Tundu Lissu hana mgogoro na utawala, ana mgogoro na chama chake. Hata akirudi hajui atafanya nini

Mkuu, kwa idadi ya wajinga nchini anaweza kupata. Umewahi kujiuliza kwanini mtu wa ovyo kama lowasa alipata mamilioni ya kura?!

Tunayo mamilioni ya raia wasioweza kufikiri, wanasubiri viongozi wao watoe matamko wao watekeleze.
Dah! Umeongea point... Hii ndiyo inafanya Tanzania tuwe na siasa za ubabaishaji uongo mwingiiiii.... Iwe upinzani iwe ccm
 
Kabudi si anacheza na upepo unavyokwenda? Maza kajitanabaisha kama mtu asiyependa kutibua maji yaliyotulia kwenye glass, hataki kuwavuruga "wakubwa" ndiyo maana anacheza appeasement game. Walio chini yake lazima watakuwa bendera fata upepo. I don't like that type of people, by the way, wasio na misingi yao binafsi. So tuichukulie toba ya Kabudi for what it is, appeasement game.

Lissu ni mtanzania wa kwanza, pengine siyo wa kwanza, kuuonyesha umma kwamba alaaniwe yeye awekaye tumaini lake kwa wanasiasa. Hakuna chochote alichokifanya Lissu katika sakata la makinikia kilichoonyesha kwamba yupo upande wa nchi iliyokuwa ikimlipa mshahara. Alifeli na alifeli pakubwa.

Who cares kama kwa Magufuli sakata la makinikia lilikuwa na lengo la kumpatia umaarufu? Umaarufu gani aliutaka zaidi ya kuwa rais wa nchi? Na kama kweli kuthubutu kufight kwa ajili ya mabadiliko katika mifumo ya mikataba ya madini ilikuwa na lengo la kupata umaarufu then well and good, umaarufu kwa kusudi jema. Unataka tuwe na viongozi wa nchi wasiotaka kuwa maarufu kwa kutofanya chochote katika kuibadilisha nchi?

Hayo ya Deo Mwanyika, na kile kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia mimi sijui. Ila ninachojua ni kwamba Lissu alicalculate vibaya sana moves zake za kisiasa. Sometimes wanasiasa wanapaswa kujua nini watu wanataka vinginevyo tutarudi hapa hapa na lawama zile zile za siku zote kwamba ccm mnaibiwa kura. Ndiyo ccm si watakatifu lakini kwa ukubwa wa chama (na watu wengi walio nao) wana uwezo wa mara fulani fulani kutuibulia mtu sahihi. Sasa chadema na kwa uduchu walio nao hata wale wachache wanaoonekana kama wanafanya vituko kama vya akina Lissu mtailalamikia sana katiba wakati adui zenu ni ninyi wenyewe.
 
Babu huwezi kututoa kwenye hoja yetu - hoja yetu ni Katiba mpya leo.
 
Kwangu mimi lowasa ni miongoni mwa watanzania wa ovyo.

Amewahi kuchunguzwa na serious fraud office ya Uingereza kuhusiana na jumba alilonunua London, akakingiwa kifua na wahujumu wenzake ndani ya CCM.

Wewe unamuona mtu wa maana?!
Mimi hapo nawaona hovyo wote wawili, mwizi au aliyemficha mwizi, usimuonee Lowassa peke yake.
 
Ulaia?
 

..waliotoa ahadi ya 300 mil ni barrick.

..halafu kuna taarifa za fedha hizo kikatwa /kupigwa cha juu na acacia kwasababu wanatudai.

..pia kuna taarifa za malipo hayo kufanyika kidogo kidogo na sio kwa mara moja kama Magufuli na Kabudi walivyokuwa wanadanganya.

..Magufuli hakujielekeza kutafuta UKWELI. Badala ya kupambana na waliotuibia akawa anapambana na Lissu. Kibaya zaidi ni kumuita Lissu msaliti na kumhukumu kifo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…