Tundu Lissu: Filamu ya Royal Tour ni biashara kubwa Amazon. Je, nani mwenye hakimiliki? Mgawo wetu ni kiasi gani?

Tundu Lissu: Filamu ya Royal Tour ni biashara kubwa Amazon. Je, nani mwenye hakimiliki? Mgawo wetu ni kiasi gani?

Hata Chadema ni chama Cha wananchi, wamesajikiwa, wanavuta ruzuku sometimes, na Sasa wanatuchangusha, hivyo kwa kuwa wanajitambulisha kupitia umma, wanakaguliwa na CAG, wao pia lazima tuwajadili
Kwa kazi ya uchawa wa mama, wewe ni mwepesi sana. Uachiwe idara ya vijembe kwa wavaa vijora.
 
Kama lile jiwe kubwa la Ruby linauzwa Dubai na serikali haina habari
 
Out of context, zinaongelewa pesa za umma sio za ponjoro.
Acheni gubu basi kuwa mpinzania mnadhani ni kupinga kila kitu? wewe unajuwa gharama za kujitangaza? unataka kutangaza nchi halafu unataka ulipwe wewe? acheni ujinga huu aje mtu aseme napiga picha biashara yako halafu umwambie hapana nilipe pesa mbona ujinga huu. Nchi haifanyi biashara katika hili lengo ni kuitangaza nchi ili sector ya utalii ikue wale wanapokuja ndio pesa inaingia katika nchi malengo ya muda mrefu. kuna nchi wananunua dakika tu CNN huko kutangaza nchi yao unajuwa wanalipa ngapi? Visit Rwanda unajuwa wanalipa ngapi? anakuja mtu ana ushawishi mkubwa katika media USA anafanya biashara lakini wakati huohuo na yeye anatengeneza pesa lakini anakutangaza duniani wewe ukatae eti nilipe, acheni ujinga sio kila jambo kupinga tu.
 
Ameandika Tundu Lissu katika akaunti yake ya Twitter

Movie ya Royal Tour kumbe ni biashara kubwa Amazon. Kukodi Sh. 13,930, Kuuza sh. 37,150. Swali langu ni je, mwenye hatimilki ya movie - & kwa hiyo mmiliki wa pesa hizo - ni nani? Je, mgawo wetu ni kiasi gani kwa vile main character ni Rais wetu & location ya movie ni mbuga zetu?

Hizi hela zote usikute zinakwenda kwa Kikwete au Mama mwenyewe, zinazobaki zinakwenda chamani if that.
 
Swali la Lissu ndo lipo hapo sasa, hiyo faida ya 50% inakwenda wapi?

Wanakula watanzania waliozoea kula
Hata yeye ni miongoni wa wafaidika wakati alikuwa mbunge

Ila wengine hawaelewi kuwa hela na faida Amazon zipo
Hela zinapigwa kutwa ila yeye pia anatamani apate pia
Nchi inspigwa sana
Mbona anauliza kama illiterate? Eti mgao tunapata ngapi
 
Rais ni taasisi na ilitumika ipasavyo katika filamu hii. Hivyo naamini nchi itapata mgao wake. Wenye dgamana wanapaswa kutufafanulia. Pili, filamu hii itachagiza sana kukua kwa sekta ya utalii na nchi kupata mapato maradufu.
 
Chadema walivuta mamia ya mamilioni kwa sabodo ili wajenge Ofisi ya makao makuu ya chama, Hela wakagawana Mnyika ...Mbowe ...na Lissu. Mpaka Leo chama kimepanga katika Ofisi za baba mkwe wa Mbowe Mzee Mtei, yaani chama kinamlipa Kodi baba mkwe wa Mbowe, Chadema tusitarajie kujengewa Ofisi ya chama, wanafamilia wanapeana kodi
nje ya ulingo
 
Hata Chadema ni chama Cha wananchi, wamesajikiwa, wanavuta ruzuku sometimes, na Sasa wanatuchangusha, hivyo kwa kuwa wanajitambulisha kupitia umma, wanakaguliwa na CAG, wao pia lazima tuwajadili

Pamoja na hayo,tujadili kwanza jambo kubwa lililopo mbele yetu.
 
Chadema walivuta mamia ya mamilioni kwa sabodo ili wajenge Ofisi ya makao makuu ya chama, Hela wakagawana Mnyika ...Mbowe ...na Lissu. Mpaka Leo chama kimepanga katika Ofisi za baba mkwe wa Mbowe Mzee Mtei, yaani chama kinamlipa Kodi baba mkwe wa Mbowe, Chadema tusitarajie kujengewa Ofisi ya chama, wanafamilia wanapeana kodi
Wahusika wamekusikia, haya jibu hoja ya Lisu!!
 
Ameandika Tundu Lissu katika akaunti yake ya Twitter

Movie ya Royal Tour kumbe ni biashara kubwa Amazon. Kukodi Sh. 13,930, Kuuza sh. 37,150. Swali langu ni je, mwenye hatimilki ya movie - & kwa hiyo mmiliki wa pesa hizo - ni nani? Je, mgawo wetu ni kiasi gani kwa vile main character ni Rais wetu & location ya movie ni mbuga zetu?

Kwa kinyakyusa tunaita A PATENT
 
Lengo ni kutangaza vivutio vya utalii Tanzania. Katika hali ya kawaida ili kutangaza biashara inabidi umlipe advertising agency. Tumeambiwa hatujalipa chochote kuandaa royal tour. Nadhani hii advertisement ambayo itafikia mamilioni duniani is a fair deal.Kazi iendelee.
 
Kwa hiyo Rais na msafara wake nani ameulipia? Kukaa ulaya muda wote nani analipa gharama? Hizo billion saba zilitolewa na akina nani?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wadau wa maendeleo
 
Kama tunapata % tu nitamdharau sana bibi Hangaya, nikiangalia ule msafara na posho walizokuwa wakilipana watu kwa siku wakati hiyo filamu ikirekodiwa, kwamba serikali ndio imegharamia halafu sisi tusipate chochote narudia tena nitamdharau sana huyu Bibi.
hana cha kupoteza akidharauliwa na wewe chakubanga huna msaada wowote zaidi ya kupost ushuzi wako apa.
 
Ameandika Tundu Lissu katika akaunti yake ya Twitter

Movie ya Royal Tour kumbe ni biashara kubwa Amazon. Kukodi Sh. 13,930, Kuuza sh. 37,150. Swali langu ni je, mwenye hatimilki ya movie - & kwa hiyo mmiliki wa pesa hizo - ni nani? Je, mgawo wetu ni kiasi gani kwa vile main character ni Rais wetu & location ya movie ni mbuga zetu?

Hela hiyo iende kwa mwenyekiti wa Chadomo ili inunulie mizinga
 
Shida umejibu kimpasho na huwenda ukawa na hoja ila uwasilishaji wako umefanya uonekana mwehu hebu rudia na uone ulivyoandika

Lisu kama mtanzania ana haki ya kuuliza na anawakilisha wengi ambao wamataka kujua hili.

Ila kwasababu una chuki moyoni mwako umeandika kama mwimba taarabu za mipasho
A silly question deserves a silly answer, period.

Unauliza swali la mipasho unajibiwa kimipasho. Maswali mengine anauliza kutekeleza majukumu yake kwa wanaomuweka Belgium.

Yeye mwenyewe Lissu nani anallipa gharama zake za kuishi Belgium?
 
Back
Top Bottom