Tundu Lissu: Kama mlifikiri kutufutia kesi ni hongo tunyamaze siku mkituibia, hiyo haipo

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu akiwa Mkoani Kagera, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, amemjibu Kinana aliyewatuhumu Viongozi waandamizi wa CHADEMA kukosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hasani aliyewafutia kesi.

Lissu amesema, hawawezi kushukuru kwa kufutiwa kesi za uwongo ambazo Rais mwenyewe amewahi kukiri hadharani kuwa zilikuwa za uwongo.

"Nakufungulia kesi ya uwongo, nakutesa, nakuweka gerezani, Mwenyekiti amekaa gerezani miezi minane, ameachiwa bure mlitaka apige magoti kushukuru?.."

“Sisi ukitufunga bure TUTAKUSEMA, ukituachia baada ya kutufunga bure TUTAKUSEMA, ukiiba TUTAKUSEMA, ukigawa nchi yetu kwa wageni TUTAKUSEMA, na tutakusema mchana kweupe, sisi hatuhongeki, kama mlifikiri mnatuachia kama hongo, hiyo haipo..." Tundu Lissu.

Huyo ndiye Lissu ‘White is White, Black is Black’.
Haya ndiyo yaliyojaa huko CCM.
Humsikii mtu yeyote akisema jambo, hata liwe bayana namna gani, kwa sababu wote ni watumwa wa hongo

Nafasi zote wanazopewa viongozi ni kwa hisani ya mteuzi.

Mteuzi huyo anaweza kufanya chochote cha hovyo, na wateuliwa watakuwa ndio wapo mstari wa mbele kutetea uovu huo.

Bunge zima, limekuwa kama la walevi tu!

Wakati wa Magufli hawa watu walikuwa na hofu, ikiwazuia kutumia akili zao. Sasa yupo Samia, yeye njia yake ni tofauti na ile ya Magufuli.
Samia anakuchekea, anakutolea sauti nyororo ya kukutia usingizin, lakini lengo ni lile lile la kunyamazisha.
 
Baada ya kusoma mada ilivyowasilishwa na mkuu 'Quinine', niliweka mawazo kabla sijaondoka kwenye uzi huu.

Lakini baada ya muda mfupi, nikaona nirudi haraka, huku nikibubujikwa na machozi yaliyoambatana na kicheko kisichokoma.

Tundu Lissu, sasa hivi kaeleza yale yale tuliyowahi kueleza humu humu JF kuhusu hizi mbinu za Bi Tozo.

Tundu Lissu anayo haki ya kuyasema aliyoyasema, kwa sababu hata siku moja hakuwahi kunaswa kwenye mtego anaoutumia Samia, lakini hali haikuwa hivyo na Mwenyekiti wa Chama.

Baada ya mkutano ule uliofanyika kule Marekani na wana-Diaspora wa huko. Mbowe alikuwa tayari ni mtu tofauti kabisa na yule tuliyekuwa tumemzoea siku zote.
Hali hiyo iliendelea kuwa hivyo, hata kwenye mkutano kule Mwanza, kwenye uwanja wa Furahisha, Mbowe hakuwa Mbowe wa siku zote. Na aliendelea kuwa na hali hiyo hiyo hadi wengine tukawa na hofu kwamba CHADEMA wametekwa, na inawezekana kuna mipango ya kuiingiza kwenye ulaji, kama wanavyofanya kule Kenya.
Hali ilikuwa inatisha sana kudhani kuwa chama hiki Kikuu cha upinzani kitakuwa sehemu ya unajisi unaofanywa na CCM ndani ya nchi hii.

Sasa ni wazi kwamba kazi kubwa sana imefanyika ndani ya chama kumwokoa mwenyekiti wao ambaye alikuwa tayari kishanaswa kwenye kokolo la Samia, kwa hizo hongo anazozieleza Tundu Lissu sasa hivi.

Tulishasema mara nyingi humu, kwamba njia anazotumia Samia inawezekana ni hatari zaidi kwa hivi vyama kuliko yale maguvu na vitisho vingi alivyokuwa akitumia Magufuli.

Sote sasa inabidi tutoe pumzi ya kushukuru, hatimaye ujanja wa Samia umegonga mwamba.

Asanteni CHADEMA, kwa kumwokoa Mwenyekiti wenu, na hatimaye kuwaeleza wananchi ulaghai mkubwa unaofanyika serikalini.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu akiwa Mkoani Kagera, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, amemjibu Kinana aliyewatuhumu Viongozi waandamizi wa CHADEMA kukosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hasani aliyewafutia kesi.

Lissu amesema, hawawezi kushukuru kwa kufutiwa kesi za uwongo ambazo Rais mwenyewe amewahi kukiri hadharani kuwa zilikuwa za uwongo.

"Nakufungulia kesi ya uwongo, nakutesa, nakuweka gerezani, Mwenyekiti amekaa gerezani miezi minane, ameachiwa bure mlitaka apige magoti kushukuru?.."

“Sisi ukitufunga bure TUTAKUSEMA, ukituachia baada ya kutufunga bure TUTAKUSEMA, ukiiba TUTAKUSEMA, ukigawa nchi yetu kwa wageni TUTAKUSEMA, na tutakusema mchana kweupe, sisi hatuhongeki, kama mlifikiri mnatuachia kama hongo, hiyo haipo..." Tundu Lissu.

Huyo ndiye Lissu ‘White is White, Black is Black’.
😂😂😂😂😂😂
 
Siku hizi umekuwa mjinga mpaka nakuhurumia, na nilijua tu toka siku ile ulipojitangaza kumuunga mkono Samia, ukihamia huko lazima akili zako umkabidhi mwenyekiti, jione sasa ulivyo!

Debe tupu.
Hata mimi nimeliona hilo.
Mtu akishajiunga na wajinga, hufanana nao
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu akiwa Mkoani Kagera, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, amemjibu Kinana aliyewatuhumu Viongozi waandamizi wa CHADEMA kukosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hasani aliyewafutia kesi.

Lissu amesema, hawawezi kushukuru kwa kufutiwa kesi za uwongo ambazo Rais mwenyewe amewahi kukiri hadharani kuwa zilikuwa za uwongo.

"Nakufungulia kesi ya uwongo, nakutesa, nakuweka gerezani, Mwenyekiti amekaa gerezani miezi minane, ameachiwa bure mlitaka apige magoti kushukuru?.."

“Sisi ukitufunga bure TUTAKUSEMA, ukituachia baada ya kutufunga bure TUTAKUSEMA, ukiiba TUTAKUSEMA, ukigawa nchi yetu kwa wageni TUTAKUSEMA, na tutakusema mchana kweupe, sisi hatuhongeki, kama mlifikiri mnatuachia kama hongo, hiyo haipo..." Tundu Lissu.

Huyo ndiye Lissu ‘White is White, Black is Black’.
Huyu jamaa yuko vizuri, ila kuna wakati anaenda ndivyo sivyo.
Yuko njema mno
 
Back
Top Bottom