Tundu Lissu hana mgogoro na utawala, ana mgogoro na chama chake. Hata akirudi hajui atafanya nini

Ulitakaaje wewe?? Waeleweke ili ubebe agenda ukaanike huko Lumumba au!?
Hakuna hoja ya chadema kwa sasa yenye mashiko unayoweza kuianika lumumba ikakauka zote mbovu
 
Kwanini unamuita Lowassa mtu wa hovyo?
Kwangu mimi lowasa ni miongoni mwa watanzania wa ovyo.

Amewahi kuchunguzwa na serious fraud office ya Uingereza kuhusiana na jumba alilonunua London, akakingiwa kifua na wahujumu wenzake ndani ya CCM.

Wewe unamuona mtu wa maana?!
 
Nilipomsikia akisema "tutashtakiwa MIGA", "Tanzania inawahitaji wazungu kuliko wazungu wanavyoihitaji Tanzania" nkajua sasa basi. Hivi huyu jamaa aliwaza angepata urais kwa kauli kama hizo? Watu wanamoverrate sana Lissu lakini siyo smart kisiasa.

..kwani hatuwahitaji wazungu?

..tungekuwa hatuwahitaji tungesamehe trillion 350++ na kuchukua kishika uchumba toka kwa barrick?

..na unaishi dunia gani kiasi kwamba hujui kuwa acacia walitupeleka mahakamani? Au ulikuwa unasubiri Magufuli na Polepole wakutaarifu?
 
If opposing views are rubbish, then they should be responded to accordingly!
Always remember that your trash is another man's treasure. The views you cherish might as well be rubbish to other people.
 
MATAGA MNAHANGAIKA NA CHADEMA KULIKO WANACHADEMA WENYEWE Mwendazake alihangaika nayo akawanunua Wabunge na Madiwani akawabambikizia KESI za Mauaji UHUJUMU UCHUMI na UGAIDI lakini Chadema haikufa akafa yeye
 
Acacia kutupeleka mahakamani ni maamuzi yao, walikuwa wakitetea maslahi yao. Hilo halishangazi. Kinachonishangaza ni huyu mtu aliyekuwa akijiita mwakilishi wa wananchi kusimama upande wa mabeberu kinyume na maslahi ya nchi. Na msilete arcadabra mnazotumia kumtetea Lissu kuhusu hili. It was clear kwa mtanzania wa kawaida kwamba Magufuli was trying to do something positive kwenye inshu ya madini, na Lissu alikuwa kinyume. Sasa weka na kauli zake zingine za kijinga zilizozidi kumuexpose jinsi alivo kibaraka. Halafu etu huyu ndiye mlimweka agombee urais.

Kuhusu hilo la Tanzania kuihitaji mzungu kuliko mzungu anavyoihitaji Tanzania njooni na slogan hiyo tena 2025. Afu tutatalk later baada ya matokeo ya kura.
 
Ualimu vyuo vikuu una vigezo vyake
Vigezo my foot!

Hao wenye vigezo wamefanya nn cha maana zaidi kunywa pombe, ngono na upuuzi mwingine?

Wana tija gani ktk taifa hili? Vigezo uchwara!
 

..nadhani una tatizo la uelewa.

..njia alizotumia Magufuli hazikuwa sahihi.

..nia njema inatoka wapi ikiwa tuliandaa ripoti za uchunguzi za hovyo-hovyo ambazo hatuwezi kuzitumia popote kudai HAKI yetu?
 
Unaonekana una njaa sana, kila issue muhimu inapoongelewa unawaza kula tu.
Kama Tanzania hawakuacha chanxo cha mapato kutokana na kukosa kwao ubunge 2020, sioni tatizo wakiendelea kukaa Ulaya na Marekani, tena chama chao hata ruzuku siku hizi hakina, unataka wakirudi wakale polisi?
 
Always remember that your trash is another man's treasure. The views you cherish might as well be rubbish to other people.
1+1=2, hakuna ubishi hapo! unless ni matrimonial mathematics. Arguments zingine ziko hivyo, mathematically calculated
 
Tatizo Lisu kwa sasa hajielewi. Siasa za bongo zimebadilika lakini yeye bado kabakia enzi za awamu ya tano.
 
