Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Kamati Kuu itakaa kutoa msimamo rasmi juu ya Mbunge wa Nkasi, Aida Khenan

Kwani kina Mbowe walikuwa wanatetea nini bungeni huko, na kwa uchache wao walishawahi kupitisha nini?
Acheni ubinafsi nyie
 

Maeneo mengine siwezi kusema kwa kuwa sikuwa on the ground lakini kwa Hao Constituency kwa kaka Mbowe sina shaka na nasema Mbowe kapigwa kweupe na hakupiga kura sababu wananchi ndio waliokuwa hawamtaki.

Nimepita tarafa zifuatazo: Uroki, Nkira, Aishi, Uswaa, Nshara, Mamba, Kalali,Uraa, Kisiki, Nkoraya, Sonu, Kyeeri, Nkuu, Kisereni, Mwowe, Nkwarungo, Nkweseko.Matikoni, N'guni,Masama Magharibi, Masama Kusini, Kashinsha, Ivaeny, na kituo changu kikuu kilikuwa Lyamungo Sinde na Mwowe msikitini huku nikinywa chai na Bii mkubwa.

Na nimetembelea usiku ule mpaka asubuhi yake vijiji karibu 162.
 
Wangejua namna uyu dada ana pambana na game yake ilivo tight wangemuacha tu awahudumie wananchi walomchagua..other wise wanaonesha ubaguzi wa hali ya juu. We all know CCM lost the war.
 
Tofauti ya kura za Wabunge na Urais labda sijui majimbo mengine ambayo I was not on the ground, lakini kwa Jimbo la Hai ambako nilikuwepo siku tatu kabla ya Uchaguzi na siku tatu baada ya Uchaguzi, sikuliona hilo.

Hai ni moja ya Majimbo ya wajanja na walalamishi, sula hilo lingeibuka kule kule Hai, na hapa mtandaoni pangekuwa hapatoshi.
 
Kutaka kujua hiyo tofauti ni mpaka uwepo kila jimbo, au ni kupitia figure za tume? Hao watu wa Hai si ndio huko wapinzani walikuwa wanapigwa kwa maagizo ya DC chini ya uratibu wa OCD? Mitandao ipi wakati imefungwa na ushahidi mwingi unaowekwa hapa mnasema ni uzushi wa mitandaoni?
 
Tafadhali usipotoshe, nilikuwa Hai na interest yangu ilikuwa ni Uchaguzi na mimi ni mwanachama na sio shabiki wa Chadema.
1) Zilihesabiwa kura zote.
2) Kura alizo pata mshindi na zilibandikwa.
3) Kura alizo pata Mbowe na zilibandikwa.
4) Na kura za Rais zilibandikwa, tena Mbunge mteule Saasisha alilazimisha kura za Rais zitangazwe na akiwepo kwanza ndipo asaini form yake ya ushindi na kuondoka.

UCHAGUZI HUU HAI ULIKUWA NA MSISIMKO WA KIVYAKE NA KARIBU KILA MWANA HAI ALIJUHUSISHA NA UCHAGUZI HUU.

KWA HAI , HAKUNA CHA WIZI WALA BABAYAKE MWIZI. BINGWA KAPIGWA HANDS DOWN.

Uchaguzi umekwisha, sasa tuangalie jinsi gani mkate utafika juu ya meza. Ni jukumu lako kuifanyia mema Serikali na sio Serikali ikufanyie nini.
 
yale yale ya corona, wabunge wameenda bungeni wakafutwa uanachama, kwa kifupi chama cha kipuuzi sana hiki
 
Halafu akihamia CCM watasema kanunuliwa

Hapana..

Shida yake ni ubunge. Kama shida ni ubunge anaweza kuwa nao kwa kupitia forum yoyote..

In my opinion, CHADEMA hawana tatizo na Aida Khenan as a person..

CHADEMA wanatambua kuwa "ubunge" ni ajira tena inayolipa vizuri sana..

CHADEMA inatambua kuwa Aida Khenan anaihitaji ajira hiyo..

Shida iko kwenye mfumo unaotoa riziki kupitia ajira hiyo..

CHADEMA inapambana na mfumo huu..

Na kwa kuwa vita ni ya kimfumo zaidi, basi matokeo yake yatawaathiri individuals on the way...

Na hawa wanaoutawala mfumo huu wa dhuluma (yaani CCM na serikali yao), they know exactly what they are doing..

Mimi naamini, CHADEMA watakuwa na akili ktk kuamua hili jambo..

Binafsi nataka huyu mama asiwe mwathirika wa vita hii. Ni vyema akaitumikia ajira yake aliyoipata kwa jasho na damu...

Hata ikibidi ajisajiri CCM, wamwache afanye hivyo. Itafika wakati haya mambo yatafikia mwisho na kila kitu kitakuwa wazi...

Pia, hata hawa wabunge wa viti maalumu wateuliwe tu kisha waende..
 
Wewe unaefikiria kwa kutumia tumbo ndo hauko serious. Kama sio chadema kumpa dhamana hio kazi unayodai angeitoa wapi?
Amechaguliwa na wananchi. We unadhani mbowe angeshinda angesusa?
 
Wanasiasa wengi wa Tanzania wako hivyo (kama wewe). Wengi tu wanampigia dikteta makofi kwa mawazo kama haya yako. Siyo kwamba wanampenda. Na hata huyo Aida anafikiria kama wewe. Ndio maana analazimisha kwenda. Ushenzi wote uliofanyika, ameshasahau!
Mimi sio mwanasiasa, siwezi kuwa na fikra kama zao
 
 
Tulisema kuwa mtakimbiana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…