Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji, Waliagizwa wanipoteze baada ya Uchaguzi

Mwanasiasa machachari wa Tanzania anayeishi mamtoni baaada ya kufanyiwa unyama amekanusha taarifa na kauli ya Igp Sirro kuwa alipigiwa simu na jeshi la polisi ili ahojiwe juu ya madhila yaliyompata.

Kupitia ukurasa wake wa Twita Lissu amedai kuwa taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote.

Soma >IGP Sirro: Kipindi cha kampeni nilimtafuta Tundu Lissu aje kuhojiwa lakini hakuja
====

IGP Sirro ni mwongo asiyefaa kuvaa sare ya Jeshi la Polisi, let alone kuwa Mkuu wake. For the record:

1) Hajawahi kunipigia simu au kuniita kwenye mahojiano yoyote.

2) Nikiwa Nairobi Hospital niliambiwa polisi watakuja kunihoji hospitalini. Niliwasubiri lakini hawakuonekana.

3) Polisi hawajahoji mtu yeyote wala kutoa taarifa yoyote juu ya uchunguzi wao, zaidi ya kudai wahusika ni watu wasiojulikana na hakuna hata mtu wanayemshuku.

4) Polisi walisema wana footage ya CCTV camera iliyokuwa kwenye jengo nilikoshambuliwa. Hadi leo wako kimya juu ya hilo.

5) Polisi hawajawahi kusema ni nani aliyeondoa walinzi wote kwenye makazi ya viongozi wa serikali ili kuwaruhusu wauaji waingie ndani na kunishambulia kwa risasi.

6) Nilisema hadharani kwamba nilikuwa nafuatiliwa kwa gari na watu waliotumwa na IGP Sirro na Mkuu wa TISS Kipilimba.

Niliwataja IGP Sirro na DG-TISS Kipilimba specifically na kuwataka waingilie kati, na nilitaja gari iliyokuwainanifuata fuata. Majibu yalitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba aliyepuuza taarifa yangu na kudai gari iliyokuwa inanifuata fuata iko Arusha, sio Dar.

Baada ya shambulio, Jeshi la Polisi lilifanya jitihada kubwa kuzuia wananchi kunipa msaada wowote. Waliojaribu kuniombea makanisani na misikitini walipigwa marufuku. Waliojaribu kujitolea damu walikatazwa. Waliovaa Tshirt zenye picha yangu walikamatwa na kuwekwa mahabusu.

6) Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, chini ya Mwenyekiti wake Balozi Adadi Rajabu (DCI mstaafu), ilifanya uchunguzi wa shambulio dhidi yangu na kuandaa taarifa rasmi. Taarifa hiyo ilizimwa na uongozi wa Bunge masaa machache kabla ya kuwasilishwa rasmi bungeni. Kwa nini?

7) Nilinyimwa haki ya kutibiwa kwa fedha za Bunge kama sheria inavyotaka. Baadae Katibu wa Bunge aliniandikia barua kwamba Rais Magufuli hakutoa idhini ya matibabu hayo.

8) Ni Magufuli aliyesema, saa 2 kabla sijashambuliwa, kuwa wanaopinga vita yake ya uchumi hawastahili kuishi!

9) Mwaka jana nilienda Polisi Dodoma kudai gari yangu ambayo iko polisi tangu niliposhambuliwa. Jibu la RPC Muroto lilikuwa sitapewa gari yangu mpaka nitakapohojiwa juu ya shambulio. Lakini polisi hawakuwa na interest ya kunihoji zaidi ya kupiga mabomu mikutano yangu ya hadhara.

10) Nilikimbia nchi baada ya kupata taarifa kuwa Rais Magufuli alikuwa ametoa amri kwa 'watu wasiojulikana' kuwa niuawe mara baada ya uchaguzi. Nilikamatiwa na polisi wa IGP Sirro nje ya Ubalozi wa Ujerumani na isingekuwa wanadiplomasia wa Kijerumani kuingilia kati ningepotezwa.