Haya ndio madhara ya kushindana na mtu badala ya kudeal na issues.

Lisu alimfanya Magufuli kama ndio mtaji wake kisiasa.

Yaani Magufuli ndio alikua political agenda yake na njia ya kujipatia umaarufu. Akimtukana basi anajiona bonge la mwanasiasa.

Sasa hayupo he is no longer relevant.
 
Yani umenipiga na kitu kizito cha 'ulaia', nikaona isiwe taabu... wacha nihame uzi kabisaaa.
 
..nadhani una tatizo la uelewa.

..njia alizotumia Magufuli hazikuwa sahihi.

..nia njema inatoka wapi ikiwa tuliandaa ripoti za uchunguzi za hovyo-hovyo ambazo hatuwezi kuzitumia popote kudai HAKI yetu?
Magufuli kwa nafasi aliyokuwa nayo kama Rais (akipokea reports kutoka kwa washauri mbali mbali chini yake), na kwa uzoefu wake akiwa mjumbe wa baraza la mawaziri kwa miaka 20, alikuwa na data za kutosha kuhusu hili na kujua njia gani sahihi ya kutumia. Ulitaka tumsikilize Lissu kuliko amiri jeshi mkuu wa nchi?

Na hata kama njia iliyotumika haikuwa sahihi ndivyo mapambano yalivyo. Hakuna njia moja itakayokuwa effective aslimia 100. Cha muhimu hapa ilikuwa nia, uthubutu, na mwanzo (initiative) katika kuwaonyesha mabeberu kwamba tunahitaji mabadiliko. Na vyovyote vile utakavyolitazama huwezi kuunderestimate impact ya hizo initiatives za Magufuli kwenye madini.

Kinyume chake impact za tantalila za Lissu zipo wazi kabisa kisiasa kwake na kwa chama chake. Jamaa alijiexpose jinsi asivyokuwa reliable (na by extension chama chake) kusimama kwa ajili ya maslahi ya nchi.
 

..hakutumia njia sahihi ndio maana Prof.Kabudi amejitokeza na kukiri kwamba madai dhidi ya acacia yalikuwa sio sahihi/ uongo, na wengine wameita kanyaboya.

..kwa msingi huo huwezi kusema Magufuli alikuwa anatetea maslahi ya nchi. Huwezi kumuita mzalendo kwasababu nchi haitetewi kwa njia za uongo, hila, na ulaghai.

..Lissu ni Mtanzania wa kwanza aliyekuwa na ujasiri wa kusema ukweli kuhusu ripoti na madai ya Magufuli. Prof.Kabudi amepata ujasiri wa kutubu na kusema ukweli 5 yrs later.

..sakata zima la makinikia lilikuwa na lengo la kuwalaghai wananchi na kujiongezea umaarufu wa kisiasa.

..Kama Magufuli alikuwa serious na mwenye uchungu kuhusu rasilimali zetu angechukua hatua kali dhidi ya vigogo waliotumia madaraka yao vibaya kuliingiza taifa ktk mikataba ilitusababishia hasara.

..Vilevile asingemteua Deo Mwanyika, ambaye aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Acacia hapa nchini kuwa mgombea ubunge wa Ccm.
 
Tanzania itajengwa na Mwenye Enzi Mungu mwenyewe!
Kama alisimamisha kuta za Israel sembuse Tanzania [emoji1241]!
Usiangalie 1+1=2 angalia kwa jicho la tatu ambalo 1+1=8
Unajiuliza kwa vipi!
Njia za Mwenye Enzi Mungu sio za binadamu!
AMINI
 
..sakata zima la makinikia lilikuwa na lengo la kuwalaghai wananchi na kujiongezea umaarufu wa kisiasa.
Kuna USD 300m+ ambayo kuna pahala umeiita kishika uchumba, nayo tulilaghaiwa? Kwamba hakuna ahadi kama hiyo iliyotolewa na acacia?

Kama ahadi ilitolewa, kwanini kampuni kubwa kama acacia itoe ahadi ya kulipa kiasi hicho kikubwa cha pesa kwenye madai ya kilaghai/kitapeli?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…