Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Tundu amekutana na akili kubwa Tanzania
Wale aliodhani ni wajinga na wasiojua kiingereza wamemwambia ulinzi na usalama ni wajibu wa serikali kwa kila raia.
Yeye anataka ulinzi binafsi sasa alishawahi jiuliza wangapi wamepitia magumu kama yeye na wako salama nchini? Je aliambiwa walipewa ulinzi binafsi!?

..wako raia ambao walitishiwa, hawakushambuliwa kama Lissu, lakini serikali iliwapa ulinzi.

..tutangulize ubinadamu. Tusichukue maamuzi kwa nia ya kumkomoa mtu.
 
Nimeanza kupata mashaka na hii issue ya Tundu Lissu iweje CHADEMA wako kimya juu ya kuishinikiza serikali kuanzisha uchunguzi huru?..iweje wanaharakati wa tweeter hawaweki pressure kwa serikali ili ukweli ueleweke na haki ipatikane?....Au tunaisubiri serikali yenyewe iamue kufanya uchunguzi?

Nilitegemea mambo mazito yalitoikuta CHADEMA kama watu kupotea, kufa na kushambuliwa wanachama na wapenzi wahamasishwe umma ujue ukweli na hatua zichukuliwe kwa wahusika..Sioni harakati zozote zaidi ya mchezo wa paka na Panya CHADEMA na Serikali....kuna vilivyojificha bila shaka..
Hujitambui
 
Mwanasiasa machachari wa Tanzania anayeishi mamtoni baaada ya kufanyiwa unyama amekanusha taarifa na kauli ya Igp Sirro kuwa alipigiwa simu na jeshi la polisi ili ahojiwe juu ya madhila yaliyompata....
Kwa haya majibu hii inaitwa Niguse ninuke😅😅
 
Hujawahi kuona IGP at all. Mie ningekuwa wewe ningejiukiza maswali kadhaa. Mosi, tundu alienda lunch, kawaida, kama siku zote. Iweje wauaji siku hiyo wajue kuwa CCTV inezimwa au walinzi hawapo?..
Mkuu
Ni nani aliekudanganya kua siku hio cctv camera zilikua zimezima?

E6FWKIkXEAAi1Oc.jpeg
 
Tundu amekutana na akili kubwa Tanzania
Wale aliodhani ni wajinga na wasiojua kiingereza wamemwambia ulinzi na usalama ni wajibu wa serikali kwa kila raia.
Yeye anataka ulinzi binafsi sasa alishawahi jiuliza wangapi wamepitia magumu kama yeye na wako salama nchini? Je aliambiwa walipewa ulinzi binafsi!?
Hebu tutajie waliopitia magumu kama yeye bado wapo nchini walau mmoja tu
 
Hebu tutajie waliopitia magumu kama yeye bado wapo nchini walau mmoja tu
Wapo waliouwawa kwa risasi na wapo walichomwa moto na kuzikwa kabisa
Huwa hupitii habari? Au hao wao sio watanzania?
 
IGP alivuka hadhi ya nafasi yake. Angeishia kusema alimpigia Lissu simu hakwenda wenye akili wangemwelewa lakini alipoongeza kwamba Lissu anafurahia/anatumia hali aliyonayo kujipatia fedha, hata wasio na akili wakaona IGP ni ndugu yao.
Nilisikiliza majibu yake nikapa shaka. Alimnanga badala kuzungumza kitaaluma.
 
Sawa Mimi kenge..Ila urudi shule kwanza ukajifunze kuandika Kwanza kisha uje tubishane Kwa oja..'fara' ndiyo nini?

Ila sishangai,vitoto vitukutu ndy kawaida yenu mkishaanza kujifunza kuandika cha Kwanza mnajifunza kuandika matusi ukutani..naona Jf umefanya ndy ukuta wako[emoji1787]
Fara ndiyo jina lako wewe mbwa koko usije kulishangaa tena
 
Wapo waliouwawa kwa risasi na wapo walichomwa moto na kuzikwa kabisa
Huwa hupitii habari? Au hao wao sio watanzania?
Hata Siro nilimshangaa kama ninavyokushangaa wewe!

Alisema Lissu ni mwanasiasa maarufu, lakini kwa upande mwingine akimlinganisha na wananchi wengine wa kawaida pale alipoulizwa kuhusu umuhimu wa ulinzi wake.
 
Lisu ni debe tupu!

Alisema haogopi chochote na yupo tayari kurusha chopa yake toka KIA to Dar bila kibali!
.
Huyu ikawaje akaogopa kitisho cha kwenye simu?
Debe tupu lililochukua shaba 16, na kubaki limesimama!
 
