johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Wote wanasema wamekuja kupata Neno la Kwanza la Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Tundu Lissu na makamu wake Mh John Heche wakiwa rasmi ofisini
Ngoja tumsikie.
TUNDU LISSU
"Kwa sababu ya majukumu makubwa tuliyonayo mbele ya safari naomba mniruhusu nikaribishe wote ambao sio wanachama wetu wajiunge na CHADEMA tunahitaji nguvu kubwa tunahitaji jeshi kubwa zaidi mara dufu ya tulilonalo tunahitaji kila mtu alete karama, talanta zake kwenye hii kazi inayohitajika kufanyika kwa pamoja. Nikaribishe wote ambao kwa sababu mbalimbalo hawajawa bado wanachama wawe wanachama wetu.""Tuna uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba na kuna No reform no election(hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi).
Hayo mambo mawili hayaendi pamoja hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi sio hatutasusia uchaguzi tunaenda kujifungia tuijadili tuna chama haitakuwa uamuzi wa Tundu Lissu, itakuwa ni uamuzi wa chama tutakaa viongozi tutakaa na Sekretarieti tutakaa na Kamati Kuu, tutatoka na msimamo ukitoka msimamo utakuwa ni msimamo wa chama. Ninachoweza kusema tu ni kwamba sasa inabidi tuzungumze lugha pekee anayoweza kuielewa Rais Samia Suluhu Hassan.”
JOHN HECHE
“Nimememuona Mzee Wasira(Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara) amekuwa serikalini tangu akiwa na miaka 20 mimi sijazaliwa. Anataka atengeneze kama mabishano fulani na Mwenyekiti wetu wa taifa kwamba Wasira amshughulikia Lissu. Mzee Wasira Lissu atashughulika na Rais. Lissu anakuja kushughulika na Rais Samia hakuna nafasi ya Lissu kushughulika nawe. Wasira yule hawezi kuja na mawazo mapya kwa watu wamemaliza vyuo vikuu hawana ajira”
"Hakuna mtu atapata upendeleo kwa sababu alimuunga Lissu mkono na Heche tutachagua watu kutokana na uwezo, uwezo wako utakuweka kwenye nafasi tulihubiri mabadiliko na tutasimamia mabadiliko hakuna mtu ataonewa kwa sababu hakutuunga mkono kuweni na amani kabisa. Nataka niwaambieni wanachama wetu wanataka kutumia watu fulani hivi tupoteze muelekeo hiyo nafasi haipo. Tutawashughulikia sana, tutaacha kushughulika na CCM iwe tumekufa au tupo gerezani. Mtatunyamazisha tumekufa au tupo gerezani vinginevyo hakuna msalia mtume kwa hiyo msiwe na mashaka kwamba chama hakitaenda."