Tundu Lissu: Idadi ya wabunge wa kuchaguliwa iwiane na idadi ya raia wanaowakilisha

27 Agosti, 2020
UCHAGUZI OKTOBA 2020, CHADEMA NA CUF ZALALAMIKIA KUENGULIWA KWA MAMIA YA WAGOMBEA WAO

Benson Kigaila

Benson Kigaila
Ona maoni
Vyama kadha vya upinzani nchini Tanzania vimelalamika kwamba mamia ya wagombea wao wameenguliwa katika mchakato wa kuidhinisha ushiriki wao katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.

Vyama hivyo vimetoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushughulikia malalamiko yao ambayo yamewasilishwa rasmi baada ya maafisa katika ngazi za chini kuondoa wagombea wengi wa ubunge na udiwani kutoka vyama vya upinzani kuliko ilivyo kwa wagombea wa chama tawala cha CCM.

Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA nchini humo, Benson Kigaila, amesema hadi kufikia Alhamisi wagombea wao katika nafasi za ubunge katika majimbo 57 na wagombea udiwani 642 wameenguliwa katika mazingira tata.

Kigaila alieleza kisa cha mgombea mmoja aliyeomba fomu ya kukata rufaa na badala yake Mkurugenzi akaondoka na kufunga ofisi huku mgombea akilazimika kusubiri ofisini kutwa nzima bila mkurugenzi kurejea ofisini hapo.

Malalamiko ya aina hiyo yamejirudia katika majimbo mbali mbali ya uchaguzi nchini humo kwa wagombea kutoka vyama vya upinzani.

Kigaila amesema kuwa wamekwishatoa taarifa kwa Tume ya taifa ya Uchaguzi na kutaka uchunguzi ufanywe ili wagombea wao warejeshwe katika ugombea.
Ibrahim Lipumba kiongozi wa chama cha CUF

Nacho chama cha wananchi CUF kupitia kwa Mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Lipumba wao kinasema kimepokea taarifa za wagombea wao kuwekewa pingamizi na baadhi ya maeneo wagombea wao kuporwa fomu za ugombea na watu wasiojulikana.

“kuna watu wamewekewa pingamizi kuna kwingine watu wamevamiwa wamenyang’anywa fomu,” alisema Professa Lipumba.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles, aliithibitishia VOA kwamba wamepokea malalamiko na mapingamizi na kwamba bado wanayafanyia kazi na kusema kuwa katika kipindi cha siku nane watatoa maamuzi.

Source : VOA Swahili
 
1660055216803.png

WILSON MAHERA CHARLES
Rais Magufuli amemteua Dkt Wilson Mahera Charles kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kabla ya uteuzi huo Dkt.Wilson Mahera ......
 
11 August 2022

JOHN HECHE : MCHAKATO WA UCHAGUZI KENYA HAKUNA JANJA JANJA​

John Heche anaangazia uchaguzi wa mkuu wa Kenya 2022 akiulinganisha na ule wa Tanzania 2020.

Mkurugenzi wa Halmashauri DED ambaye ni mtumishi wa serikali ndiye anatumika kuwa mwakilishi wa NEC kuhakiki fomu, kunyima fomu au kukataa kupokea fomu za uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020 badala ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kuajiri wasimamizi wa vituo.

Jimbo la Tarime vijijini nchini Tanzania ni kubwa kuliko baadhi ya kaunti nchini Kenya.

Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020 jimbo kwa jimbo hayaja tangazwa katika tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC hadi leo, nini siri ya NEC kukosa uwazi anahoji John Henche kama siyo nia ovu ya kuchafua uchaguzi ili CCM ishinde.....
Source : mubashara studio
 
Idadi ya watu isiwe kigezo pekee, Chukulia mfano mkoa wa Morogoro ulivyo mkubwa leo uweke uwakilishi kisa tu idadi ya watu huo uwakilishi utawezekana vipi mtu awakilishe kutoka Malinyi hadi Gairo?

Mfano Njombe yenye watu 250K leo ugawe majimbo mawili Mbunge atawakilisha vipi sauti za watu zilizotawanyika?