Mwanasiasa machachari wa Tanzania anayeishi mamtoni baaada ya kufanyiwa unyama amekanusha taarifa na kauli ya Igp Sirro kuwa alipigiwa simu na jeshi la polisi ili ahojiwe juu ya madhila yaliyompata.


Kupitia ukurasa wake wa Twita Lissu amedai kuwa taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote.

Soma >IGP Sirro: Kipindi cha kampeni nilimtafuta Tundu Lissu aje kuhojiwa lakini hakuja
====

IGP Sirro ni mwongo asiyefaa kuvaa sare ya Jeshi la Polisi, let alone kuwa Mkuu wake. For the record:

1) Hajawahi kunipigia simu au kuniita kwenye mahojiano yoyote.

2) Nikiwa Nairobi Hospital niliambiwa polisi watakuja kunihoji hospitalini. Niliwasubiri lakini hawakuonekana.

3) Polisi hawajahoji mtu yeyote wala kutoa taarifa yoyote juu ya uchunguzi wao, zaidi ya kudai wahusika ni watu wasiojulikana na hakuna hata mtu wanayemshuku.

4) Polisi walisema wana footage ya CCTV camera iliyokuwa kwenye jengo nilikoshambuliwa. Hadi leo wako kimya juu ya hilo.

5) Polisi hawajawahi kusema ni nani aliyeondoa walinzi wote kwenye makazi ya viongozi wa serikali ili kuwaruhusu wauaji waingie ndani na kunishambulia kwa risasi.

6) Nilisema hadharani kwamba nilikuwa nafuatiliwa kwa gari na watu waliotumwa na IGP Sirro na Mkuu wa TISS Kipilimba.

Niliwataja IGP Sirro na DG-TISS Kipilimba specifically na kuwataka waingilie kati, na nilitaja gari iliyokuwainanifuata fuata. Majibu yalitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba aliyepuuza taarifa yangu na kudai gari iliyokuwa inanifuata fuata iko Arusha, sio Dar.

Baada ya shambulio, Jeshi la Polisi lilifanya jitihada kubwa kuzuia wananchi kunipa msaada wowote. Waliojaribu kuniombea makanisani na misikitini walipigwa marufuku. Waliojaribu kujitolea damu walikatazwa. Waliovaa Tshirt zenye picha yangu walikamatwa na kuwekwa mahabusu.

6) Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, chini ya Mwenyekiti wake Balozi Adadi Rajabu (DCI mstaafu), ilifanya uchunguzi wa shambulio dhidi yangu na kuandaa taarifa rasmi. Taarifa hiyo ilizimwa na uongozi wa Bunge masaa machache kabla ya kuwasilishwa rasmi bungeni. Kwa nini?

7) Nilinyimwa haki ya kutibiwa kwa fedha za Bunge kama sheria inavyotaka. Baadae Katibu wa Bunge aliniandikia barua kwamba Rais Magufuli hakutoa idhini ya matibabu hayo.

8) Ni Magufuli aliyesema, saa 2 kabla sijashambuliwa, kuwa wanaopinga vita yake ya uchumi hawastahili kuishi!

9) Mwaka jana nilienda Polisi Dodoma kudai gari yangu ambayo iko polisi tangu niliposhambuliwa. Jibu la RPC Muroto lilikuwa sitapewa gari yangu mpaka nitakapohojiwa juu ya shambulio. Lakini polisi hawakuwa na interest ya kunihoji zaidi ya kupiga mabomu mikutano yangu ya hadhara.

10) Nilikimbia nchi baada ya kupata taarifa kuwa Rais Magufuli alikuwa ametoa amri kwa 'watu wasiojulikana' kuwa niuawe mara baada ya uchaguzi. Nilikamatiwa na polisi wa IGP Sirro nje ya Ubalozi wa Ujerumani na isingekuwa wanadiplomasia wa Kijerumani kuingilia kati ningepotezwa.

IGP Sirro anasema sistahili kupewa ulinzi wowote kwa sababu mimi ni Mtanzania sawa na Watanzania wengine. Lakini sio Watanzania wote waliowahi kushambuliwa kwa risasi 16 wala kutendewa kama nilivyotendewa mimi. Majibu yake ni utetezi wa wauaji wasiojulikana na wale waliowatuma!
View attachment 1849851
Viongozi WETU , lazima kujua tz ya Sasa sio ile ya mwalim , wengine tumezeeka ,tuna wajukuu, ipo siku wajukuu watatuuliza maswali tutashindwa wajibu , let be smart ,KAZI zapita tu ,
 
Back
Top Bottom