Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Huyu jamaa anaropoka kila linalokuja kichwani mwake ili mradi aendelee kupata msaada
Akihisi anasahaulika anatoa single nyingine.
Tumemchoka!
 
USA kuandamana ni haki ya msingi, huku unaruhusiwa kuandamana kupongeza ujinga lakini ukiandamana kudai haki unapotezwa mazima.

Sasa unafikiri haki itakuja tu kwa kubembeleza bila watu kuidai...?
 
AKILI za kuambiwa, changanya na za kwako.” - Mh Jakaya Mrisho Kikwete

Jibu ni hiyo signature yako hapo juu. 👆👆👆

Huyu si siku ile ya kuondoka alionekana airport akiwa anatembea kwa madaha, ameweka mikono mfukoni huku akipiga mluzi. Wapambe wake wakiwa wamemzunguka kila upande wake. Kweli mtu aliyekuwa akiwindwa anaweza kuondoka sehemu anayotafutwa kwa udi na uvumba kwa namna ile??
 
Kwa akili za kawaida isingekuwa rahisi kukubali kwamba alipigiwa simu.
 
AKILI za kuambiwa, changanya na za kwako.” - Mh Jakaya Mrisho Kikwete

Jibu ni hiyo signature yako hapo juu. [emoji115][emoji115][emoji115]

Huyu si siku ile ya kuondoka alionekana airport akiwa anatembea kwa madaha, ameweka mikono mfukoni huku akipiga mluzi. Wapambe wake wakiwa wamemzunguka kila upande wake. Kweli mtu aliyekuwa akiwindwa anaweza kuondoka sehemu anayotafutwa kwa udi na uvumba kwa namna ile??
Wewe unafikiri walipanga kumwua kwa uwazi kiasi hicho? Kwa fikra zako, wangeweza kumwulia airport, mahali ambapo tukio lingeonekana kwa watu wengi?

Kwa nini wakati wa shambulio la risasi 16, hawakumshambulia ndani ya ukumbi wa Bunge?

Kuna arguments watu wanafanya, mpaka unajiuliza, aliyeitoa kama ana akili hata ile ya kawaida sana!!
 
IGP Sirro ni mwongo asiyefaa kuvaa sare ya Jeshi la Polisi, let alone kuwa Mkuu wake. For the record:

1) Hajawahi kunipigia simu au kuniita kwenye mahojiano yoyote.

2) Nikiwa Nairobi Hospital niliambiwa polisi watakuja kunihoji hospitalini. Niliwasubiri lakini hawakuonekana.

3) Polisi hawajahoji mtu yeyote wala kutoa taarifa yoyote juu ya uchunguzi wao, zaidi ya kudai wahusika ni watu wasiojulikana na hakuna hata mtu wanayemshuku.

4) Polisi walisema wana footage ya CCTV camera iliyokuwa kwenye jengo nilikoshambuliwa. Hadi leo wako kimya juu ya hilo.

5) Polisi hawajawahi kusema ni nani aliyeondoa walinzi wote kwenye makazi ya viongozi wa serikali ili kuwaruhusu wauaji waingie ndani na kunishambulia kwa risasi.

6) Nilisema hadharani kwamba nilikuwa nafuatiliwa kwa gari na watu waliotumwa na IGP Sirro na Mkuu wa TISS Kipilimba.

Niliwataja IGP Sirro na DG-TISS Kipilimba specifically na kuwataka waingilie kati, na nilitaja gari iliyokuwainanifuata fuata. Majibu yalitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba aliyepuuza taarifa yangu na kudai gari iliyokuwa inanifuata fuata iko Arusha, sio Dar.

Baada ya shambulio, Jeshi la Polisi lilifanya jitihada kubwa kuzuia wananchi kunipa msaada wowote. Waliojaribu kuniombea makanisani na misikitini walipigwa marufuku. Waliojaribu kujitolea damu walikatazwa. Waliovaa Tshirt zenye picha yangu walikamatwa na kuwekwa mahabusu.

7) Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, chini ya Mwenyekiti wake Balozi Adadi Rajabu (DCI mstaafu), ilifanya uchunguzi wa shambulio dhidi yangu na kuandaa taarifa rasmi. Taarifa hiyo ilizimwa na uongozi wa Bunge masaa machache kabla ya kuwasilishwa rasmi bungeni. Kwa nini?

8) Nilinyimwa haki ya kutibiwa kwa fedha za Bunge kama sheria inavyotaka. Baadae Katibu wa Bunge aliniandikia barua kwamba Rais Magufuli hakutoa idhini ya matibabu hayo.

9) Ni Magufuli aliyesema, saa 2 kabla sijashambuliwa, kuwa wanaopinga vita yake ya uchumi hawastahili kuishi!

9) Mwaka jana nilienda Polisi Dodoma kudai gari yangu ambayo iko polisi tangu niliposhambuliwa. Jibu la RPC Muroto lilikuwa sitapewa gari yangu mpaka nitakapohojiwa juu ya shambulio.

Pia soma > IGP Sirro: Kipindi cha kampeni nilimtafuta Tundu Lissu aje kuhojiwa lakini hakuja
 
Ok tumewasikia Sasa mtajuana wenyewe huko maana kila mtu anatetea tumbo lake na mm ngoja nikatetee tumbo langu
 
8) Nilinyimwa haki ya kutibiwa kwa fedha za Bunge kama sheria inavyotaka.

Hapa maneno mazuri yangekuwa fedha za umma maana zinatokana na kodi zetu, tumeambiwa wabunge hawalipi kodi
9) Ni Magufuli aliyesema, saa 2 kabla sijashambuliwa, kuwa wanaopinga vita yake ya uchumi hawastahili kuishi!

9) Mwaka jana nilienda Polisi Dodoma kudai gari yangu ambayo iko polisi tangu niliposhambuliwa. Jibu la RPC Muroto lilikuwa sitapewa gari yangu mpaka nitakapohojiwa juu ya shambulio.
Maneno mazito haya!!! Tanzania!!!
 
Wewe unafikiri walipanga kumwua kwa uwazi kiasi hicho? Kwa fikra zako, wangeweza kumwulia airport, mahali ambapo tukio lingeonekana kwa watu wengi?..
Kama wale wanaosema mbona aliachwa akafanya kampeni za urais, hivi unawezaje kumuua mgombea mwenza wa upinzani, si dunia nzima itakua na taharuki tena baada ya mgombea kupona jaribio la kwanza la kuuwawa!
 
Use ni kulinda legacy kwa mtutu wa bunduki
legacy hailindwi wala haitafutwi inajionyesha yenyewe yaani mnapata tabu sana na legacy ya jpm ambayo ipo automatically mtasema mtamtukana mtaongea lakini ameshaacha alama ambayo hakuna pimbi yoyote chadema anaweza kufanya
 
Kama wale wanaosema mbona aliachwa akafanya kampeni za urais, hivi unawezaje kumuua mgombea mwenza wa upinzani, si dunia nzima itakua na taharuki tena baada ya mgombea kupona jaribio la kwanza la kuuwawa!
nani alitaka kumuua huyo pimbi wenu? hakuwa na nguvu yoyote ya kuipa wasiwasi nchi hii alikuwa anaogopa kivuli chake tu anakimbia hov=yo
 
Back
Top Bottom