Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili

Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili

TUACHE KUCHANGANYA KWA MIHEMKO YA KISIASA NA PROPAGANDA ZA KIJINGA KWENYE TAALUMA YA SHERIA. MFANO HALISI NI HUU HAPA
SABABU ZA KUKAMATWA WAKILI PETER MADELEKA

Mnamo mwaka 2020 Wakili Peter Madeleka alikamatwa na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi no. 40 (Economic case no 40/2020) katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha. Katika kesi hiyo alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi (forgery) kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Adhabu (Penal Code) kifungu cha 337 cha sheria hiyo. Pia alishtakiwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumu ( Anti Money laundering Act).

Wakati shauri lake linaendelea aliomba kufanya makubaliano na serikali ( Plea Bargaining) na taratibu zote za kufanya makubaliano zilifuatwa na ndipo aliachiwa huru.

Mara baada ya kuachiwa huru kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii Wakili Madeleka aliendelea kuchapisha habari kuwa alilazimishwa kukiri kosa na aliekuwa mkurugenzi wa mashtaka.

Baadae alifungua kesi katika mahakama kuu akipinga taratibu hizo lakini maombi hayo madogo yalitupwa nje kwa kuwa mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri Hilo.

Ndipo alifungua shauri hilo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kupinga maamuzi hayo lakini mahakama ilitoa maamuzi kuwa taratibu zote za makubaliano ( plea bargaining )zilifanyika sawa.

Baada ya maamuzi hayo alikata rufaa tena na kuja na sababu tofauti ambapo mahakama ilisikiliza Hoja zake na kutoa amri kuwa taratibu za makubaliano hazikuzingatiwa hivyo kuamuru status ya kesi yake kurudi kama ilivyokuwa awali.

Baada ya maamuzi hayo Wakili Madeleka alikamatwa tena ili kuweza kuendelea na kesi yake ya msingi na kwa kuwa makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.

UPOTOSHAJI:

Jamii inapotoshwa na kuaminishwa kuwa mshtakiwa ameshikwa kutokana na kutoa maoni yake juu ya Mkataba wa DP world na Serikali ya JMT jambo ambalo si sahihi.

Ikumbukwe watu mbalimbali wametoa mawazo yao na hakuna yoyote alieshikwa.
Hata katika kesi iliyofunguliwa na mawakili yeye si miongoni Mwao.

Hivyo ifahamike na itambulike mshtakiwa ameshikwa kwa makosa yake aliyoyafanya huko nyuma ambapo yeye mwenyewe alikiri na sasa ameomba mahakama ifute maamuzi hayo hivyo kesi yake ya msingi inaendelea.

Ninyi wevi wa rasilimali za Taifa, endeleeni kujifariji lakini hamtashinda.

Kwa ushenzi wenu mnawabambikia watu kesi, mnawaweka mahabusu na kuwatesa ili kuwalazimisha wakiri mnayoyataka, halafu bila aibu mnakuja hapa kusema eti alikiri.

Kama kulikuwa na kesi genuine, mlishindwa nini kwa mwaka mzima kuufikisha ushahidi mahakamani?
 
Sijawahi kupoteza imani na Lisu, japo alikosea kwa kukubali kumpokea jizi Lowassa ndani ya CDM na kupewa nafasi adhimu ya kugombea urais wakati alikuwa hastahili.
Lowasa alikuibia nini?
 
Hivi vitendo vya kamata kamata mara weka ndani baada tu ya kuonesha kutokubaliana na mkataba wa bandari, sasa inaonesha dhahiri pasi na shaka kuna kitu hakipo sawa.
Hawa watu, kwenye huu uporwaji wa bandari za Tanganyika, kuna mengi maovu yaliyojificha.

Wanahangaika sana kuwafumba watu midomo, lakini kamwe hawatashinda. Wataaibika tu.
 
Kamata hao weka kolokoloni wasote kabisa mpaka 2026. Mbowe na Lisu ni wahuni wahuni, walitutukania Dkt Magufuli mpaka wakafanya sherehe ya kifo chake na wameyakoroga tena kwa Mama, acha wakomeshwe!

Ningekuwa polisi ningehakikisha namrusha kichura chura lisu na mbowe halafu namtandika mbowe kirungu utosini huku analia anaruka kichura chura na lisu namchapa kirungu cha kwenye magoti namrusha kichura chura akome.
Mbususu iliyochacha
 
Kumkamata mtu kisa kapinga jambo flani, hii ni hatari. Na hao Polisi jinsi ambavyo hawatumiagi akili kwenye kuamua, ndo kabisaaa.
 
Hawa watu, kwenye huu uporwaji wa bandari za Tanganyika, kuna mengi maovu yaliyojificha.

