Tundu Lissu: Kama mlifikiri kutufutia kesi ni hongo tunyamaze siku mkituibia, hiyo haipo

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu akiwa Mkoani Kagera, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, amemjibu Kinana aliyewatuhumu Viongozi waandamizi wa CHADEMA kukosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hasani aliyewafutia kesi.

Lissu amesema, hawawezi kushukuru kwa kufutiwa kesi za uwongo ambazo Rais mwenyewe amewahi kukiri hadharani kuwa zilikuwa za uwongo.

"Nakufungulia kesi ya uwongo, nakutesa, nakuweka gerezani, Mwenyekiti amekaa gerezani miezi minane, ameachiwa bure mlitaka apige magoti kushukuru?.."

“Sisi ukitufunga bure TUTAKUSEMA, ukituachia baada ya kutufunga bure TUTAKUSEMA, ukiiba TUTAKUSEMA, ukigawa nchi yetu kwa wageni TUTAKUSEMA, na tutakusema mchana kweupe, sisi hatuhongeki, kama mlifikiri mnatuachia kama hongo, hiyo haipo..." Tundu Lissu.

Huyo ndiye Lissu ‘White is White, Black is Black’.
 
Mwezi mchanga huu. Muacheni tu aendelee kuongea
 
Piga spana

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
 
Hivi wajuzi wa mambo nambieni ndani ya CCM kama kuna kiongozi mwenye IQ inayokaribiana na ya Lissu
 
Salute 100%
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…