Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Umesoma vizuri maelezo ya Lissu? Pale kwa kamanda Mroto Dodoma, eneo ambalo pia ndio alikopigwa risasi sio police pale??? Ilishindikana nini kumuhoji mtu ambaye kajileta mwenyewe? Nadhani kuna mengine hata kama tunataka kutetea basi tukae kimya tu, ni aibu sana kwa mtu mzima kudanganya; jamani, kuna Mungu pia, tukumbuke hilo. Yuko wapi aliyeagiza jamaa asipewe pesa za matibabu? Yuko wapi mtu aliye agiza jamaa anyang'anywe ubunge? Yuko wapi.....!? Tumuogope Mungu, maisha tumepewa kama rehani tu, mwenyewe anaweza kuyataka muda wowote, tuache KIBURI.
unajuwa mnapobishania mambo ya kijinga kama haya msimuhusishe Mungu mnamchosha hivi yeye alikuwa au huwaga anasubiri aitwe kuhojiwa? hivi alipokuja kufanya kampeni si alitakiwa aende kituo cha polisi akafungue jalada au akaripoti kushambuliwa kwake? ili sasa polisi wafanye mahojiano na yeye? sasa polisi wanaweza kuwa na kazi ya kumtafuta kila mtu aliyefanyiwa tukio ili wamuoji inawezekana? au yeye ni spesho sana kuliko wananchi wengine?
 
MAJIBU YA MHESHIMIWA TUNDU LISSU KWA IGP SIMON SIRO, KUHUSIANA NA SHAMBULIO LAKE LA TAREHE 7/9/2017

IGP Sirro ni mwongo asiyefaa kuvaa sare ya Jeshi la Polisi, let alone kuwa Mkuu wake. For the record:

1) Hajawahi kunipigia simu au kuniita kwenye mahojiano yoyote.

2) Nikiwa Nairobi Hospital niliambiwa polisi watakuja kunihoji hospitalini. Niliwasubiri lakini hawakuonekana.

3) Polisi hawajahoji mtu yeyote wala kutoa taarifa yoyote juu ya uchunguzi wao, zaidi ya kudai wahusika ni watu wasiojulikana na hakuna hata mtu wanayemshuku.

4) Polisi walisema wana footage ya CCTV camera iliyokuwa kwenye jengo nilikoshambuliwa. Hadi leo wako kimya juu ya hilo.

5) Polisi hawajawahi kusema ni nani aliyeondoa walinzi wote kwenye makazi ya viongozi wa serikali ili kuwaruhusu wauaji waingie ndani na kunishambulia kwa risasi.

6) Nilisema hadharani kwamba nilikuwa nafuatiliwa kwa gari na watu waliotumwa na IGP Sirro na Mkuu wa TISS Kipilimba. Niliwataja IGP Sirro na DG-TISS Kipilimba specifically na kuwataka waingilie kati, na nilitaja gari iliyokuwainanifuata fuata. Majibu yalitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba aliyepuuza taarifa yangu na kudai gari iliyokuwa inanifuata fuata iko Arusha, sio Dar. Baada ya shambulio, Jeshi la Polisi lilifanya jitihada kubwa kuzuia wananchi kunipa msaada wowote. Waliojaribu kuniombea makanisani na misikitini walipigwa marufuku. Waliojaribu kujitolea damu walikatazwa. Waliovaa Tshirt zenye picha yangu walikamatwa na kuwekwa mahabusu.

7) Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, chini ya Mwenyekiti wake Balozi Adadi Rajabu (DCI mstaafu), ilifanya uchunguzi wa shambulio dhidi yangu na kuandaa taarifa rasmi. Taarifa hiyo ilizimwa na uongozi wa Bunge masaa machache kabla ya kuwasilishwa rasmi bungeni. Kwa nini?

8) Nilinyimwa haki ya kutibiwa kwa fedha za Bunge kama sheria inavyotaka. Baadae Katibu wa Bunge aliniandikia barua kwamba Rais Magufuli hakutoa idhini ya matibabu hayo.

9) Ni Magufuli aliyesema, saa 2 kabla sijashambuliwa, kuwa wanaopinga vita yake ya uchumi hawastahili kuishi! Mwaka jana nilienda Polisi Dodoma kudai gari yangu ambayo iko polisi tangu niliposhambuliwa. Jibu la RPC Muroto lilikuwa sitapewa gari yangu mpaka nitakapohojiwa juu ya shambulio. Lakini polisi hawakuwa na interest ya kunihoji zaidi ya kupiga mabomu mikutano yangu ya hadhara.

