Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 4,107
- 9,671
Shangaa na wewe. Rais wa Tanzania ni mungu mtu.Hivi Rais ni ni nani yeye ?Rais anakwenda chooni anakata gogo kama sisi tu.Yeye asisemwe ni nani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shangaa na wewe. Rais wa Tanzania ni mungu mtu.Hivi Rais ni ni nani yeye ?Rais anakwenda chooni anakata gogo kama sisi tu.Yeye asisemwe ni nani?
Usikute? We hujui ili tutawalike lazima moto upitishwe kila wilaya? Na kafara kama zote🤔🤔Huu mwenge unatakiwa itupwe mbali ndio inafanya Watanzania watawaliwe na mazuzu..usikute ndio kimbola tunapigwa watanzani tunakosa umoja wa kusimamia mambo yetu.
Kama Akina Lissu na Mbowe walikubali mimi na wewe ni nani tupinge?
Kama kwa maumivu na shida walizopata kujenga chama hadi mimi na wewe tukakipenda na ikafika mahali wakatafakari wakaona Lowasa anaweza kugombea sidhani kama kuna Mtu mwingine ana uhalali wa kupinga.
I stand to be corrected
"Utu na heshima ya Rais Samia" itatokana na matendo ya uongozi wake. Kama matendo yake hayaendani na matakwa ya wananchi anaowaongoza, asitegemee kupewa hiyo heshima inayohimizwa..Hoja gani Mzee? Matusi na kudhalilisha sio Demokrasia vinginevyo hata Shetani wenu atawashangaa View attachment 2692265
Huyo kingai ameshatibiwa ile fistula yake aliyopata wakati anawekwa mtukati na Kibatala?Baada ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu. Leo DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo kuwakabili. Madalali wa bandari zetu wasitutishe!
Rais anayesaini mikataba ya hovyo kuliko hata wa Chifu Mangungo; anayegawa bandari zetu zote na nia za usafirishaji kisirisiri kwa wageni; anayelazimisha Bunge kubariki uharamia huo, na anayenyang'anya watu wetu ardhi zao na kuwapa wageni, anastahili kukosolewa kwa staha gani?
Tundu Lissu
Julai 18, 2023
View attachment 2692285
Barua ya wito wa Polisi
====
Mnamo jana, Julai 17 Mdau wa JF alidokeza kuwa Lissu na Mbowe walikuwa wanasakwa DOKEZO - Lissu na Mbowe wanatafutwa kukamatwa lakini Lissu aliifahamisha JF "Sijazisikia tetesi hizo. Kama ni za kweli, itakuwa ni mara ya kwanza kwa mimi au Mwenyekiti kukamatwa?"
Hii "kila la heri" inamhusu nani, mkuu 'Proved'?...kila laheri
Abautani ?? 😂😂Mtanikumbuka kwa mazuri 😀😀😀
Mropokaji tuLissu is one the people who were born so the rest we can live/survive on this planet.
Kwa maneno mengine, watu aina ya Lissu, waliletwa duniani kwa malengo maalumu; wengine tulizaliwa kujaza ulimwengu(kuishi).
Kama kiongozi ukiongea vitu vya kijinga na watu wakakuambia huo ulioongea ni upuuzi. Kuna shida gani? Kiongozi anapokusea na anakaza shingo, unataka wanaoongozwa wafanyaje?Samahani bwana Red blood cells hivi akitumia lugha ya ustaha ni kwamba hatoeleweka ama naye ni wale wanaotafuta sifa mitandaoni?
At Court is where CDM feels at home,Kingai mwenyewe analijua vizuri hilo,hata yeye anaomba sana asikutane nao hukoBad move.
Court is where CDM loves to battle.
Utazikunya hizo hela ulizoongwa na Dp World🤣🤣Kamata hao weka kolokoloni wasote kabisa mpaka 2026. Mbowe na Lisu ni wahuni wahuni, walitutukania Dkt Magufuli mpaka wakafanya sherehe ya kifo chake na wameyakoroga tena kwa Mama, acha wakomeshwe!
Ningekuwa polisi ningehakikisha namrusha kichura chura lisu na mbowe halafu namtandika mbowe kirungu utosini huku analia anaruka kichura chura na lisu namchapa kirungu cha kwenye magoti namrusha kichura chura akome.
Upuuzi mtupu. Hizo kesi zote za kubambikia watu walisema wanazifuta. Sahizi kwa sababu mtu amewakosoa, wanazirudisha! Ni uwendawazimu wa madaraka kwa nia ya kukomoa watu.TUACHE KUCHANGANYA KWA MIHEMKO YA KISIASA NA PROPAGANDA ZA KIJINGA KWENYE TAALUMA YA SHERIA. MFANO HALISI NI HUU HAPA
SABABU ZA KUKAMATWA WAKILI PETER MADELEKA
Mnamo mwaka 2020 Wakili Peter Madeleka alikamatwa na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi no. 40 (Economic case no 40/2020) katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha. Katika kesi hiyo alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi (forgery) kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Adhabu (Penal Code) kifungu cha 337 cha sheria hiyo. Pia alishtakiwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumu ( Anti Money laundering Act).
Wakati shauri lake linaendelea aliomba kufanya makubaliano na serikali ( Plea Bargaining) na taratibu zote za kufanya makubaliano zilifuatwa na ndipo aliachiwa huru.
Mara baada ya kuachiwa huru kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii Wakili Madeleka aliendelea kuchapisha habari kuwa alilazimishwa kukiri kosa na aliekuwa mkurugenzi wa mashtaka.
Baadae alifungua kesi katika mahakama kuu akipinga taratibu hizo lakini maombi hayo madogo yalitupwa nje kwa kuwa mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri Hilo.
Ndipo alifungua shauri hilo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kupinga maamuzi hayo lakini mahakama ilitoa maamuzi kuwa taratibu zote za makubaliano ( plea bargaining )zilifanyika sawa.
Baada ya maamuzi hayo alikata rufaa tena na kuja na sababu tofauti ambapo mahakama ilisikiliza Hoja zake na kutoa amri kuwa taratibu za makubaliano hazikuzingatiwa hivyo kuamuru status ya kesi yake kurudi kama ilivyokuwa awali.
Baada ya maamuzi hayo Wakili Madeleka alikamatwa tena ili kuweza kuendelea na kesi yake ya msingi na kwa kuwa makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.
UPOTOSHAJI:
Jamii inapotoshwa na kuaminishwa kuwa mshtakiwa ameshikwa kutokana na kutoa maoni yake juu ya Mkataba wa DP world na Serikali ya JMT jambo ambalo si sahihi.
Ikumbukwe watu mbalimbali wametoa mawazo yao na hakuna yoyote alieshikwa.
Hata katika kesi iliyofunguliwa na mawakili yeye si miongoni Mwao.
Hivyo ifahamike na itambulike mshtakiwa ameshikwa kwa makosa yake aliyoyafanya huko nyuma ambapo yeye mwenyewe alikiri na sasa ameomba mahakama ifute maamuzi hayo hivyo kesi yake ya msingi inaendelea.