Tundu Lissu: Idadi ya wabunge wa kuchaguliwa iwiane na idadi ya raia wanaowakilisha

Tundu Lissu: Idadi ya wabunge wa kuchaguliwa iwiane na idadi ya raia wanaowakilisha

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media
Tume ya Uhusiano na Uratibu Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha ... Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema..... soma zaidi : source : Hotuba ya Jaji Josefu Warioba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Tanzania
 
Unapendekeza mbunge/muwakilishi apatikane kwenye jimbo lenye idadi gani ya watu?
Idadi ya watu isiwe kigezo pekee, Chukulia mfano mkoa wa Morogoro ulivyo mkubwa leo uweke uwakilishi kisa tu idadi ya watu huo uwakilishi utawezekana vipi mtu awakilishe kutoka Malinyi hadi Gairo?

Mfano Njombe yenye watu 250K leo ugawe majimbo mawili Mbunge atawakilisha vipi sauti za watu zilizotawanyika?

Hii formula anayopendekeza Lissu inawezekana kwenye developed world sio huku kwetu.
 
Umekwepa swali mkuu.
 
Tundu Lisu; No, You are Myopic

What you have tried to explain is totally incorrect and myopic. The focus of electing various representatives and providing infrastructure is to facilitate Provision of Services to the community.

In large urban areas, the infrastructure and governance resources are easily shared by a large number of people. Therefore, there is no need of having too many Reps.

You seem to have you mind stuck in the number of reps; and forgets the justification and cost benefit alaysis. .

You want to increase the number of MPs whenever the population increases. What is going to be the limit. Is it logical?

USA’s Constitution is over 270 years old. The population has increased more than 100 times; but their number of Representatives and Senators has remained 495 and 100 respectively.

In the same USA, due to their population sizes, California has 54 Electro Votes and Rhode Island has 2 Electro Votes. But both are represented by 2 Senators in the Senate.

Tundu Lisu, we know that you are idle over there. Use your time to study and research issues before you write. You are disheartening us to find you still providing childish postings; and therefore wasting our time.

Take care
 
Sasa nimeelewa 'Goli la Mkono' in Nape Nnauye voice.

Kuna mambo mengi ikiwemo mfumo usio na uwakilishi sawa baina ya majimbo. Bado kuna NEC kukata majina, DED kukataa kutoa fomu, DED kukimbia ofisi zao ili wasipokee fomu za wagombea wa upinzani, ......
Haya mengine ni sawa yanahitaji tiba, ila kuhusu mgawanyo wa majimbo kwa kigezo tu cha idadi ya watu si sawa. Wakoloni walitumia factor nyingi ikiwemo kabila, tamaduni na desturi za kieneo, jiografia, njia za mawasiliano ikiwemo kufikika kirahisi n.k n.k
 
SENSA NA DEMOKRASIA
Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi
Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;

Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;

Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;

Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na

Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.

Source : Hii ndiyo tofauti ya Sensa ya 2022 na zilizopita
 
Tundu Lisu; No, You are Myopic

What you have tried to explain is totally incorrect and myopic. The focus of electing various representatives and providing infrastructure is to facilitate Provision of Services to the community.

In large urban areas, the infrastructure and governance resources are easily shared by a large number of people. Therefore, there is no need of having too many Reps.

You seem to have you mind stuck in the number of reps; and forgets the justification and cost benefit alaysis. .

You want to increase the number of MPs whenever the population increases. What is going to be the limit. Is it logical?

USA’s Constitution is over 270 years old. The population has increased more than 100 times; but their number of Representatives and Senators has remained 495 and 100 respectively.

In the same USA, due to their population sizes, California has 54 Electro Votes and Rhode Island has 2 Electro Votes. But both are represented by 2 Senators in the Senate.

Tundu Lisu, we know that you are idle over there. Use your time to study and research issues before you write. You are disheartening us to find you still providing childish postings; and therefore wasting our time.

Take care

..The US has two chambers in their Congress.

..there is an upper chamber / the senate where each state is allocated 2 seats.

..there is a lower chamber / house of representatives where the number of seats for each state is based on population size.

..there have been times when some states lost or gained seats in the house of representatives because of changes in their population.

..I dont think it is correct to dismiss everything that Lissu is complaining about with regards to our election laws and processes.

..There is a serious problem of some areas in our country being under represented, while others are over represented.
 
Idadi ya watu isiwe kigezo pekee, Chukulia mfano mkoa wa Morogoro ulivyo mkubwa leo uweke uwakilishi kisa tu idadi ya watu huo uwakilishi utawezekana vipi mtu awakilishe kutoka Malinyi hadi Gairo?

