Wananchi wanataka kufahamu yafuatayo:
1. Wahitimu watalipa asilimia ngapi ya mkopo kutoka bodi ya mikopo na ni kwa muda gani.
Maana hata huko Ulaya mhitimu huwekewa kiasi cha mshahara alo nao ili akipata kazi tu huanza kurejesha mkopo wake hata kwa miaka 30.
2. Kama Tundu Lissu angekuwa yeye ndie anaongoza serikali angefidia vipi kodi alozifuta?
Na je, atatumia vyanzo gani vya mapato kuendesha serikali?
3. Hiyo tozo ya 20,000 ni administrative cost ya kutengeneza hiyo kadi lakini kwa mawazo yangu, hiyo kadi ingeungaishwa iwe kadi moja yenye TIN, kitambulisho cha taifa, kitambulisho cha mpiga kura na kitambulisho cha mjasiriamali.
Nchi kama Estonia wana aina hii ya kitambulisho hivyo ni rahisi kuzungumza nao kwa ushauri.
4. Nilifarijika sana kuona barakoa za kitanzania na zinazotengenezwa na moja ya viwanda vyetu vya hapahapa nchini.
Pia nilifarajika sana kuona kifumba uso Face Cover ambayo pia imetengenezwa hapahapa Tanzania baada ya sakasaka la COVID -19
Sasa Tundu Lissu anaposema kwamba atahakikisha anaruhusu bidhaa za kutoka nje kwa kuwa na soko huru si anazuia ukuaji wa ubunivu na uzalishaji wa bidhaa za kitanzania?
Sasa hapa mbona tunakuwa tunarudi kulekule miaka ya nyuma ambapo Tanzania ikigeuzwa kuwa dampo la bidhaa za nje?
5. Je, hawa wamachinga suluhisho lake limekaa vipi maana sijasikia ama CCM wala Chadema wakisema watalishughulikia vipi suala la wamachinga.
Maana tungesema sera ya kilimo ingekuwa ni kipaumbele je, ni kilimo kitakuwa ni kipaumbele au serikali ya CCM ina mikakati gani na Chadema nao wana mikakati ipi kuhusu sera ya kilimo?
Kwenye kilimo kuna kubadili njia za uzalishaji, njia ya uhifadhi wa mazao na njia ya uuzaji wa mazo na bidhaa za kilimo.
Kilimo cha kisasa ndo njia pekee ya kuonyesha moja ya tofauti maendeleo katika sekta hiyo.
How to sort out machinga situation in our country, iwe ni wahitimu wa vyuo ambao ni wamachinga na wamachinga wa kawaida?