Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu (CHADEMA), aomba mdahalo na Dkt. Pombe Magufuli (CCM)

Lisu anataka kutuletea mambo ya kisekondari sekondari. Eti Debate.

Nani anataka kudebate na mgombea wa chama kikuu cha wapangaji.

Wanapokea ruzuku wananywea konyagi badala ya kujenga ofisi.

Hivi kweli wanadhani watamdanganya nani kuwa wanaweza kuleta maendeleo wakati kujisimamia wao tu hawawezi.
 
Sisi tunataka kusikia sera na sio mashindano ya midahalo. Kwanza anatakiwa ajue Magufuli anafanya mambo mawili makubwa kwa wakati mmoja kuendesha nchi kama rais na kuendelea na kampeni na mambo yote kaweza kuyamudu vizuri sana. Chadema mwambieni mgombea wenu asimpotezee muda jemedari
Ndyomaana tunataka katiba mpya isiokuwa na upuuzi wa namna iyo.
 
Tuseme tu na ukweli, Magu hawezi risk hata siku mmoja kufanya mdahalo na lisu. Ni kamma anavyohofia kuhojiwa na BBC.
 
Tuseme tu na ukweli, Magu hawezi risk hata siku mmoja kufanya mdahalo na lisu. Ni kamma anavyohofia kuhojiwa na BBC.
Sio risk ni suala la kuamua unafanya nini kwa faida gani. Ccm hatuendeshwi na maono ya Lissu
 
Tuseme tu na ukweli, Magu hawezi risk hata siku mmoja kufanya mdahalo na lisu. Ni kamma anavyohofia kuhojiwa na BBC.
Kwa akili yako hata hao Bbc aogope kuhojiwa na kwa sababu ipi? Yule ni mtu wa vitendo, kazi anayoifanya inaonekana, unamhoji nini? Miaka mingine mitano anapewa ili akamikishe makubwa akiyoyafanya.
 
Mr. Pushups hawezi midahalo. Yeye hasira kaweka mbele. Kuna mambo ya kujisifia na sio miundo mbinu. Huwezi kujisifia barabara, au flover ukataka wananchi wakuchagua. Huwezi kujieleza mbele ya hadhara ya watu wanaoweza kukuhoji. Mtihani sana kutawaliwa na CCM.
 
Hilo jibu nililokwoti ni la kijinga sana na wala halikuwa na uhusiano na post yangu kiasi kuwa linaonyesha mapungufu makubwa sana ya uelewa wako wa mambo unayosoma. Post yangu ni kuwa kujua Kiiengereza siyo kigezo cha urais kwani hata mimi najua kiingereza kuliko wote waiwili lakini sijidai kuwa mimi ni bora kuwa raisi kuliko wao. lakini wewe kwa akili fupi ukakurupukia mambo ya ajabu yasiyohusika

Mimi sikusema kama ukijua Kiingereza ndiyo una uwezo mkubwa wa kuwa rais. Tatizo langu ni wewe kumuweka Lissu na Magufuli kwenye level moja ya kujua Kiingereza. Juha ni wewe ambaye hukujua ni kitu gani nilikuwa nabishania. Nina mashaka kama kweli kazi yako ni ya kufundisha huko Marekani kwasababu ujinga wako unaonekana dhahiri hapa Jamiiforums.
 
Magufuli atakubali mdahalo iwapo IGP, CDF. Kabudi na Polepole watakuwepo.
Afanye mdahalo wa nini na mgombea ambae anasema mto Rufiji hauna maji ya uhakika? Ndio asumbuke kuandaa mdahalo na mtu kama huyu! Igp na Cdf wa nini kwenye mdahalo wa mtu kama huyu!
 