10) Nilikimbia nchi baada ya kupata taarifa kuwa Rais Magufuli alikuwa ametoa amri kwa 'watu wasiojulikana' kuwa niuawe mara baada ya uchaguzi. Nilikamatiwa na polisi wa IGP Sirro nje ya Ubalozi wa Ujerumani na isingekuwa wanadiplomasia wa Kijerumani kuingilia kati ningepotezwa. IGP Sirro anasema sistahili kupewa ulinzi wowote kwa sababu mimi ni Mtanzania sawa na Watanzania wengine. Lakini sio Watanzania wote waliowahi kushambuliwa kwa risasi 16 wala kutendewa kama nilivyotendewa mimi. Majibu yake ni utetezi wa wauaji wasiojulikana na wale waliowatuma! Tundu A. Lissu Belgium
 
Ungepotezwa mana lisasi wewe nindogo kwako hazikuwezi

Siro ajirekebishe apunguze ubambikizaji kesi ,tundu lisu hakufa anaongea uongo au
Siro hatambui lisu hakufa nimzima inawezekana lisu anayefahamika najeshi lapolisi alishakufa ,huyu aliyepigwa mvua za lisasi ni mwingine

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Si Wanyamaze tu Mbona Swala la Tundu Lissu Ni kama Lipo Wazi. Mungu ameshaingilia Kati, Lissu Kapona japo amekuwa na Ulemavu lakini kwa watesi wake Mungu Kama Kawaida yake Hukumu yake Haina Makosa; So tusamehane na Maisha Yaendelee.
 
..Igp alisema polisi hawakuwa na taarifa kuhusu Lissu kufuatiliwa na gari ya watu wasioeleweka.

..waziri wa mambo ya ndani alisema wamechunguza na kubaini namba za gari iliyokuwa ikimfuatilia Lissu ni za gari iliyoko Arusha ambayo haijawahi kufika Dsalaam.

..kati ya Igp na Waziri wa Mambo ya ndani yupi anasema ukweli?
 
Tukio la Lissu sio lakuchukulia kisiasa wala kishabiki.
Kuna watu wengi tu wa Imani na itikadi tofauti walimchangia kwa siri.
Huko walikoendelea wanakosolewa lakini hawafiki unyamaa ule wa Lissu.
Pia machafuko huanzia kwenye Dini na Siasa.Tujifunze kupitia Haiti,tabia zilifanana na awamu 5
 
MAJIBU YA MHESHIMIWA TUNDU LISSU KWA IGP SIMON SIRO, KUHUSIANA NA SHAMBULIO LAKE LA TAREHE 7/9/2017

IGP Sirro ni mwongo asiyefaa kuvaa sare ya Jeshi la Polisi, let alone kuwa Mkuu wake. For the record:

1) Hajawahi kunipigia simu au kuniita kwenye mahojiano yoyote.

2) Nikiwa Nairobi Hospital niliambiwa polisi watakuja kunihoji hospitalini. Niliwasubiri lakini hawakuonekana.

3) Polisi hawajahoji mtu yeyote wala kutoa taarifa yoyote juu ya uchunguzi wao, zaidi ya kudai wahusika ni watu wasiojulikana na hakuna hata mtu wanayemshuku.

4) Polisi walisema wana footage ya CCTV camera iliyokuwa kwenye jengo nilikoshambuliwa. Hadi leo wako kimya juu ya hilo.

5) Polisi hawajawahi kusema ni nani aliyeondoa walinzi wote kwenye makazi ya viongozi wa serikali ili kuwaruhusu wauaji waingie ndani na kunishambulia kwa risasi.

6) Nilisema hadharani kwamba nilikuwa nafuatiliwa kwa gari na watu waliotumwa na IGP Sirro na Mkuu wa TISS Kipilimba. Niliwataja IGP Sirro na DG-TISS Kipilimba specifically na kuwataka waingilie kati, na nilitaja gari iliyokuwainanifuata fuata. Majibu yalitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba aliyepuuza taarifa yangu na kudai gari iliyokuwa inanifuata fuata iko Arusha, sio Dar. Baada ya shambulio, Jeshi la Polisi lilifanya jitihada kubwa kuzuia wananchi kunipa msaada wowote. Waliojaribu kuniombea makanisani na misikitini walipigwa marufuku. Waliojaribu kujitolea damu walikatazwa. Waliovaa Tshirt zenye picha yangu walikamatwa na kuwekwa mahabusu.

7) Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, chini ya Mwenyekiti wake Balozi Adadi Rajabu (DCI mstaafu), ilifanya uchunguzi wa shambulio dhidi yangu na kuandaa taarifa rasmi. Taarifa hiyo ilizimwa na uongozi wa Bunge masaa machache kabla ya kuwasilishwa rasmi bungeni. Kwa nini?

8) Nilinyimwa haki ya kutibiwa kwa fedha za Bunge kama sheria inavyotaka. Baadae Katibu wa Bunge aliniandikia barua kwamba Rais Magufuli hakutoa idhini ya matibabu hayo.

