Lisu huwenda akawa mhamiaji wa maisha huko Brazos! Na pengine tayari ana ulaia wa huko!
Na ili aje huku, Chadema wananjia moja tu ya kumfanya aje!
Ni kumruhusu agombee nafasi ya Urais, na hili lijulikane pia, akishiriki kugombea nafasi hiyo, ikitokea ameshindwa! Hawezi ishi nchini kamwe!
Na huo ndio uchaguzi wake Kwa sasa!
Tusitaniane bajameni, Ulaya ni Ulaya tuu, Africa itabaki kuwa Africa tu
Ole wa mtu mweusi aonje maisha ya ulaya tena Kwa kibali cha huko, na akapata walau ajira!!! Hawezi kumbuka home!
Waulizeni wazenji, wako tayari familia wauze nyumba na viwanja ili tu mmoja kati yao wa familia hiyo, azamie ulaya, na akizamia, atahakikisha anatuma pesa nyumbani ili kuijenga tena familia hiyo!
Na Zanzibar inajengwa Kwa njia hiyo, na wahamiaji wa ulaya Zanzibar huenda Kwa nia hiyo!
Nani anayebeza maisha ya Ulaya?
Na ndiyo maana hata marais wa nchi za Ki Africa, huwekeza huko ulaya, na wanaishi tu huku Kwa shingo upande ila mioyo yao, iko ulaya
Africa itajengwa na watu wa kawaida saana, wenye kudharauliwa saana na kubezwa na watu weupe na siyo wanaosifiwa na wazungu,
Kwa sababu wote wansosifiwa na wazungu, kuna mawili, either wameuza utu wao, na labda mzungu ana miadi na nchi yake!
Tanzania nakupenda!