Mfano Njombe yenye watu 250K leo ugawe majimbo mawili Mbunge atawakilisha vipi sauti za watu zilizotawanyika?

Hii formula anayopendekeza Lissu inawezekana kwenye developed world sio huku kwetu.

..hakuna mgawanyo wa haki, wenye uwazi, na unaoeleweka, wa majimbo ya uchaguzi.

..Lissu ametolea mfano kasoro moja tu inayohusu idadi ya watu ktk mgawanyo wa majimbo, lakini haimaanishi kwamba hana hoja nyingine.

..Umetoa mfano mzuri kuhusu mkoa wa Morogoro kuwa ni mkubwa sana.

..Lissu pia amezungumzia Morogoro kutokutendewa haki ktk uwakilishi, ukiilinganisha na mkoa kama Lindi.
 
SAMPULI / SAMPLE YA UWIANO Katika uwakilishi

Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaOfisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za MitaaHalmashauri ya Manispaa ya Temeke​

Matokeo ya uchaguzi Manispaa ya Temeke 2020​

thumb_1047_800x420_0_0_auto.jpg
Posted On: October 29th, 2020
CCM YAIBUKA KIDEDEA MAJIMBO 2 YA WILAYA YA TEMEKE NA KATA ZOTE 23
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika majimbo mawili (2) ya Wilaya ya Temeke, Jimbo la Mbagala na Jimbo la Temeke, pia kimefanikiwa kujinyakulia kata zote 23 za Manispaa ya Temeke.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi Ndg Lusubilo Mwakabibi kwa upande wa jimbo la Mbagala ambalo lina Kata 10 amemtangaza Mhe Abdallah Chaurembo kwa tiketi ya CCM kuwa ndiye mshindi wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo kwa kujipatia kura 280,003 sawa na 89.32%.

Akitoa ufafanuzi Zaidi alisema jimbo hilo la Mbagala lilikuwa na waogombea wapatao 15 kwa nafasi ya Ubunge kutoka vyama tofauti vya Siasa ikiwemo CHADEMA, ACT, SAU, NCCR, UDP, NRA, DEMOKRASIA MAKINI, UMD, DP, CUF, ADC, AAFP, ADA TADEA, na CHAUMMA.

Idadi ya wapiga kura walioandikishwa 432,326, idadi halisi ya wapiga kura 314,355, idadi ya kura halali 313,489, idadi ya kura zilizokataliwa ni 866.

Kwa upande wa Jimbo la Temeke lenye jumla ya Kata 13, Msimamizi wa Uchaguzi akiwa katika ukumbi wa chuo kikuu cha Ualimu (DUCE) amemtangaza Bi Dorothy Kilave kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge kwa kujipatia kura 192,756 sawa na 75.24%.
Aidha msimamizi wa uchaguzi alifafanua kuwa katika nafasi hiyo ya Ubunge vyama vya Siasa vilivyoshiriki ni 13 ambavyo ni CCM, ACT, CHADEMA, CUF, CCK, ADC, ADA TADEA, AAFP, NCCR, UDP, DEMOKRASIA MAKINI, NRA na UPDP.

Idadi ya wapiga kura walioandikishwa 478,630, idadi halisi ya wapiga kura 259,492, idadi ya kura halisi 258,925, idadi ya kura zilizokataliwa 567.

Mwisho Ndg Lusubilo Mwakabibi akikabidhi vyeti vya ushindi kwa wateule hao katika majimbo yote mawili amewataka wakienda bungeni Dodoma wakaisemee Temeke,walete miradi ya maendeleo na sio vinginevyo wananchi wa wilaya ya Temeke wanataka maendeleo.

KIDEDEA MAJIMBO 2 YA WILAYA YA TEMEKE NA KATA ZOTE 23
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika majimbo mawili (2) ya Wilaya ya Temeke, Jimbo la Mbagala na Jimbo la Temeke, pia kimefanikiwa kujinyakulia kata zote 23 za Manispaa ya Temeke.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi Ndg Lusubilo Mwakabibi kwa upande wa jimbo la Mbagala ambalo lina Kata 10 amemtangaza Mhe Abdallah Chaurembo kwa tiketi ya CCM kuwa ndiye mshindi wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo kwa kujipatia kura 280,003 sawa na 89.32%.

Akitoa ufafanuzi Zaidi alisema jimbo hilo la Mbagala lilikuwa na waogombea wapatao 15 kwa nafasi ya Ubunge kutoka vyama tofauti vya Siasa ikiwemo CHADEMA, ACT, SAU, NCCR, UDP, NRA, DEMOKRASIA MAKINI, UMD, DP, CUF, ADC, AAFP, ADA TADEA, na CHAUMMA. Idadi ya wapiga kura walioandikishwa 432,326, idadi halisi ya wapiga kura 314,355, idadi ya kura halali 313,489, idadi ya kura zilizokataliwa ni 866.