Mimi sikusema kama ukijua Kiingereza ndiyo una uwezo mkubwa wa kuwa rais. Tatizo langu ni wewe kumuweka Lissu na Magufuli kwenye level moja ya kujua Kiingereza. Juha ni wewe ambaye hukujua ni kitu gani nilikuwa nabishania. Nina mashaka kama kweli kazi yako ni ya kufundisha huko Marekani kwasababu ujinga wako unaonekana dhahiri hapa Jamiiforums.
1600047063742.png


Kuna thread hii

Wapenzi wa CHADEMA ndio kundi la watu wenye hasira sana kwa sasa
 
Sijakuelewa comrade, unasema upuuzi unazungumzia mdahalo wa Lissu?
Mdahalo, Sera hatuna haja nazo sisi
Wengine mauno, misambwanda ya wasanii wacheza show yao inatosha mzee

Ova
 
Sawa basi acha tuendele kuangalia mauno ya wsanii
Sera hatuna mpango nazooo kwa Sasa

Ova
Labda huwa husikilizi nini JPM huwa ananadi ilani ya Ccm ilivyotekelezwa,itavyotekelezwa kwa kila mkoa. Kazi yako ni kusikiliza wasanii.
 


Akiwa mkoani Iringa leo tarehe 13 Septemba, Lissu amesema "Natoa rai kwa Mgombea Urais wa CCM na vyombo vyetu vya habari, kufanikisha mdahalo kuhusu mustakabali wa Taifa letu la Tanzania"

=====

LISSU IRINGA: MDAHALO NA MAGUFULI, MIKOPO ELIMU YA JUU NA HIFADHI YA JAMII KWA WOTE

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mhe. Tundu Lissu ametoa wito kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. John Magufuli, kuwa tayari kushiriki mdahalo utakaowakutanisha wagombea hao wawili ili waeleze na kuhojiwa kuhusu maono na mipango yao ya namna ya kutekeleza agenda zinazohusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania, ikiwa ni sehemu ya wapiga kura kuwapima na kuwajua vyema washindani hao wakubwa katika nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.

Mhe. Lissu amesema kuwa ushiriki wa midahalo kwa wagombea urais ni mojawapo ya kipimo muhimu kinachotumika kimataifa kujua uwezo wa wagombea urais na kwa hapa nchini, takriban wiki mbili tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu, Agosti 26, mwaka huu, haina shaka yoyote kuwa ushindani katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uko kati ya Mgombea wa Chadema na Mgombea wa CCM, ambapo amesisitiza wito huo kwa kuviomba vyombo vya habari vikubwa hususan vituo vya luninga, kuandaa mdahalo huo.

“Natoa rai kwa mgombea mwenzangu wa CCM, tukutane kwenye mdahalo. Ufanyike kwa lugha yoyote ile na uendeshwe na wataalam tutakaokubaliana. Ili tuwaeleze na tuhojiwe hadharani na kujibu hadharani mipango na maono yetu. Naamini mwenzagu ambaye ameshakuwa Rais kwa miaka mitano hatakuwa na hofu ya kushindana na mimi ambaye sijawahi kuwa Rais. Tukutane pamoja. Tuache haya mambo ya kuogopana na kuchengana. Nina imani hatakimbia mdahalo. Akiogopa tutahoji majigambo ya usomi wake,” amesema Mhe. Lissu.

Aidha, Mhe. Lissu amesema Serikali atakayoiunda chini ya chama Chadema, itaondoa mara moja masharti ya kibaguzi na utaratibu mbovu wa kisheria unaotumika katika mfumo wa sasa wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambao umegeuka kuwa adha kubwa kwa wanafunzi na wazazi na badala yake, kanuni pekee itakayosimamia upatikanaji wa mikopo hiyo ni uhitaji wa mhusika.

Akisisitiza hoja hiyo, Mhe. Lissu amesema kuwa mfumo wa urejeshaji riba ya mikopo hiyo unaotumika sasa nao pia uko kinyume na utaratibu wa kisheria uliokuwa mwongozo kwa wanafunzi na wazazi kuingia makubaliano ya kukopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB), ambapo Serikali imeingiza utaratibu mwingine kuwataka wanufaika kulipa riba ya asilimia 15 badala ya asilimia 3 ya awali, akiahidi kuwa Serikali ya Chadema itaufutilia mbali kwa sababu unawafilisi kiuchumi wanufaikaji wa mikopo hiyo.

