Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Nimeanza kupata mashaka na hii issue ya Tundu Lissu iweje CHADEMA wako kimya juu ya kuishinikiza serikali kuanzisha uchunguzi huru?..iweje wanaharakati wa tweeter hawaweki pressure kwa serikali ili ukweli ueleweke na haki ipatikane?....Au tunaisubiri serikali yenyewe iamue kufanya uchunguzi?

Nilitegemea mambo mazito yalitoikuta CHADEMA kama watu kupotea, kufa na kushambuliwa wanachama na wapenzi wahamasishwe umma ujue ukweli na hatua zichukuliwe kwa wahusika..Sioni harakati zozote zaidi ya mchezo wa paka na Panya CHADEMA na Serikali....kuna vilivyojificha bila shaka..
Uchuguzi mpaka usubiri CHADEMA na wanaharakati washinikize? polisi siku hizi wanafanya kazi kwa mashinikizo na siyo taratibu na sheria?
 
Mtu anakwambia anafatiliwa wewe unapuuza

Walinzi wanaondolewa kwenye makazi yake alafu anapigwa risasi eneo ilo ilo.

Baada ya tukio CCTV zinaondolewa kwenye eneo la tukio

Badae baadhi ya wema serikalini waungwana wanamshauri Mbowe wampeleke nje

Unazuia makanisa na misikiti wasimuombee

Unapiga marufuku watu wasivae tisheti zake zilizoandikwa pray for lissu.

Ananyimwa pesa ya matibabu bila sababu

Anazuiliwa pesa zake za ubunge

Anavuliwa ubunge kinyume cha sheria

Anarudi kugombea urais anaibiwa kura na anataka kuuwawa tena baadhi ya vigogo serikalini wanamshauri kuondoka nchini!

Huyu mtu utasema hataki uchunguzi wa shambulio lake?

Kwanini uchunguzi usianzie kwenye walioondoa walinzi na CCTV?

Magufuli, Ndungai na Siro mtalipa huu uhuni!!
Mmoja kashalipa bado, Mwigulu, Ndugai, Siro na Makonda
 
'Nilikimbia nchi baada ya kupata taarifa kuwa Rais Magufuli alikuwa ametoa amri kwa 'watu wasiojulikana' kuwa niuawe mara baada ya uchaguzi. Nilikamatiwa na polisi wa IGP Sirro nje ya Ubalozi wa Ujerumani na isingekuwa wanadiplomasia wa Kijerumani kuingilia kati ningepotezwa."-Mh Tundu Lissu
Angekuwa Mwenda zake!
 
Mkuu Lissu hawezi kuwa Rais wa Tz. Usipoteze muda wako. Na wala sio sababu ya Polisi wala Nini. Wananchi nje ya wewe hawawezi kumchagua huyo. Kuongoza nchi sio kufanya debate ya maneno. Sasa wewe kwa akili yako unaweza amini ujinga huo : eti nilipata habari Rais anataka kuniua. For what. It’s too much ujinga mpaka nashangaa.
Moja wapo ni wewe uliyeshiriki hilo tukio
 
..wale wa dodoma hospital walikuwa hawajajipanga.

..wa huku d'salaam wangekuwa wana maelekezo kutoka juu.
Kwaiyo hawezi kumpanga katibu mkuu aliyeteua? Tukio lifanyike Dodoma si alikuwa anajua direct kuwa kuna kituo cha kwanza then chapili na cha tatu?
 
Huyo mwanaharakati aache kugeuza tukio Lake kuwa mtaji wa kisiasa, mtu yoyote akitendewa kinyume na sheria hasa kijinai anajukumu la kutoa taarifa kituo cha polisi cha jirani yake na pia ana jukumu la kutoa ushirikiano wa kutosha kuwezesha upelelezi na kumpata aliyemtendea uhalifu huo.

Pamoja na kuwa alikuwa akijiuguza huko nchi jirani baadae Ulaya lakini baada kupata nafuu hakurudi nyumbani kutoa ushirikiano na polisi lakini akawa anapiga misele kwenye vyombo mbali mbali vya habari akihubili kuhusu kupigwa risasi ili aonewe huruma na aje kugombea uraisi na uchaguzi ulipo karibia alirudi na hakwenda kulipoti polisi akafanya kampeni na baada ya kushindwa uchaguzi alisingizia anatishiwa

bila kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na wala hakusema anatishiwa na nani na kwanini na matokeo yake alikwenda kutunga uwongo kwenye ubalozi wa nchi fulani ya ulaya akasafirishwa kwenda huko alipo na wakati alifanya kampeni takribani miezi mitatu huku akikorofishana na polisi mara nyingi.
Ichunguze akili yako ndugu.
Vipi Kama angekufa au angepata coma
Nani angetoa ushirikiano?
Hivi wengine mioyo ya kibinadamu mlipeleka wapi?.
 
'Nilikimbia nchi baada ya kupata taarifa kuwa Rais Magufuli alikuwa ametoa amri kwa 'watu wasiojulikana' kuwa niuawe mara baada ya uchaguzi. Nilikamatiwa na polisi wa IGP Sirro nje ya Ubalozi wa Ujerumani na isingekuwa wanadiplomasia wa Kijerumani kuingilia kati ningepotezwa."-Mh Tundu Lissu
Huyu mhuni akinywaga pombe za msaada anakurupuka sana kutafuta public sympathy
 
Back
Top Bottom