Hii formula anayopendekeza Lissu inawezekana kwenye developed world sio huku kwetu.
Hoja mfu kwahiyo Tanzania ita remain developing country milele..kwanini tusianze hizo move kuelekea developing country.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa .kanuni anazopendekeza Lisu Zanzibar itakuwa na wabunge 2 tu. Mmoja Pemba na mwingine Unguja
 
Kwa hili nampinga Lissu, uwakilishi ni zaidi ya idadi ya watu. Ukisema tu tuangalie idadi kuna jamii na maeneo yatakosa uwakilishi kabisa.
Unakosaje uwakilishi tumia akili acha kutumia makalio ..fafanua kama unachosema ni kweli kivipi utakosa uwakilishi kwa kutumia kigezo cha wapiga kula wakati lazima utapiga kula kwa mbunge
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media

Kimewashinda Nini kuhamia Kenya?
 
Idadi ya watu isiwe kigezo pekee, Chukulia mfano mkoa wa Morogoro ulivyo mkubwa leo uweke uwakilishi kisa tu idadi ya watu huo uwakilishi utawezekana vipi mtu awakilishe kutoka Malinyi hadi Gairo?

Mfano Njombe yenye watu 250K leo ugawe majimbo mawili Mbunge atawakilisha vipi sauti za watu zilizotawanyika?

Hii formula anayopendekeza Lissu inawezekana kwenye developed world sio huku kwetu.
Kwani muwakilishi anawakilisha nini? Si watu zaidi ndiyo anawawakilisha ...tena kuna madiwani pia ...kwahiyo mkoa mkubwa kama morogoro ukiwa na watu 1000 upatiwe wabunge wengi kisa ukubwa wa mkoa mbunge anawakulisha watu.KIGEZO CHA MSINGI CHA KWANZA NI IDADI YA WATU ...tunacho fanya sasa ni kusafisha kikombe kwa nje na kutokusafisha ndani ya kikombe ....yaani kigezo chenye umuhimu sana tumekiacha na kutumia kigezo kisicho na umuhimu sana.
 
Kwa .kanuni anazopendekeza Lisu Zanzibar itakuwa na wabunge 2 tu. Mmoja Pemba na mwingine Unguja
Wanatosha sana ila aujafafanua wabunge wa bunge gani maana wazenji wana bunge lao pia
 
Idadi ya watu isiwe kigezo pekee, Chukulia mfano mkoa wa Morogoro ulivyo mkubwa leo uweke uwakilishi kisa tu idadi ya watu huo uwakilishi utawezekana vipi mtu awakilishe kutoka Malinyi hadi Gairo?

Mfano Njombe yenye watu 250K leo ugawe majimbo mawili Mbunge atawakilisha vipi sauti za watu zilizotawanyika?

Hii formula anayopendekeza Lissu inawezekana kwenye developed world sio huku kwetu.
Kwani hakuna madiwani? Mbona kuna mkuu wa mkoa mmoja tu Morogoro nzima? Anyway hili suala hata Ndugai amewahi sema haiwezekani idadi ya madarasa Kila Jimbo yalingane maana unakuta demand ni tofauti kulingana na population.

Imagine zanzibar Ina wabunge 50 ila wapiga kura wao ni idadi moja na Jimbo la Temeke na Mbagala!! Sasa jiulize hapo uwiano ukoje maana both geography na population hakuna uwiano.
 
Kama umesoma comment yangu vizuri nimeandika idadi ya watu isiwe kigezo pekee.
 
Unakosaje uwakilishi tumia akili acha kutumia makalio ..fafanua kama unachosema ni kweli kivipi utakosa uwakilishi kwa kutumia kigezo cha wapiga kula wakati lazima utapiga kula kwa mbunge
Hivi kwanini huwa hamna adabu na minakasha? Unataka mawazo yangu na yako au Lissu yafanane?
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media

Jiongrafia ya eneo ndio muhimu sana kuliko idadi ya watu kwa sababu mfano alioutolea ni rahisi kuwafikia hao waliolundikana kwenye eneo dogo kuliko waliotawanyika kwenye eneo kubwa la kijiografia..

Pili akitaka hiyo kanuni pia awe tayari na kanuni ya mgawanyo wa rasilimali kwa kutumia kigezo cha watu na uchangiaji kwenye Pato la Taifa hivyo mkoa wake utakuwa wa mwisho na asilalamike.
 