Wanahangaika sana kuwafumba watu midomo, lakini kamwe hawatashinda. Wataaibika tu.
Hakuna maovu mbona kila kitu kipo sawa
 
Nakumbuka Lisu aliwahi kumuuliza swali Afisa mmoja wa jeshi la polisi mahakamani wakati anatoa ushahidi(Nimesahau maneno aliyomuuliza) ikabidi yule Afisa aombe kwenda toilet [emoji28]
Nakataa sio LISSU
 
Mi nnavyojua ni kwamba CDM wameingia kwenye mtego wa wa CCM kupoteza muda wa kupigania katiba mpya.
Hapo wataundiwa kesi waanze kushinda Mahakamani mpk uchaguzi mkuu bila katiba mpya.
Na CDM watashiriki tena huo uchaguzi chini ya tume hii hii.
Kama nimeanza kukuelewa hivi
 
Mi nnavyojua ni kwamba CDM wameingia kwenye mtego wa wa CCM kupoteza muda wa kupigania katiba mpya.
Hapo wataundiwa kesi waanze kushinda Mahakamani mpk uchaguzi mkuu bila katiba mpya.
Na CDM watashiriki tena huo uchaguzi chini ya tume hii hii.
Kama nimeanza kukuelewa hivi
 
Upuuzi mtupu. Hizo kesi zote za kubambikia watu walisema wanazifuta. Sahizi kwa sababu mtu amewakosoa, wanazirudisha! Ni uwendawazimu wa madaraka kwa nia ya kukomoa watu.

Kama zingekuwa ni kesi halisia, ilishindikana vipi kwa zaidi ya mwaka mzima, serikali ishindwe kupata ushahidi?

Watu wajinga wanajifanya wana akili kuliko watu wenye akili. Wacha wenye mamlaka wajifariji kwa mbinu zao za kishetani kuwakomoa watu, lakini hawatashinda.

Wala hatutashangaa kuona watu wote walio mstari wa mbele katika kupinga wizi wa rasilimali za nchi unaofanywa na watawala kupitia uwekezaji magumashi, wakiwekwa mahabusu na wakibambikiwa kesi. Wamekwishaanza na Dr. Rugemeleza, Mwambukusi, Madeleka, Lisu, na bila shaka watafuata wengine. Lakini hawatafanikiwa. Shetani humpa mwanadamu ushindi wa muda ili kumpumbaza, lakini hawezi kumpa ushindi wa kudumu.
Usichanganye Mihemko na Sheria .Kama angekuwa ameona kuwa kaonewa jibu rahisi angesubiri kesi yake iishe ashinde ila yeye mwenyewe aliomba kupatana na DPP sasa OPP kamdikiliza akalipa mambo yakaenda fresh sasa leo amejilaumu maamuzi yake mwenyewe amekwenda kusema hakubaliani na hayo maupuuzi ya kupatana hivyo yupo tayari kuendelea na kesi hivyo karudi jela ili apambane kushinda kesi . Msimuhusishe Madeleka na kesi ya Bandari yeye anapambana na kesi ya Uhujumu uchumi ikiwemo kughushi .Asitafute kiki kwenye Bandari aongeze juhudi ashinde kesi .
 
Baada ya mawakili Mwabukusi, Madeleka & Ruge Nshala, sasa ni zamu yangu. Leo DCI Kingai ametuma watu kuleta barua ya kuripoti ofisini kwake. Wamerudi nayo baada ya kujulishwa niko nje ya nchi. Nitarudi wiki ijayo kuwakabili. Madalali wa bandari zetu wasitutishe!

Rais anayesaini mikataba ya hovyo kuliko hata wa Chifu Mangungo; anayegawa bandari zetu zote na nia za usafirishaji kisirisiri kwa wageni; anayelazimisha Bunge kubariki uharamia huo, na anayenyang'anya watu wetu ardhi zao na kuwapa wageni, anastahili kukosolewa kwa staha gani?

Tundu Lissu
Julai 18, 2023

View attachment 2692285
Barua ya wito wa Polisi


====

Mnamo jana, Julai 17 Mdau wa JF alidokeza kuwa Lissu na Mbowe walikuwa wanasakwa DOKEZO - Lissu na Mbowe wanatafutwa kukamatwa lakini Lissu aliifahamisha JF "Sijazisikia tetesi hizo. Kama ni za kweli, itakuwa ni mara ya kwanza kwa mimi au Mwenyekiti kukamatwa?"
Wakishamalizana na hawa viongozi wa kisiasa, tunaofuatia ni raia
 
Mlisema Jiwe ni mbaya.

Bora mtu unayejua ni mbaya utamkwepa ila Delila mtanikumbuka.
 
Mchungaji ameelezea jinsi safari ya kuwaondoa Wana wa Israel Utumwani Misri na kuwapeleka nchi ya Ahadi ilivyokuwa Ngumu

Mchungaji amesema wakiwa katikati ya safari Wana wa Israel wakamlalamikia Musa kwamba mbona wanakufa Njaa jangwani ? Bora awarudishe Misri kwa sababu kule hata wakifa kuna makaburi ya kuwafikia .

Niwatakie siku njema
 
Tangu lini Mwanamke akawa na vinasaba vya uongozi, apambane amalize mwaka wake mmoja na nusu uliobaki akapumzike Nungwi Zanzibari alee vitukuu.
Hukuwahi kuwasikia kina Angela Merkel, Margareth Thatcher, Golda Meir na wengineo?
 
Back
Top Bottom