Kwa wizi sawa ila tumeshuhudia watanzania maelfu kwa maelfu wakiikataa CCM kwa vitendo. Tumeshuhudia mgombea wa urais wa CCM kila aendapo anakwenda na konvoi la wasanii ili kujaribu kuwashawishi watu waende kwenye mikutano yake, tumeshuhudia mgombea huyo wa CCM akifunga shule na kuagiza watumishi wa umma na wanafunzi kuvaa sare za CCM ili wajaribu kuongeza umati.
Ni ukweli usiopingika kwamba CCM imekataliwa na wananchi wa Tanzania kwa sababu kuu ya kuminya UHURU wa kujieleza, Usalama wa wananchi hasa wakosoaji wa Serikali kuwa na wakati mgumu, kupotea, kubabikiziwa kesi zisizo na dhamana na hata kuuawa, Hali ngumu ya maisha waliyonayo watu, Ajira kwa vijana ni ndoto, vyeti feki vimeancha madonda makubwa mioyoni wa watanzania wengi, kuvunjiwa nyumba bila fidia nako, kutosaidia wananchi kwenye majanga ya kitaifa kama mafuriko na matetemeko kwa sababu kwamba serikali huwa haiyaagizi haya majanga kuwafuata wao.
Kifupi CCM haiwezi kushinda hiyo kesho kutwa !!! labda wafanye hujuma ya kupindua matokeo kitu ambacho kitakuwa hatari sana kwa usalama wa nchi.