akakutana na Lissu ITV live,kilichomkuta hana hamu,akajichanganya tena balozi wetu huko Marekani bwana Masilingi alitaka kukimbia studio.

Jiwe hawezi kukubali labda adanganywe ni mkutano wa waandishi,halafu Lissu atokee ghafla.[emoji3]
 
Kamanda msaliti ameona maji yako shingoni sasa anatafuta kiki kupitia kwa JPM. Mtu mropokaji kama huyu hata mimi nisingefanya naye mdaharo: anaweza kuamua kukutukana hadharani, yeye hana chakupoteza, utakayeumia ni wewe!
 
Sisi tunataka kusikia sera na sio mashindano ya midahalo. Kwanza anatakiwa ajue Magufuli anafanya mambo mawili makubwa kwa wakati mmoja kuendesha nchi kama rais na kuendelea na kampeni na mambo yote kaweza kuyamudu vizuri sana. Chadema mwambieni mgombea wenu asimpotezee muda jemedari
 
Awe rais kwanza ili apate mdahalo na mwenzie wa level ya urais ila kwa sasa atembeze cv tu kwanza afanye midahalo hata na wakina Rungwe ndo wapo level sawa
 
Tmuulize Lissu kama anakubali tuwatumie madalali kwenye huo mdahalo. Kafulila anaweza wakilisha ccm.
 
Huo utakuwa mdahalo ama mipashoo ya waimba taraab kama hawa.



Mkuu, tafuta nyimbo moja ya kusuuza roho yaitwa "Nina Moyo Si Jiwe" imeimbwa na bibie Leyla Rashid.

Hutajuta.
 
Sisi tunataka kusikia sera na sio mashindano ya midahalo. Kwanza anatakiwa ajue Magufuli anafanya mambo mawili makubwa kwa wakati mmoja kuendesha nchi kama rais na kuendelea na kampeni na mambo yote kaweza kuyamudu vizuri sana. Chadema mwambieni mgombea wenu asimpotezee muda jemedari

Hii "statement" yako ndo bora kabisa kuliko zote hadi sasa.
 
Lissu lissu lissu nimekuita mara3 naomba umwache ndugu yetu asije anguka kesho anamkutano kijijini kwake naona na harmonize yupo kwa ajili ya burudani mpk nyumbn huna uhakika na umewafanyia maendeleo ya taa barabarani na uwanja wa ndege hahahaa
 
Huyo mjamaa amekulia porini afu anajiona lugha ya kingereza ni kijijini kwao

Kufanya mjadala na mropkaji wa matusi nani atakubali?
Aende ubeligiji akafanye mjadala na robert


Wewe ndiyo mjinga mwingine ambaye sikutegemea kama katika mtandao mkubwa kama huu tutakuona humu na kiswahili kama hiki uliondika hapa mjinga wewe😏😏
 
Lissu lissu lissu nimekuita mara3 naomba umwache ndugu yetu asije anguka kesho anamkutano kijijini kwake naona na harmonize yupo kwa ajili ya burudani mpk nyumbn huna uhakika na umewafanyia maendeleo ya taa barabarani na uwanja wa ndege hahahaa


Na aanguke kha ha haaa😆😆😆😆
 
Tundu Lissuuuuuuuuuu.. Mwenye nchi yake. Anatufurahisha sana huyu Mh. Mimi, familia yangu na ukoo wangu, kura zote ni kwa Tundu Lissu.
 
Huyo mjamaa amekulia porini afu anajiona lugha ya kingereza ni kijijini kwao

Kufanya mjadala na mropkaji wa matusi nani atakubali?
Aende ubeligiji akafanye mjadala na robert
Hivi ukiacha kuchangia utapungukiwa nini? Haujisikia vibaya ukiwa unasoma ulichokiandika. Mmekuja na ngojera mpya kuwa TAL anatumia lugha ya matusi. Ebu sema tusi nusu tu ambalo TAL katukana. Ebu kua hata kwa siku moja tu.
 
Rais Magufuli endelea kuchapa kazi na kuwaletea maendeleo watanzania. Kampeni unazofanya ni kama kutimiza matakwa ya katiba ya JMT, unazunguka kufanya presentation ya mazuri ambayo umewafanyia watanzania.

Itakuwa na mantiki gani kufanya mdahalo na mgombea ambae anasema eti hata wakoloni walijenga barabara! Hivi mwaka 1997 hivi majuzi tu kulikuwa na barabara ya lami hapo kwao Ikungi? Amesahau kuwa ulikuwa unatoka Dar asubuhi na kufika kwo Ikungi saa nne usiku?

Kwa nini Rais wetu kipenzi unayetufanyia makubwa uje ufanye mdahalo na mgombea ambae anadanganya watu eti Rufiji basin ipo eneo la Kitropiki na hivyo uhakika wa kuwa na maji ya kudhalisha umeme ni mdogo!

Hajui kuwa Rufiji river ina matawi ya mito mikubwa kama minne kama mto Kilombero,Ruaha mkuu na mingine mingi,hivyo muda wote wa mwaka una maji ya kutosha!

Rais wetu itakuwa ni kupoteza muda kufanya mdahalo na mgombea ambae anasema mradi kama JNHPP ni White E lephant hivyo hauna manufaa kwa wananchi. Maana ni mradi mkuubwa lakini hauta wanufaisha wananchi. Hivi hajui kuwa gharama za umeme zitashuka na wananchi wa kawaid na wenye viwanda watanufaika! Na hili litapunguza ukali wa maisha!

Itakuwa ni kupoteza muda kufanya mdahalo na mgombea ambae anakubali kweli umefanya makubwa ila anataka uweke wazi hizo pesa ulizitoa wapi. Yaani pamoja na kuwa mgombea wa urais hafahamu kuwa vyanzo vya mapato ni,mikopo,kodi,misaada na fine zinatozwa na serikali. Na haoni aibu kusema eti serikali ikikopa mikataba iwe inawekwa wazi hadi kwenye magazeti.

Itakuwa aibu kwa rais mchapa kazi kama wewe ambae anasema atafuta kodi na kuacha kutoza kodi. Huku akijua hakuna serikali duniani inajiendeha bila kodi. Na hii ni aibu kubwa sana kwa chama chake kuwa na mgombea kama huyu.

Leo ameshuhudia utiaji saini wa mradi wa bomba la mafuta la EACOP nafikiri roho imemuuma sana maana halitakii meme taifa hili.
Maana kama kununua ndege anasema hakuna faida sababu zipo grounded sasa hivi, huyu unafanya nae mdahalo wa nini! Ina maana hajui kuwa ugonjwa wa Covid-19 umesababisha ndege nyingi ziwe grounded. Kwa ujumla usipoteze muda kufanya mdahalo na mgombea ambae saizi yake ilikuwa ni kugombea ubunge.
 
Back
Top Bottom