Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

Huwa najiuliza kwanini watu huwa wanamsema Pasco kuwa anatafuta teuzi? Lakini pia najiuliza hivi huwa anaandika akijua ni yeye tu anayejua? Hivi kila akionacho yeye kuwa ni 'kweli' kinakuwa kweli kwa wote? Huwa sipati majibu ila naigundua tofauti kati ya P huyu na P yule wa zamani
kwenye Tv
 
Kilichomkuta Zito ni nia yake ya kugombea uenyekiti na sio urais..na huyu lissu ndo alishiriki kikamirifu kumuondoa Zito pale CDM
 
Kiukweli leo ndo najua chadema Wana viongozi Wa Maisha haijawahi kutajwa hii kwamba waliondoa kipengele cha ukomo Wa viongozi wao nadhani hapa mlengwa alikua ni mweneyekiti mbowe aendelee kusalia kwenye kiti kwa kisingizio hawana mtu wa kushika wadhfa huo inasikitisha na kufikirisha sana nadhani hao viongozi wengine wamewekwa kama geresha flani hivi lengo ni mwenyekiti adumu milele..
 

Pasko kakosea nn sasa hapo yeye kamsifia lissu kua mkweli kuhusu mwwnyekiti Wa maisha mwamba ni kweli kipengele kiliondolewa ili tu mbowe aendelee na walifanya hivo ili kuua Fikra kama za kina Zitto kabwe za kuutamani uenyekiti
 
Zito alikuwa haaminiki.
Zito alikua haaminiki !? Kutokuaminika kwa Zitto kuna uhusiano gani na kunyofoa kioengele cha ukomo wa mwenyekiti....na hayo Ndo maneno waliolishwa wanaCDM Kipindi kile ili tu kumuondoa zito na mwenyekiti aendelee milele..na wakafika mbali wakanyofoa kipengele cha ukomo Wa mwenyekiti..
 

Hoja yako ni ipi hapa? Mbona ni kama umepanick?!
 
Wanabodi

Jana nimetazama mahojiano ya Tundu Lissu kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV na kumsikiliza kwa makini Tundu Lissu, nikafarijika sana kwa jinsi Tundu Lissu alivyokuwa mkweli.
Paskali
Nimeona hii habari huko Twitter. Inasema kuwa Mbowe alikuwa mwenyekiti wa CDM mwaka 2004. Wakati huo katiba ya chama ilikuwa imezungumza kuwa kutakuwa na ukomo wa miaka kumi kwa mwenyekiti.
Mkuu Wakili wa shetani, hapo juu Lissu amekujibu ila ni kweli Mbowe alipoingia kuwa Mwenyekiti wa Chadema, katiba ya Chadema ilikuwa na ukomo wa uongozi mwisho ni vipindi 2 vya miaka 5 jumla ni miaka 10.
Mwaka 2006 yalifanyika mabadiliko ya katiba. Lakini suala la ukomo wa uongozi halikuzungumzwa kwenye mkutano.
Ni kweli 2006 Chadema walifanya mabadiliko ya katiba na ni kweli kipengele hicho hakikujadiliwa.
Inasema kuwa katiba ilipoendwa kuchapwa, Mbowe akaondoa kipengele cha ukomo wa uongozi kinyemela. Hii ndiyo hadi leo mwaka wa 20 bado ni mwenyekiti.

Madai haya yanaukweli wowote?
Ni kweli katiba ilipoenda kuchapwa, hicho kipengele hakikuwepo, kiliyeyuka ila aliyekiyeyusha sio lazima awe ni Mbowe.

Hili jambo tuliisha lijadili humu kwa kirefu, Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
Dr. Slaa alikuwa KM na alichangia Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

na JJ Mnyika akiwa Mkurugenzi wa Habari wa Chadema pia alichangia Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
Nyuzi nyingine zinazohisiana na hili ni hizi Hatma ya Freeman Mbowe CHADEMA Elections 2015 - CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu! ila juzi kati hapa hili jambo Lissu kalifafanua vizuri kabisa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

P
 
Stan Katabalo, Azory Gwanda, Mwangosi, Steven Ulimboka (si mwandishi lkn ni binadamu nae) Saed Kubenea, Jamal Kashogi, Julian Asange na list inaendelea.
Msioneshe tu watu waliopata madhara kipindi cha JPM ili kumchafua! Hata USA yanatokea. Tutoe mifano kimataifa pia. Juzi kuna mtangazaji UK anaitwa Gary Lineker amefukuzwa kazi kwa kutoa maoni kuhusu sera mbaya ya uhamiaji!
 
Acha ushabiki mandazi!
 
Hata ndani ya vyama wanagombea

Cc johnthebaptist
Ndani ya vyama ni kugombea kuteuliwa, ukiisha shinda uteuzi wa ndani ya chama ndipo sasa unagombea uongozi.

Hata CCM, japo ina utaratibu wa rais aliyemadarakani hapingwi mid term hivyo mgombea wa urais wa CCM kwa uchaguzi wa 2025 ni mmoja tuu, Samia Suluhu Hassan, lakini kamwe huwezi kumsikia Samia akisema ni yeye atagombea urais 2025, bali wakati utakapofika, Samia ataomba kuteuliwa na CCM, akiishateuliwa sasa ndio anakuwa mgombea.

Wanachadema kubalini kataeni kitendo cha Tundu Lissu kusema ni yeye atagombea urais 2025 kwa tiketi ya Chadema, it's a mistake!. Unaweza kutangaza nia ya kugombea lakini sio kusema atagombea!.

Kosa kama hili la Lissu, Zitto alilifanya na alishughulikiwa ipasavyo nikiwemo mimi Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!.

Kitendo cha Tundu Lissu kutangaza expressly kuwa atagombea urais wa 2025 kupitia Chadema, tangazo hilo litawafanya presidential hopefuls wengine wote wa Chadema wasithubutu kumpinga Lissu.

Hii tabia ya viongozi wa Chadema waliogombea nafasi fulani kujimilikisha kugombea tena ndicho kilichomtoa Dr. Slaa Chadema baada ya kumpokea Edward Lowassa na kumfanya ni mgombea wake Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM!

Hivyo ikitokea Chadema ikapata mgombea bora zaidi wa urais 2025 kuliko Lissu, Jee Lissu atakubali?.
P
 
facts, CHADEMA ni wanadamu tu kama walivyo TLP, CUF na chama cha waasi wa CCM yani CCK.
 
Afadhali leo ndio TL amelizungumzia hili, anashangiliwa, kama hakuna ukomo, then hakuna kung'ang'ania madaraka,hili neno kung'ang'ania madaraka ni kumsema mtu kwa mlango wa nyuma!。

Msikilize TL hapa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

Siku nilipoibua hii issue ya ukomo wa madaraka, KM wa wakati huo, Dr Slaa, aliruka kimanga na kuniparua Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Nilipolisema hili, niliparuliwa, sasa leo TL kayasema, nasubiria kuona kama je na yeye ataparuliwa?。
P
 
Pasco, natumai utahusika sana kwenye siasa za 2025 kama katiba mpya na tume zitapatikana.
 
P huwa adui anaombewa njaa kwani TL adui yako?Inakuwaje umwoombee kuparuliwa.
 
Anafuata falsafa za Cromwell kwamba watu waachiane madaraka na si kuganda tu.Ametoa mfano wa wenyeviti wa kwanza wa Chadema Mzee Mtei na W Amani walitumikia kipindi kimoja kimoja.
Hivyo Mbowe nae aachie kijiti kwa wengine.
It is not over until it is over.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…