IGP Sirro anasema sistahili kupewa ulinzi wowote kwa sababu mimi ni Mtanzania sawa na Watanzania wengine. Lakini sio Watanzania wote waliowahi kushambuliwa kwa risasi 16 wala kutendewa kama nilivyotendewa mimi. Majibu yake ni utetezi wa wauaji wasiojulikana na wale waliowatuma!
View attachment 1849851
 
Attachments

  • twitter_20220120_101600.mp4
    77.2 KB
Nimesoma comments zote nilichokiona ni:-

1. Sirro tumuweke mbele za mungu afe ili Tundu lissu arudi nyumbani. Uwepo was Sirro ni kikwazo Kwa watanzania, amwagiwe maji ya upako afe

Naimani atakufa mwaka huu hamalizi 2022

2. Walitumwa kumuua lissu wanajulikana kisasi kinaweza lipwa individually

3. Kule police wajulikane waliokuwa wamejivika kumpigania dictator uchwala magu

Haya mambo ni makubwa lakini tutashinda
 
Sijui kwa nini, lakini baada ya kushindwa kumwua TL, nilikuwa naona Mag angetangulia kufariki kabla ya TL. Ilistahili TL ashuhudie kifo cha aliyetaka kumwua. Na yote, ni ili ukuu na utukufu wa Mungu upate kushuhudiwa na wengi waliojaliwa macho ya kiroho.

Marehemu amemaliza safari yake, lakini kubwa zaidi ni kwa tuliobakia nyuma, kujiuliza kama kuna kitu chochote tulichojifunza katika dhamira zetu.

Uweza wa Mungu ni mkuu, tuishi kwa kuhofu kutenda kinyume na maagizo yake. Tunaweza kuwa dhaifu na wadhambi, lakini tusikufuru na kujiona ni wenye uweza kama wake hata wa kuamua nani aishi na nani asiishi, nani afurahie na nani ateseke, nani apendelewe na nani aonewe.

"Mungu wetu kwa maisha ya huyu mwenzetu uliyemwita kwako, imekuwa ni injili inayoishi. Injili hii iyaguse maisha yangu, japo mimi siyo Rais, lakini kwa nafasi yangu natambua nina wajibu wa kutenda haki, wajibu wa kuwasaidia wenzangu wapate haki uliyoitoa wewe mwenyewe, haki ya kuishi, wapate maisha ya furaha, wapate kilicho haki yao, maana najua ni katika wao, uMungu wako unaishi, na katika mema ninayowatendea wenzangu ikawe sababu ya kupata msamaha wangu pale nitakapopungukiwa, siku utakaponiita kwako. Tunaomba uwape faraja ya pekee wale ambao ndugu zao waliuawa, ndugu zao walipotezwa, ndugu zao walitekwa.

Faraja yao inaweza kupatikana kutoka kwako tu, na wala siyo kutoka kwa mwanadamu yeyote maana majonzi yao hayapimiki wala kuhesabika. Wayapokee yaliyotokea kama sadaka yao kwaajili ya uovu wa Ulimwengu. Naomba wakati wote unijalie moyo wa kuyaona maovu yangu kabla ya kuyaona ya wengine"

Ni upendo gani unaozidi ule wa mtu kuyatoa maisha yake kwaajili ya rafiki zake? Maneno haya yadumu moyoni mwangu na kwa yeyote anayetaka kuuona ukuu wako.
Amen [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Anatoa macho yake kama kabudi
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
IMG_20210824_182457.jpg
 
Risasi zilipigwa upande wa kushoto zikaumiza upande wa kulia,hii ni zaidi ya sanaaa

..wewe utakuwa mjinga sana.

..jambo rahisi namna hiyo you can not figure out?

..halafu inawezekana wewe ni polisi uko idara ya uchunguzi lakini uelewa wako ni mdogo namna hii.
 
Mwanasiasa machachari wa Tanzania anayeishi mamtoni baaada ya kufanyiwa unyama amekanusha taarifa na kauli ya Igp Sirro kuwa alipigiwa simu na jeshi la polisi ili ahojiwe juu ya madhila yaliyompata.

Kupitia ukurasa wake wa Twita Lissu amedai kuwa taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote.