Kwa upande wa Jimbo la Temeke lenye jumla ya Kata 13, Msimamizi wa Uchaguzi akiwa katika ukumbi wa chuo kikuu cha Ualimu (DUCE) amemtangaza Bi Dorothy Kilave kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge kwa kujipatia kura 192,756 sawa na 75.24%.

Aidha msimamizi wa uchaguzi alifafanua kuwa katika nafasi hiyo ya Ubunge vyama vya Siasa vilivyoshiriki ni 13 ambavyo ni CCM, ACT, CHADEMA, CUF, CCK, ADC, ADA TADEA, AAFP, NCCR, UDP, DEMOKRASIA MAKINI, NRA na UPDP. Idadi ya wapiga kura walioandikishwa 478,630, idadi halisi ya wapiga kura 259,492, idadi ya kura halisi 258,925, idadi ya kura zilizokataliwa 567.

Mwisho Ndg Lusubilo Mwakabibi akikabidhi vyeti vya ushindi kwa wateule hao katika majimbo yote mawili amewataka wakienda bungeni Dodoma wakaisemee Temeke,walete miradi ya maendeleo na sio vinginevyo wananchi wa wilaya ya Temeke wanataka maendeleo.

Source : Matokeo ya uchaguzi Manispaa ya Temeke 2020

..hakuna mgawanyo wa haki, wenye uwazi, na unaoeleweka, wa majimbo ya uchaguzi.

..Lissu ametolea mfano kasoro moja tu inayohusu idadi ya watu ktk mgawanyo wa majimbo, lakini haimaanishi kwamba hana hoja nyingine.

..Umetoa mfano mzuri kuhusu mkoa wa Morogoro kuwa ni mkubwa sana.

..Lissu pia amezungumzia Morogoro kutokutendewa haki ktk uwakilishi, ukiilinganisha na mkoa kama Lindi.
Nilimsikiliza vizuri sana ile siku, ali criticize sana mfumo wa sasa wa kijiografia na mawasiliano kutumika kugawanya majimbo, akitolea mfano Morogoro yenye wapiga kura 1+ kuwa sawa na Dar es salaam yenye wapigakura 3M+.

Akaendelea kusisitiza mfumo wa majimbo kwa kuangalia kigezo tu cha idadi ya watu na kufikia hata kwenye calculations na kutaja pengine DSM ingekua na majimbo 30+ kama hiyo kanuni ingerumika.

Hoja yangu kwa nchi changa kama zetu zenye changamoto nyingi za kijamii, kieneo,kimazingira,kikabila hata kitamaduni si sawa kuleta mfumo unaofanya kazi kwenye jamii zilizopevuka kama Uingereza na marekani.

Pia nimejaribu kutoa opinion yangu kwa mujibu wa hoja zake ambazo nilizisikia hizo unazosema wewe kuwa pengine hakuzitaja lakini zilikua kwenye mawazo yake siwezi zichambua.
 
UCHAGUZI WA MWAKA 2015
MATOKEO : JIMBO LA MBEYA MJINI

Tume ya uchaguzi Tanzania iliendelea kutoa matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili nchini humo. Tume hiyo ilimtangaza mshindi wa kiti cha ubunge huko Mbeya mjini katika mkoa wa Mbeya ni mgombea wa chama cha upinzani cha CHADEMA, bwana Joseph Mbilinyi aliyetetea jimbo lake kwa kupata kura 97,675.

Baadhi ya matokeo yatangazwa

Mpinzani wake mkuu kutoka Chama cha Mapinduzi-CCM bwana Mwaliygo Shitambala alipata kura 46,894. Tume ya uchaguzi ilisema itaendelea kutoa matokeo rasmi kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa wiki nchini humo. Source : NEC na VOA Swahili
 
Wakoloni walitumia factor nyingi ikiwemo kabila, tamaduni na desturi za kieneo, jiografia, njia za mawasiliano ikiwemo kufikika kirahisi n.k n.k
Kwa hiyo bado unataka tuendelee na waliyofanya wakoloni?

Hii akili ya matope inatoka wapi?

Ndiyo, nimeandika hivi maksuddi, kwa sababu ulichoandika hapo hukutumia akili hata kidogo.
Bado unaona vigezo vya "kabila/tamaduni" ni 'relevant' kwenye Tanzania ya leo?
 
Jifunze kuvumilia mawazo/mitazamo tofauti na yako/yenu. Ungeweza tu kutoa opinions zako bila makasiriko.
 
Back
Top Bottom