Tundu Lissu: Filamu ya Royal Tour ni biashara kubwa Amazon. Je, nani mwenye hakimiliki? Mgawo wetu ni kiasi gani?

Lisu mtata sana.

Chadema wameishiwa hoja!
Lissu ana hoja usimbeze! Kama CD inakodishwa Kwa elfu kumi na tatu na kuuzwa Kwa elfu thelathini na saba huoni tofauti ya elfu ishini na nne? Hiyo pesa anayeichukua ni nani kati ya mkodishaji na mweñye filamu yake? Serikali au wizara husika wajibu juu ya pesa hizi ili zijulikane zinakokwenda!
 
Kwenye vitu vya msingi unaongea ujinga hivi. Wewe utakuwa umeharibiwa maumbile
 
Tundu Lissu na WAPINZANI wa Rais Samia wamekuwa kama pakashume. Paka shume akikosa chakula anakwenda kila jalala anapekua kutafuta chakula.

Samia aliposema anacheza film ya kutangaza utalii mlibeza sana. Kisha mkasema anatumia vibaya fedha za Nchi. Serikali iliwajibu kuwa anayegharamia ni wafadhili mbalimbali.

Hatimaye mzigo umeteremka uko intact na unasoma vibaya huko majuu. Choyo kimewashika, Lissu anauliza haki ni za nani?

Hata kama haki by 100 za wanaonunua hiyo film kama akina Netflix au Histoy Channel au National Geographic, as long as itatuletea watalii, sisi kwetu hiyo ndiyo DIVIDEND yetu, Period!!

Hizo fedha za kuuza film ni peanut
 
Serikali haikutoa hata senti moja. Wamesema ni fedha za wadau wengine.
Serikali ndio ilizikusanya hizo pesa kutoka kwa wadau wengine ili kuzitumia kwa maslahi ya umma wa watanzania Na ndio kazi ya serikali ya siku zote. Muongozaji wa hiyo movie hakutoa hata senti tano.

Sasa swali linakuja, pesa za mauzo ya hiyo filamu atalipwa nani?
Watalipwa waandaji?
Italipwa serikali ya Tanzania?
Watalipwa wadau waliochangia?
 

Fedha za kukodi mfumo wa IT wa Tanesco analipwa nani? Na fikiri maarifa ni hayohayo yaliyo yafanya haya yote.
 
Inategemea hayo makundi uliyoyataja yalikubalianaje
 
That's pety buss
Muhimu kwetu ni multiplier effect yake kwa sector utalii, na uchumi wetu kwa ujumla
Duuuh! watu hawajui kua kichwa chako ni chakubebea meno tu.Wewe bila shaka unajua watanzania tulishaacha kulipa hata kodi,na Rais ametoa pesa zake akishirikiana na CCM kuitengeneza hiyo filamu.Unajua Rais ni tajiri sana,hivyo CHADEMA na wale wasiokua na vyama hawajachangia chochote kwenye pesa zilizotumika kutengeneza filamu.Pole sana.
 
Pesa zikishaingia serikalini huwa ni mali ya umma, mali ya serikali, haijarishi ni nani alizitoa.
Kikubwa sote tunakubaliana kuwa serikali ndio ilizikusanya kutoka kwa wadau mbali mbali (na sio muongozaji wa filamu alizitoa mfukoni mwake), tuna haki kujua pesa za mauzo ya filamu zitakwenda mfukoni kwa nani?

Hoja hujibiwa kwa hoja, na uwazi kwenye mikataba ya kipesa ni jambo la msingi sana.
 
Ulisema kitndo cha marehemu JPM kuzuia makinikia Taifa litashitakiwa na kufilisiwa. Huo mpango wa kulifilisi Taifa letu bado upo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…