Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili

Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili

View attachment 2692232
Baada ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu. Leo DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo kuwakabili. Madalali wa bandari zetu wasitutishe!

Tundu Lissu
Julai 18, 2023

View attachment 2692285
Barua ya wito wa Polisi

====

Mnamo jana, Julai 17 Mdau wa JF alidokeza kuwa Lissu na Mbowe walikuwa wanasakwa DOKEZO - Lissu na Mbowe wanatafutwa kukamatwa lakini Lissu aliifahamisha JF "Sijazisikia tetesi hizo. Kama ni za kweli, itakuwa ni mara ya kwanza kwa mimi au Mwenyekiti kukamatwa?"
Kama hiyo barua wamerudi nayo, hii picha ya barua hiyo imepatikanaje?
 
View attachment 2692232
Baada ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu. Leo DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo kuwakabili. Madalali wa bandari zetu wasitutishe!

Tundu Lissu
Julai 18, 2023

View attachment 2692285
Barua ya wito wa Polisi

====

Mnamo jana, Julai 17 Mdau wa JF alidokeza kuwa Lissu na Mbowe walikuwa wanasakwa DOKEZO - Lissu na Mbowe wanatafutwa kukamatwa lakini Lissu aliifahamisha JF "Sijazisikia tetesi hizo. Kama ni za kweli, itakuwa ni mara ya kwanza kwa mimi au Mwenyekiti kukamatwa?"
Hivi Rais ni ni nani yeye ?Rais anakwenda chooni anakata gogo kama sisi tu.Yeye asisemwe ni nani?
 
Vibaraka wa mabeberu nyie inje za inje mnatafuta nini mmeacha jengo lenu la mchongo kutwa inje za inie hopeless kabisa nyie.
Mnapinga uwekezaji ili tuendelee kuwa tegemezi kwa hao mabeberu wenu🚮
Ccm ni majizi ya rasilimali za Taifa
 
Tumeshasema hapa kwamba! Kilikuwa ni kipere tu, kadiri siku zinavyozidi, kipere kinazidi kukunwa na kinatengeneza kidonda kiduchu kiduchu

Hili la DP world na hatima ya kinachoendelea, litakuwa donda ndugu na wa kulitibu hatapatikana!

Wao waendelee tu kutumia akili ndogo, jibu litapatikana tu

Iko hivi!

Huwa haiwezekani jambo jema likalindwa kwa uovu! Bali ni uovu pekee ambao kwa sababu ya kuogopa fedheha na kushindwa kuukubali ukweli ndiyo hulindwa kwa uovu

Binadamu waovu huamua kuulinda uovu wao kwa uovu!

Mungu hawi nyuma ya uongozi wa kidhalimu kamwe, na udhalimu kwake ni pamoja na ufisadi, rushwa, mauwaji, utesaji, utekaji, kuamru kupiga watu kwa hila,,, na mambo yote yanayofanana na hayo!

Utawala wa aina hiyo huwa hauwezi kudumu abadani!

Ni watu saba tu tena ni wakoma ambao Mungu alikaa ndani yao! walilifukuza jeshi la maelfu ya kishami,
 
Vibaraka wa mabeberu nyie inje za inje mnatafuta nini mmeacha jengo lenu la mchongo kutwa inje za inie hopeless kabisa nyie.
Mnapinga uwekezaji ili tuendelee kuwa tegemezi kwa hao mabeberu wenu🚮
Wewe sio mtanzania, hata kuandika kiswahili hujui, jinga wewe rudi kwa nchi yako!
 
Huu mwenge unatakiwa itupwe mbali ndio inafanya Watanzania watawaliwe na mazuzu..usikute ndio kimbola tunapigwa watanzani tunakosa umoja wa kusimamia mambo yetu.
Lazima iwe shida Maana tumeliwa vuguvugu na Mungu alisema mtu achague kuwa baridi au moto kama ni vuguvugu atatutapika. Sasa sie tunamuomba Mungu na watumishi wa Mungu akina Mwakasege na wengineo wengi huku wengine wakiabudi mwenge na mizimu. Ndio maana mambo hayaendi.
 
Tundu Lissu should vie for his party nomination for President and Party Leadership.
 
Sawa endeleeni basi mtavuna mnachopanda Kila mtu Kwa size yake.
Vilio vimeanza kusikika huku 👇
 
Huyu kingai ninavyomjua alivyotolewa jasho na akina kibatala na mtobesya huyu huyu akumbane na moto wa Tundu Antipas Mughwai Lissu? Nawahakikishia Kingai siyo amri yake hii huyu kaamrishwa na ninachojua hapa kuna Dokta wa mhimbili anatengeneza ugonjwa feki ili kumuokoa Kingai kuanzia siku atakayotakiwa kuonana na lissu uso kwa uso.
 
Vibaraka wa mabeberu nyie inje za inje mnatafuta nini mmeacha jengo lenu la mchongo kutwa inje za inie hopeless kabisa nyie.
Mnapinga uwekezaji ili tuendelee kuwa tegemezi kwa hao mabeberu wenu🚮
wewe bwege bonge la tahira yani,
kinachopingwa sio uwekezaji ila mkataba mbovu wa kuuza bandari za Tanganyika

hujiulizi kwanini mkataba huo upigiwe kelele na kuna mikataba mingi haikua na shida imepitishwa bila kelele?

think twice Chawaz!
 
Back
Top Bottom