Tundu Lissu: Idadi ya wabunge wa kuchaguliwa iwiane na idadi ya raia wanaowakilisha

Kwa hili nampinga Lissu, uwakilishi ni zaidi ya idadi ya watu. Ukisema tu tuangalie idadi kuna jamii na maeneo yatakosa uwakilishi kabisa.
We nae kichwani una kitu umeongea pumba. Akisema kuangalia anamaanisha ili liwe jimbo la uchaguzi idadi inaanza mfano
1 - 1000
Ikizidi ndipo liongezwe jimbo sasa kuna sehemu ina watu 800 alafu ina majimbo matatu, usikariri huo ni mfano nimekupa. So kwa demokrasi ya usawa anachosema lisu ni sawa tuwe na wabunge kwa idadi ya wapiga kura, kiasi kwamba hata wale wavivu wataamka na kujua umuhimu wa uchaguzi na watapiga kura. Sasa unapinga hoja za msingi kiasi hiki utakuwa unapinga maendeleo kaka. Tukiweka uchama pembeni na kutaka maendeleo tunatakiwa tuwe na nchi huru kidemokrasia tuwe na katiba rafiki ambayo inawabana viongozi kwanzia ngazi ya chini mpaka raisi mwenyewe,
Utofauti kati ya Bunge, Serikali na Mahakama uonekane na kila mhimili ufanye kazi yake kwa uweledi kaka hutosikia ufisadi wala ulaji wa fedha za miradi tutakuwa na nchi safi sana. Na maskini kuwa raisi iwe mwiko.
 
Maana yake majimbo Zanzibar yenye watu 3,000 yafutwe au yaunganishwe na mengine hivyo kuyapunguza idadi yake
 
Kwa formula ya tundulisu Kinondoni Wabunge 10, Temeke 15, Ilala 9, Ubungo 11, na Zanzibar yote wabunge 3. Ingiza Shinyanga na Geita na Mwanza na Mtwara na Tabora na,Dodoma, una jumla ya Wabunge wote itakuwa 900, too big kwa vile Warioba alisema wasizidi 75.

Ili kuendana Warioba cha ni kungeza idadi ya wawakilishwa kupunguza idadi ya Wabunge hadi 75 maximum. Hii itatupa Wabunge 4 Kinondoni 6 Temeke etc etc. SMZ yote haitotosha kuwa na Wabunge wake: itabidi Unguja iwakilishwe na Jimbo la Ilala na Pemba imezwe ndani ya Jimbo la Tanga. Muungano saa hiyo tiyari ushavunjika. Kwa nini Watanzania leo tunataka kuonjeshwa simu? Wenzetu Mbowe na Tundu Lissu watoto wao na wake zao wako Marekani ni raia wa huko.
 
Katiba mpya iondoe wabunge wa viti maalum na wanaoteuliwa bila kuwa na majimbo ya kuwakilisha.
 
Zanzibar oyee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…