Tundu Lissu hajawahi kunyamaza na hatonyamazishwa kamwe

Bado sija amini kama watatokea wapinzani wakweli kama hamisi kalage na richadi kilango na mbonge munanga na kasela bantu lakini hawa akina shibuda na choyo hawa ni sawa na mpiga marimba anacheza na makalio tukubali matokeo
 
ujinga mtupu, mbona jana katoka kimyakimya?
 


Hata risasi haiwezi kumnyamazisha?
 
Kumbukumbu ni muhimu na kama huna ndio maana wengine hufanya 'research' ili wapate uhalali wa kuongea.
Wengi wanaomuandama TL leo wakati JK anatoa hiyo kauli walikuwa hawana hata ndoto za kushika vyeo walivyo navyo. Wangelikuwa wanachimba chimba basi wangelimfuata kwanza JK awaeleze ni kwa nini alisema hivyo. Sasa angalia gharama zote walizotumia lakini yuko nje wakati angeweka bando ya 250/- wangelimpigia akaja mwenyewe na hizo gharama zingine wakapeleka kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa ...maana nimeona chanel ten huko Simiyu madawati yametosha mpaka mengine hayana madarasa ya kuingizwa hiyo yanakaa tu nje!
 
Bado sija amini kama watatokea wapinzani wakweli kama hamisi kalage na richadi kilango na mbonge munanga na kasela bantu lakini hawa akina shibuda na choyo hawa ni sawa na mpiga marimba anacheza na makalio tukubali matokeo
kweli, hawa wacheza malimba wa nzega, hawajaenda kuwaona wahanga wa moto kule monduli halafu wanajazana mahakamani wauze sura kwenye magazeti.
 
Hakuna mahali popote katika dunia hii ambapo dikteta aliwahi kushinda , fanya utafiti .

Waende kumuulize Wakili wa serikali alivyokuwa mdogo kama piriton mbele ya ajuaye sheria za Dunia na ya mwaka gani utadhani ameeziandika yeye. Huyu si mwingine ni kamanda wa ukweli LISSU.

Ukitaka kumpata huyu kisheria inabidi ujipange haswaaaaa. Na ndio maana walitaka wamchukue Wakili wa LISSU ili wamshinde na bado Wakili Peter kawatolea nje.

Achana na CHADEMA imejaa wanasheria.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Tatizo kubwa la huyu bwana ni kutokujua nini anachokifanya na ni kwa maslahi ya nani. Wenzie wenye akili nzuri hizi harakati wanafanyia nje ya mikoa yao. Ndiyo maana utakuta mikoa ya wafamaji wenzie at least hali si mbaya sana. MKOA anakotoka huyu bwana ni hali ngumu sana kimaendeleo. Ni moja kati ya mikoa maskini kabisa hapa Tanzania. Vita ikipiganiwa katika nchi yako, hata kama utashinda lakini utakuwa umepata hasara kubwa. Ni vema akabadili staili, badala ya kuhamasisha maandamano aanze kuhamasisha maendeleo katika mkoa wake ili awe sawa na wenzie. Kwa hilo hata mimi ningeona kama yuko vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…