Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili

Ofisi ya Upelelezi wa makosa ya jinai imemtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Antiphas Mughwai Lissu kufika kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai makao makuu Dar es Salaam kwa kosa la kutoa maneno yasiyo na staha kumjibu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamesemwa kupitia barua ya Ofisi hiyo kwa Lissu ikibainisha kuwa Ofisi inafanya uchunguzi kuhusiana na maneno ambayo Lissu aliyatumia ambayo hayana staha kumjibu Mh. Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia tarehe 15/07/2023.

“Ili tuweze kukamilisha uchunguzi wetu, ofisi hii inakutaka ufike ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Makao Makuu Ndogo Dar es Salaam siku ya alhamisi tarehe 20 Julai, 2023 saa 3:00 kamili asubuhi bila kukosa kwa ajili ya mahojiano.” imesema barua hiyo.
 
Huu mwenge unatakiwa itupwe mbali ndio inafanya Watanzania watawaliwe na mazuzu..usikute ndio kimbola tunapigwa watanzani tunakosa umoja wa kusimamia mambo yetu.
Usikute? We hujui ili tutawalike lazima moto upitishwe kila wilaya? Na kafara kama zote🤔🤔
 

Kwani hao hawawezi kufanya maamuzi kwa makosa? Au wakishaamua chochote kwako ww ni sawa? Huyo Lowassa leo bado yuko cdm?
 
Shame on it, yaani mkataba wa bandari ndio iwe kero wananchi kuanza kukamatwa kamatwa hovyo kwa kutoa maoni ya kupinga hicho kitu! Kama wananchi wenyewe hawautaki huo mkataba ya nini kuwanyamazisha kwa kitisho? Hao ni akina lissu wanaojulikana, wapo wasiojulikana ambao nao hawautaki huo mkataba wakikamatwa wote mahabusu zote nchini hazitatosha
 
Safi sana akamkabili, namshauri Kingai kitu cha kwanza ili kuisaidia mahakama ampeleke Lussu akapimwe wazimu.
 
Hoja gani Mzee? Matusi na kudhalilisha sio Demokrasia vinginevyo hata Shetani wenu atawashangaa View attachment 2692265
"Utu na heshima ya Rais Samia" itatokana na matendo ya uongozi wake. Kama matendo yake hayaendani na matakwa ya wananchi anaowaongoza, asitegemee kupewa hiyo heshima inayohimizwa..

Maajabu ya nchi yetu ndiyo haya. Mtu anatumia cheo chake kufanya ujambazi kwa watu wake, badala ya kumshutumu na kumtaka aachie ngazi, kuna watu bado wanataka jambazi huyo apewe heshima?

Samia wakati huu angetakiwa kuwa jela badala ya kudai apewe heshima.

Heshima haidaiwi, inatolewa tu kwa mtu yeyote kutokana na matendo yake katika jamii anayoishi
 
Huyo kingai ameshatibiwa ile fistula yake aliyopata wakati anawekwa mtukati na Kibatala?
 
Naona wahafidhina wa CCM wameamua kuitumia polisiccm kumharibia Samia
 
...kila laheri
Hii "kila la heri" inamhusu nani, mkuu 'Proved'?

Maajabu ninayoyaona hapa ni kuwa mtu anayepanga mbinu za ujambazi kwa taifa lake, ndiye huyo huyo anayepambana kuwabana wanaotafuta njia za kumzuia jambazi huyo, hadi kutumia vifaa vinavyotakiwa kuzuia ujambazi huo, kama polisi.

Haya uliwahi kuyaona wapi?
 
ala, komandoo Kingai mzee wa Rau madukani bado upo baba !! umeshasahau lile kalinyekalinye la PGO 😀
 
Samahani bwana Red blood cells hivi akitumia lugha ya ustaha ni kwamba hatoeleweka ama naye ni wale wanaotafuta sifa mitandaoni?
Kama kiongozi ukiongea vitu vya kijinga na watu wakakuambia huo ulioongea ni upuuzi. Kuna shida gani? Kiongozi anapokusea na anakaza shingo, unataka wanaoongozwa wafanyaje?
 
Sa100 bhn badala ya kurekebisha makosa anaanza kuweka watu ndani.Kwamba mkimuweka TL ndani ndio itabadilisha mawazo ya watu?Juzi hapo mtoto wa Karume kawapa makavu live mkaishia kumtoa kwenye chama
 
Utazikunya hizo hela ulizoongwa na Dp World🤣🤣
 
Upuuzi mtupu. Hizo kesi zote za kubambikia watu walisema wanazifuta. Sahizi kwa sababu mtu amewakosoa, wanazirudisha! Ni uwendawazimu wa madaraka kwa nia ya kukomoa watu.

Kama zingekuwa ni kesi halisia, ilishindikana vipi kwa zaidi ya mwaka mzima, serikali ishindwe kupata ushahidi?

Watu wajinga wanajifanya wana akili kuliko watu wenye akili. Wacha wenye mamlaka wajifariji kwa mbinu zao za kishetani kuwakomoa watu, lakini hawatashinda.

Wala hatutashangaa kuona watu wote walio mstari wa mbele katika kupinga wizi wa rasilimali za nchi unaofanywa na watawala kupitia uwekezaji magumashi, wakiwekwa mahabusu na wakibambikiwa kesi. Wamekwishaanza na Dr. Rugemeleza, Mwambukusi, Madeleka, Lisu, na bila shaka watafuata wengine. Lakini hawatafanikiwa. Shetani humpa mwanadamu ushindi wa muda ili kumpumbaza, lakini hawezi kumpa ushindi wa kudumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…