Akihutubia mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Mji wa Iringa na viunga vyake, uliofanyika leo katika Uwanja wa Mwembetogwa, Mhe. Lissu amesema mfumo unaotumika sasa umewekewa utaratibu ambao unawaumiza na kuwabagua wanafunzi na wazazzi hata wenye uhitaji wa mikopo hiyo ili waweze kujielimisha elimu ya juu kwa kadri ya uwezo wao.

Aidha, Mhe. Lissu akizungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote bila kubagua hali wala hadhi ya mtu, amesema kuwa kila mmoja katika wakati usiotarajiwa anaweza kuhitaji msaada wa kuhifadhiwa iwe kwa matibabu, ulemavu usiotarajiwa, umri wa uzeeni, kupoteza ajira au uhitaji wowote ule, hivyo Serikali atakayoiunda, akichaguliwa Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu utakaohakikisha kila Mtanzania anapata hifadhi kadri ya ya mahitaji, ikiwemo bima ya afya, badala ya sasa wanaohudumiwa walioko kwenye ajira rasmi pekee.

“Iringa ni mahali sahihi kabisa kuzungumzia agenda ya hali ya elimu yetu na hususan elimu ya juu. Kuna tatizo katika mfumo wetu wa utoaji elimu nchini. Mtakumbuka wakati ule nilipokuja wakati wa kutafuta udhamini nilizungumza hili. Tunapaswa kuubadili ili uweze kuwapatia watoto wetu maarifa na uwezo wa kufikiria kutatua matatizo yao na kuajiriwa mahali popote duniani. Kwa sababu hilo nililisema wakati ule na mlinielewa, leo nataka nizungumzie hili la elimu ya juu na hususan elimu ya juu, chuo kikuu. Wale wa makamo yangu wanajua kuwa wakati wetu elimu tuliyosoma ililipwa na umma wa Watanzania. Katika zama za CCM wanaita ya kisasa, ili motto wako asome Chuo Kikuu lazima umlipie au akopeshwe na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, mikopo hiyo na utaratibu wa utoaji wake na urejeshaji wake, imegeuka kuwa adha kubwa mno kwa wazazi na wanafunzi wenyewe.

“Kumekuwa na masharti ya kibaguzi katika utoaji wa mikopo ya hiyo. Wanafunzi waliosoma shule za binafsi wamekuwa wakiambiwa hawastahili kupata mikopo. Wanafunzi wengine wengi wameshindwa kuendelea na masomo yao. Serikali ya Chadema, nitakayoiunda mkinichagua Oktoba 28, mwaka huu, itaweka utaratibu unaohakikisha kila mtoto anastahili kupata mkopo bila kujali alisoma wapi. Kanuni pekee itakayotuongoza ni, je anahitaji mkopo? Tutahakikisha pia wanufaikaji wote wanatendewa haki kwa kurejea kwenye sheria ya mwanzo iliyokuwa inaelekeza makato ya riba ya asilimia 3 badala ya sasa ambapo imefanywa kuwa asilimia 15 hali inayowafilisi kiuchumi,” amesema Mhe. Lissu.

Akitumia mkutano huo pia kuomba kura zake na kuwaombea kura wagombea ubunge na udiwani kwa tiketi ya Chadema katika Mkoa wa Iringa, Mhe. Lissu amezungumzia umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa watu wote, ambapo amesema kuwa mfumo uliopo sasa pamoja na kuwatenga watu wengine wasiokuwa kwenye ajira rasmi, pia umeshindwa kuwahudumia hata wahusika baada ya kutumiwa vibaya kwa matumizi yasiyokuwa na tija kwa wachangiaji, ambapo amesema fedha nyingi zimefujwa kiasi cha mifuko hiyo kushindwa kujiendesha na hatimae kufilisika.

