Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
TUACHE KUCHANGANYA KWA MIHEMKO YA KISIASA NA PROPAGANDA ZA KIJINGA KWENYE TAALUMA YA SHERIA. MFANO HALISI NI HUU HAPA
SABABU ZA KUKAMATWA WAKILI PETER MADELEKA
Mnamo mwaka 2020 Wakili Peter Madeleka alikamatwa na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi no. 40 (Economic case no 40/2020) katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha. Katika kesi hiyo alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi (forgery) kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Adhabu (Penal Code) kifungu cha 337 cha sheria hiyo. Pia alishtakiwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumu ( Anti Money laundering Act).
Wakati shauri lake linaendelea aliomba kufanya makubaliano na serikali ( Plea Bargaining) na taratibu zote za kufanya makubaliano zilifuatwa na ndipo aliachiwa huru.
Mara baada ya kuachiwa huru kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii Wakili Madeleka aliendelea kuchapisha habari kuwa alilazimishwa kukiri kosa na aliekuwa mkurugenzi wa mashtaka.
Baadae alifungua kesi katika mahakama kuu akipinga taratibu hizo lakini maombi hayo madogo yalitupwa nje kwa kuwa mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri Hilo.
Ndipo alifungua shauri hilo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kupinga maamuzi hayo lakini mahakama ilitoa maamuzi kuwa taratibu zote za makubaliano ( plea bargaining )zilifanyika sawa.
Baada ya maamuzi hayo alikata rufaa tena na kuja na sababu tofauti ambapo mahakama ilisikiliza Hoja zake na kutoa amri kuwa taratibu za makubaliano hazikuzingatiwa hivyo kuamuru status ya kesi yake kurudi kama ilivyokuwa awali.
Baada ya maamuzi hayo Wakili Madeleka alikamatwa tena ili kuweza kuendelea na kesi yake ya msingi na kwa kuwa makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.
UPOTOSHAJI:
Jamii inapotoshwa na kuaminishwa kuwa mshtakiwa ameshikwa kutokana na kutoa maoni yake juu ya Mkataba wa DP world na Serikali ya JMT jambo ambalo si sahihi.
Ikumbukwe watu mbalimbali wametoa mawazo yao na hakuna yoyote alieshikwa.
Hata katika kesi iliyofunguliwa na mawakili yeye si miongoni Mwao.
Hivyo ifahamike na itambulike mshtakiwa ameshikwa kwa makosa yake aliyoyafanya huko nyuma ambapo yeye mwenyewe alikiri na sasa ameomba mahakama ifute maamuzi hayo hivyo kesi yake ya msingi inaendelea.
Ninyi wevi wa rasilimali za Taifa, endeleeni kujifariji lakini hamtashinda.
Kwa ushenzi wenu mnawabambikia watu kesi, mnawaweka mahabusu na kuwatesa ili kuwalazimisha wakiri mnayoyataka, halafu bila aibu mnakuja hapa kusema eti alikiri.
Kama kulikuwa na kesi genuine, mlishindwa nini kwa mwaka mzima kuufikisha ushahidi mahakamani?