Soma >IGP Sirro: Kipindi cha kampeni nilimtafuta Tundu Lissu aje kuhojiwa lakini hakuja
====

IGP Sirro ni mwongo asiyefaa kuvaa sare ya Jeshi la Polisi, let alone kuwa Mkuu wake. For the record:

1) Hajawahi kunipigia simu au kuniita kwenye mahojiano yoyote.

2) Nikiwa Nairobi Hospital niliambiwa polisi watakuja kunihoji hospitalini. Niliwasubiri lakini hawakuonekana.

3) Polisi hawajahoji mtu yeyote wala kutoa taarifa yoyote juu ya uchunguzi wao, zaidi ya kudai wahusika ni watu wasiojulikana na hakuna hata mtu wanayemshuku.

4) Polisi walisema wana footage ya CCTV camera iliyokuwa kwenye jengo nilikoshambuliwa. Hadi leo wako kimya juu ya hilo.

5) Polisi hawajawahi kusema ni nani aliyeondoa walinzi wote kwenye makazi ya viongozi wa serikali ili kuwaruhusu wauaji waingie ndani na kunishambulia kwa risasi.

6) Nilisema hadharani kwamba nilikuwa nafuatiliwa kwa gari na watu waliotumwa na IGP Sirro na Mkuu wa TISS Kipilimba.

Niliwataja IGP Sirro na DG-TISS Kipilimba specifically na kuwataka waingilie kati, na nilitaja gari iliyokuwainanifuata fuata. Majibu yalitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba aliyepuuza taarifa yangu na kudai gari iliyokuwa inanifuata fuata iko Arusha, sio Dar.

Baada ya shambulio, Jeshi la Polisi lilifanya jitihada kubwa kuzuia wananchi kunipa msaada wowote. Waliojaribu kuniombea makanisani na misikitini walipigwa marufuku. Waliojaribu kujitolea damu walikatazwa. Waliovaa Tshirt zenye picha yangu walikamatwa na kuwekwa mahabusu.

6) Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, chini ya Mwenyekiti wake Balozi Adadi Rajabu (DCI mstaafu), ilifanya uchunguzi wa shambulio dhidi yangu na kuandaa taarifa rasmi. Taarifa hiyo ilizimwa na uongozi wa Bunge masaa machache kabla ya kuwasilishwa rasmi bungeni. Kwa nini?

7) Nilinyimwa haki ya kutibiwa kwa fedha za Bunge kama sheria inavyotaka. Baadae Katibu wa Bunge aliniandikia barua kwamba Rais Magufuli hakutoa idhini ya matibabu hayo.

8) Ni Magufuli aliyesema, saa 2 kabla sijashambuliwa, kuwa wanaopinga vita yake ya uchumi hawastahili kuishi!

9) Mwaka jana nilienda Polisi Dodoma kudai gari yangu ambayo iko polisi tangu niliposhambuliwa. Jibu la RPC Muroto lilikuwa sitapewa gari yangu mpaka nitakapohojiwa juu ya shambulio. Lakini polisi hawakuwa na interest ya kunihoji zaidi ya kupiga mabomu mikutano yangu ya hadhara.

10) Nilikimbia nchi baada ya kupata taarifa kuwa Rais Magufuli alikuwa ametoa amri kwa 'watu wasiojulikana' kuwa niuawe mara baada ya uchaguzi. Nilikamatiwa na polisi wa IGP Sirro nje ya Ubalozi wa Ujerumani na isingekuwa wanadiplomasia wa Kijerumani kuingilia kati ningepotezwa.

IGP Sirro anasema sistahili kupewa ulinzi wowote kwa sababu mimi ni Mtanzania sawa na Watanzania wengine. Lakini sio Watanzania whote waliowahi kushambuliwa kwa risasi 16 wala kutendewa kama nilivyotendewa mimi. Majibu yake ni utetezi wa wauaji wasiojulikana na wale waliowatuma!
View attachment 1849851
HUYU SIRRO MZEE MUOVU SANA. JPM MUNGU ASINGEMUONDOA MAPEMA, TANZANIA INGEKUWA KAMA UGANDA WAKATI WA IDDI AMINI KUNUKA DAMU ZA WANADAMU. LAKINI MUNGU NI FUNDI PEKEE!
 
Back
Top Bottom