Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili

Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili

Nilisema kuhusu hili wakati na-comment kwenye uzi mmoja hivi karibuni. Hii ni mbinu ya kuwatisha ili wanyamaze.
Mi nnavyojua ni kwamba CDM wameingia kwenye mtego wa wa CCM kupoteza muda wa kupigania katiba mpya.
Hapo wataundiwa kesi waanze kushinda Mahakamani mpk uchaguzi mkuu bila katiba mpya.
Na CDM watashiriki tena huo uchaguzi chini ya tume hii hii.
 
Upuuzi wa dikteta Samia unaendelea, hawezi kutoa zetu bandari zetu zote watanganyika kwa wajomba zake kama ni mali ya familia yao halafu tunyamaze, Never.

Mapambano yataendelea tu.
Endeleeni tu na bandari isiyowahusu mpaka mzeeke, lkn hakuna kitakachobadilika
 
Mi nnavyojua ni kwamba CDM wameingia kwenye mtego wa wa CCM kupoteza muda wa kupigania katiba mpya.
Hapo wataundiwa kesi waanze kushinda Mahakamani mpk uchaguzi mkuu bila katiba mpya.
Na CDM watashiriki tena huo uchaguzi chini ya tume hii hii.
Umepotoka!!
 
Tumemis zile hekaheka za kibatala akiwapelekea moto hao manjagu na mashahidi wa mchongo akina swila na kingai mpaka wakawa wanajikojolea.....

Kama vp kesi ziende mahakamani masese aingie kazini
 
View attachment 2692232
Baada ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu. Leo DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo kuwakabili. Madalali wa bandari zetu wasitutishe!

Tundu Lissu
Julai 18, 2023

View attachment 2692285
Barua ya wito wa Polisi


====

Mnamo jana, Julai 17 Mdau wa JF alidokeza kuwa Lissu na Mbowe walikuwa wanasakwa DOKEZO - Lissu na Mbowe wanatafutwa kukamatwa lakini Lissu aliifahamisha JF "Sijazisikia tetesi hizo. Kama ni za kweli, itakuwa ni mara ya kwanza kwa mimi au Mwenyekiti kukamatwa?"
Polisi siku hizi wanachunguza maneno yenye staha😃. Better yangekuwa matusi.
So siku hizi wana deal na hisia za watu😀
 
nini kuitwa ofisini

Lipumba wa 2000 alikula rungu la Mkono akavunjwa mkono

Mrema yule wa 1995 alikula mvua za kutosha za mabomu ya Machozi wakati wa Mahita

Slaa wa 2010 alichezea kichapo cha Unga Limited usiku wa manane
 
Tundu Lissu ana hoja nzuri sana, shida inakuja lugha anayotumia kuwasilisha/kukosoa ina matusi na kejeli ndani yake.

Kwa mtu msomi kama yeye sipendezwi na kile anachokifanya na kwa kiongozi mwenye asili ya hasira hashindwi kuchukua hatua kali dhidi yake.
 
Back
Top Bottom