Ameongeza kuwa tatizo la hifadhi ya jamii si uwingi au uchache wake, bali ni matumizi mabaya ya rasilimali zake, hivyo ameahidi kuwa Serikali atakayoiunda baada ya kuchaguliwa mwezi Oktoba, itahakikisha utaratibu mpya wa hifadhi ya jamii unawahusisha watu wote kwa ajili ya maendeleo yao na kuhakikisha inaendeshwa katika namna inayozingatia matumizi sahihi yenye tija kwa wahusika ambao watakuwa na uhuru wa kuamua.

“Tunazungumzia mfumo wa hifadhi ya jamii utakaoweza kuwahudumia watu wote, wastaafu wetu, wazee, wasiojiweza, bima ya afya. Tutahakikisha kila asiyejiweza anatunzwa na hifadhi ya jamii. Sisi wote hapa tutazeeka, tunaweza kuwa walemavu, tunaweza kupoteza ajira, tutaugua, tutahitaji kuhifadhiwa. Shida hapa kwetu si wingi wa mifuko, bali mifuko hiyo imefujwa. Walipoifilisi wakaleta masuala ya fao la kujitoa na ile kanuni mpya ya kikotoo, maana mifuko hiyo haina fedha tena,” amesema Mhe. Lissu.

Mhe. Lissu amesema kuwa utekelezaji wa mipango hiyo utahitaji vyanzo vya uhakika vya fedha, ambapo ametaja mapato yatakayotokana na uuzaji wa gesi asilia, ambayo uendelezaji wake ulianza wakati wa Serikali ya awamu ya nne, ulioibainisha Tanzania kuwa mojawapo ya nchi zenye utajiri mkubwa wa rasilimali hiyo, kabla haujatelekezwa katika awamu ya tano, itakuwa ni mojawapo ya vyanzo vya fedha ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu ya uhakika na Watanzania wote wanapewa haki ya hifadhi ya jamii.

Mhe. Lissu ametumia mikutano yake mitatu katika maeneo ya Migoli (Isimani), Ifunda (Kalenga) na Iringa mjini, kunadi agenda mbalimbali zilizomo katika Ilani ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, inayozungumzia masuala yote katika muktadha wa Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.

Imetolewa leo, Jumapili, Septemba 13, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Mdahalo wa kazi gani? Mwezi ujao hatuendi kuchagua mtu anayeongea vizuri. Hayo tulikuwa tukiyafanya shuleni kwenye 'debating clubs'. Kukiwa na mashindano kati ya shule na shule, kila shule inachagua wale wanaokimwaga Kimombo vizuri kwenda kuiwakilisha shule. Mwezi ujao tunaenda kuchagua mtu wa kutuongoza na kutuletea maendeleo. Tunahitaji mtendaji, Siyo mzungumzaji. Magufuli ameisha dhihirisha utendaji wake. Huenda hana kipaji cha uongeaji. Hata Kimombo chake si kizuri sana kama wapinzani wanavyokazia. Lakini hata kipofu ameona utendaji wake. Anafuatilia mambo yeye mwenyewe. Siku ya kwanza baada ya kushika madaraka aliibukia Hazina kwa kutembea kwa mguu. Siku chache baadaye akaenda Muhimbili ambako kulikuwa na uwozo mkubwa. Mambo yakaboreshwa. Miezi michache iliyopita tulishuhudia akimpagasha Mkuu wa Mkoa wa wakati huo kuhusu kiwanda cha machinjio hapo Dar. Kwa hiyo ameendelea na ufuatiliaji hivyo hivyo tangu siku ya kwanza mpaka juzi aliposikika akimuagiza Mfugale kuhusu barabara ya Kilomita 46 huko Ukerewe. Wengine wakahusisha hilo na uchaguzi ujao ambapo ukweli ni kwamba amekuwa mfuatiliaji tangu siku ya kwanza kuingia madarakani. Lissu ni mzungumzaji tu. Kila kuhutubia kwake amekuwa akijikita katika madhaifu ya Magufuli kuliko kusema atatutendea nini. Hakuna maana kuwadanganya watu kwa maneno mazuri. Hakuna haja kabisa ya mdahalo.
 
Back
Top Bottom