9) Ni Magufuli aliyesema, saa 2 kabla sijashambuliwa, kuwa wanaopinga vita yake ya uchumi hawastahili kuishi! Mwaka jana nilienda Polisi Dodoma kudai gari yangu ambayo iko polisi tangu niliposhambuliwa. Jibu la RPC Muroto lilikuwa sitapewa gari yangu mpaka nitakapohojiwa juu ya shambulio. Lakini polisi hawakuwa na interest ya kunihoji zaidi ya kupiga mabomu mikutano yangu ya hadhara.

10) Nilikimbia nchi baada ya kupata taarifa kuwa Rais Magufuli alikuwa ametoa amri kwa 'watu wasiojulikana' kuwa niuawe mara baada ya uchaguzi. Nilikamatiwa na polisi wa IGP Sirro nje ya Ubalozi wa Ujerumani na isingekuwa wanadiplomasia wa Kijerumani kuingilia kati ningepotezwa. IGP Sirro anasema sistahili kupewa ulinzi wowote kwa sababu mimi ni Mtanzania sawa na Watanzania wengine. Lakini sio Watanzania wote waliowahi kushambuliwa kwa risasi 16 wala kutendewa kama nilivyotendewa mimi. Majibu yake ni utetezi wa wauaji wasiojulikana na wale waliowatuma! Tundu A. Lissu Belgium
Instagram media - Bt2Krycj3b7.jpg
 
Nakumbuka Lisu akiwa KIA alisema atarusha chopa yake hadi Dar hata kama hajapewa kibali maana haogopi chochote, na anaetaka kufanya kitu afanye yeye yupo tayari!

Kwa ujasiri huu wa Lisu hadi aka risk maisha yake kwa kurusha chopa toka KIA hadi Dar bila kibali alafu akaogopa kitisho cha kwenye simu?

Ok. Mbaya wa Lisu alishafariki inakuwaje sasa anaendelea kung'ang'ania kwa amsterdam?
 
10) Nilikimbia nchi baada ya kupata taarifa kuwa Rais Magufuli alikuwa ametoa amri kwa 'watu wasiojulikana' kuwa niuawe mara baada ya uchaguzi. Nilikamatiwa na polisi wa IGP Sirro nje ya Ubalozi wa Ujerumani na isingekuwa wanadiplomasia wa Kijerumani kuingilia kati ningepotezwa. IGP Sirro anasema sistahili kupewa ulinzi wowote kwa sababu mimi ni Mtanzania sawa na Watanzania wengine. Lakini sio Watanzania wote waliowahi kushambuliwa kwa risasi 16 wala kutendewa kama nilivyotendewa mimi. Majibu yake ni utetezi wa wauaji wasiojulikana na wale waliowatuma! Tundu A. Lissu Belgium
Hatari kubwa hii hapa iliyokuwa inamkabili Lissu watu wengi hawakuiwekea maanani kwa kutoelewa tu kilichokuwa kikitokea wakati huo, kwa hiyo wengi hawaoni uzito wake ulivyo.
Watu hawawaelewi maana ya Lissu akisindikizwa na Balozi hadi kupanda ndege maana yake ni nini!

Hatari inayoendelea kumkabiri Lissu, ni kwamba, pamoja na kutoweka kwa mhusika mkuu, hawa waliokuwa watekelezaji wa maagizo nao sasa hivi wanaendelea kuona hatari juu yao kutokana na Lissu kuwa hai. Lissu mfu ni bora zaidi kwao kuliko aliye hai.
 
Lisu ni debe tupu!

Alisema haogopi chochote na yupo tayari kurusha chopa yake toka KIA to Dar bila kibali!
.
Huyu ikawaje akaogopa kitisho cha kwenye simu?
 
Tundu aje hiki yaishe

Mbona alikuja kwenye kampeni!?

Au hataki hitimisho!?

..Lissu ameomba ulinzi kama wakati wa kampeni ili aweze kurudi nchini.

..serikali imewahi kutoa ulinzi maalum kwa raia ambao walikuwa wametishiwa maisha yao.

..kama haiwezekani kumpa Lissu ulinzi, basi serikali ishirikiane na Interpol na polisi wa Ubelgiji kumhoji Lissu ili suala hili lifikie tamati.
 
Tundu amekutana na akili kubwa Tanzania
Wale aliodhani ni wajinga na wasiojua kiingereza wamemwambia ulinzi na usalama ni wajibu wa serikali kwa kila raia.
Yeye anataka ulinzi binafsi sasa alishawahi jiuliza wangapi wamepitia magumu kama yeye na wako salama nchini? Je aliambiwa walipewa ulinzi binafsi!?
 
Back
Top Bottom