Haya mengine ni sawa yanahitaji tiba, ila kuhusu mgawanyo wa majimbo kwa kigezo tu cha idadi ya watu si sawa. Wakoloni walitumia factor nyingi ikiwemo kabila, tamaduni na desturi za kieneo, jiografia, njia za mawasiliano ikiwemo kufikika kirahisi n.k n.k
Temeke idadi kubwa lakini panafikika kiurahisi pia na hata namna ya kutambua changamoto ni rahisi pia. Kitu kinachowafanya washindwe kuelewa ni kwamba, kazi ya mbunge ni kuchukua zile changamoto zilizoshindikana katika halmashauri yake na kuzipeleka bungeni kwa ajili ya kufanyiwa kazi na serikali kuu na ndio maana kuna baraza la madiwani ambapo mbunge nae ni mjumbe wa baraza hilo kwa nafasi yake. Yale yaliyo ndani ya uwezo wa halmashauri yanatekelezwa kulingana na vipaumbele vya halmashauri na yanayoshindikana ndio mbunge anayabeba. (shida wabunge wengi wanavipaumbele vyao na ndio maana kuna wakati huwa wanaambiwa warudi kwenye halmashauri zao kujadili)

Bahati mbaya wabunge wengi wanakwenda kivyaovyao na kwa kuwa wanapenda kuchukua ujiko kivyao vyao ndio maana unaona hoja ya idadi ya wabunge iendane na idadi ya watu jimboni wakati tunasahau kuna mamlaka zingine za chini kama madiwani nao ni wawakilishi wa wananchi katika kutatua changamoto.
 
Safi sana mkuu.
 
Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania
Hawa ndio wakujilinganisha na Kenya?
 
Temeke idadi kubwa lakini panafikika kiurahisi pia na hata namna ya kutambua changamoto ni rahisi pia. Kitu kinachowafanya washindwe kuelewa ni kwamba, kazi ya mbunge ni kuchukua zile changamoto zilizoshindikana katika halmashauri yake na kuzipeleka bungeni kwa ajili ya kufanyiwa kazi na serikali kuu na ndio maana kuna baraza la madiwani ambapo mbunge nae ni mjumbe wa baraza hilo kwa nafasi yake.
Kwa wabunge hawahawa wa kupita bila kupingwa?
 
Jiongrafia ya eneo ndio muhimu sana kuliko idadi ya watu kwa sababu mfano alioutolea ni

CCM wanakata mipaka ya kiutawala / maeneobunge (jimbo) kupata wabunge wengi wala hawana mkakati wa maendeleo yoyote.

Soma makala hii :

https://www.standardmedia.co.ke › ...
Maeneo bunge 27 yatakayouliwa na sense - The Standard
Nairobi, Kenya
24 Jul 2019 — Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati. Huenda maeneo bunge zaidi ya 27 nchini yakavunjwa baada ya zoezi la sensa kukamilika .....
Kama mageuzi ya mipaka baada ya sensa ya mwaka huu yatafaulu huenda wanasiasa wengine wakavipoteza viti hivyo na kustaafu siasa. Hata hivyo kuna dhana kwamba idadi ya watu isitumiwe peke yake kama kigezo cha kuvunja maeneo bunge huku wengi wakidai kwamba kuna maeneo bunge yenye watu wachache lakini eneo kubwa mraba hivyo kuwabidi wabunge kwenda mwendo mrefu wakiwahudumia wananchi.

Hata hivyo ni jambo la kukanganya inapodhihirika kwamba kuna maeneo bunge ambayo idadi ya watu inatoshana na kaunti nzima kwenye sehemu zingine nchini. Kwa mfano gavana wa gatuzi la Lamu lenye watu 101, 000 anapata mshahara na marupurupu sawa na gavana wa Kiambu yenye watu milioni 1.6.

Kwa misingi hiyo hiyo, mbunge wa Lamu mashariki yenye watu 20,000 anapata mshahara sawa na mbunge wa Eldoret kaskazini yenye watu zaidi ya 400,000 mara 20 zaidi ile ya Lamu mashariki. Kwa ujumla kuna maeneo bunge 27 ambayo huenda yakavunjiliwa mbali baada ya sensa ya mwaka huu zikiwemo.

Hii ni kwa sababu ingawa katiba mpya imeeleza kwamba maeneo bunge ya taifa yatakuwa 290 tume huru ya uchaguzi na mipaka ya (IEBC) imepewa uhuru wa kugeuza mipaka na kupunguza maeneo bunge mengine na kuongeza kulingana na idadi ya watu itakayotokana na sensa.

Cha msingi kabisa kwenye mageuzi hayo ambayo yamkini yatakuwa na athari kubwa kisiasa na kimaendeleo ni kota ya idadi ya watu kwenye kila eneo bunge ambayo kutokana na sensa ya mnamo mwaka 2009 ni jumla ya watu 133,000.
 
Back
Top Bottom