Tundu Lissu: Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Yatoka na Maazimio nane dhidi yake

Tundu Lissu: Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Yatoka na Maazimio nane dhidi yake

Beberu ni mbuzi Dume ina maana ccm ni mbuzi jike? Meko si kasema wanazo pesa zao Nchi ni Tajiri iweje wanaanza kuchachawa?
MEKO na GENGE lake wanajimwambafai tu , si umeona sakata la Zito na Fedha za Bank ya Dunia. mpaka wanapendekeza MTU AUAWE. njaa kitu kibaya sana ,tena hawa wananjaa ya Tumbo na Njaa ya Kichwani.
Na bahati mbaya BEBERU kashanusa mkojo......
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema- Bara, Tundu Lissu
Moshi. Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) umetoa tamko kuhusu sakata la mbunge bwa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu likipendekeza kuundwa kwa jopo la wajumbe watakaomsindikiza kurejea nchini.

Chombo hicho pia kimeeleza kushangazwa na kitendo cha Bunge la Jamhuri ya Muungano kutounda kamati kuchunguza shambulio dhidi ya Lissu wakati alipata tatizo hilo akitokea katika shughuli za kibunge.

Lakini Spika Job Ndugai naye amemshangaa Lissu kwa kupeleka malalamiko yake IPU wakati suala lake liko mahakamani na huku akijua kuwa chombo hicho hakina uwezo wa kisheria kutekeleza maamuzi yake.

Lissu, ambaye pia alikuwa Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitangaza kurejea nchini Septemba 7, 2019, lakini baadaye akafuta mpango huo kwa kile alichodai kuwa ni sababu za kiusalama.

Lissu alishambuliwa kwa risasi zipatazo 30 akiwa ndani ya gari, nje ya makazi yake jijini Dodoma Septemba 7, 2017 na siku hiyo usiku alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Baada ya hali yake kuimarika, alihamishiwa Ubelgiji kwa ajili ya kurekebisha mifupa iliyoharibiwa na risasi.

Lakini akiwa Ubelgiji, Spiga Ndugai alitangaza kiti chake kuwa wazi kwa maelezo kuwa hajulikani alipo na hakujaza fomu za mali na madeni.

Jana, alipoulizwa kuhusu taarifa ya IPU, Ndugai alisema atatoa taarifa Ijumaa, siku ambayo Bunge litaahirisha shughuli zake.

“Sijaliona (tamko la IPU) kabisa, lakini nikiliona nitakuwa tayari kueleza, nitatoa ufafanuzi,” alisema Ndugai.

“Cha muhimu ni kwamba IPU ni umoja wa mabunge yaliyo chini ya mwamvuli wa mfumo wa Umoja wa Mataifa, si chombo cha uchunguzi.

“Nisiseme sana nitasema keshokutwa. (Lissu) amepeleka kesi mahakamani sasa IPU itaingiliaje mambo ya ndani ya nchi ambayo yanahusisha mahakama?”

Uamuzi wa IPU kupendekeza kuundwa kwa kamati ndogo ya kumsindikiza Lissu, umetolewa na Kamati ya Haki za Binadamu ya IPU baada ya kusikiliza malalamiko yake.

Kamati hiyo pia ilisikiliza malalamiko ya wabunge 90 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambao ubunge wao ulibatilishwa na pia ilitoa maamuzi dhidi ya malalamiko ya wabunge kutoka nchi za Ecuador, Venezuela, Maldives, Mongolia, Philippines, Israel na Palestina.

Katika moja ya maamuzi nane ya kamati, kwa mujibu wa taarifa rasmi ya IPU iliyosambaa mitandaoni jana, ni pendekezo la kumsindikiza Lissu.

“Kamati inaamini kuzuru Tanzania kutatoa fursa muhimu kukutana na Serikali, Bunge na mahakama au mtu yeyote atakayesaidia kutoa uelewa wa suala hilo la kurejea kwa Lissu,” inasema.

Inasema kamati inaamini kwamba mamlaka ya Bunge la Tanzania itajibu maombi ya kamati hiyo ya IPU iliyokutana Geneva, Uswisi kati ya Januari 20 hadi 30.

Kamati pia imekubali kuwa malalamiko ya Lissu yanakubalika chini ya kanuni za uchunguzi na uamuzi wa malalamiko za IPU na ina mamlaka ya kuchunguza.

Mbali na hilo, kamati hiyo imesikitishwa na jaribio la mauaji dhidi ya Lissu na tuhuma dhidi ya mamlaka katika jaribio hilo ambalo imesema Lissu alinusurika kimiujiza.

Kamati hiyo imesema ni jambo linalolatiza kwamba Lissu alivuliwa ubunge wake wakati ilikuwa wazi kwa Bunge na umma kwamba Lissu alikuwa nje kwa matibabu kutokana na shambulio hilo.

“Kamati inapongeza hatua za haraka zilizochukuliwa kumpeleka eneo salama na kuhakikisha anapata matibabu, lakini inataka kujua Bunge lilichukua hatua gani kufuatilia uchunguzi,” inasema.

Hivyo kamati inasema inapenda kupata maoni kutoka kwa mamlaka ya chombo hicho cha kutunga sheria kuhusu sababu Lissu avuliwe ubunge.

Kamati hiyo pia inataka kupata taarifa rasmi ya Serikali kuhusu ukweli na uhalali wa kisheria kuhusu kila hatua inayohusu kukamatwa kwake na kushitakiwa mahakamani.

Kamati hiyo poia inasema inatambua Lissu anataka kurejea Tanzania haraka, hivyo imeshauri kuundwe kamati ndogo ambayo itamsindikiza hadi Tanzania siku atakapokuwa akirejea.

Kamati imemuomba katibu mkuu wa IPU kuwasilisha uamuzi huo kwa mamlaka ya kibunge ya Tanzania na kuomba ruhusa ya kutembelea Tanzania kama ilivyopendekezwa.

Pia Kamati itaendelea na uchunguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo ndiyo kwanza yanaanza ‘Aluta Continue’.

Kwa kumponya Lissu nadhani Mungu alikuwa na makusidio mengi. Moja ni kwamba aendelea kuwa kielelezo hai cha jinsi wanadamu walioaminiwa na wenzao wanavyoweza kuwa wabaya kiasi cha kukufuru dhamana waliyopewa na umma kwa maslahi yao binafsi.

Lissu angefariki katika shambulio hilo unyama huu ungekuwa umeshasahaulika kabisa. Maadam yuko hai tutaendelea kukumbushwa unyama huo. Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu tunasubiri kwa hamu kuona kama chama cha siasa kilichowadhamini watu hao kimejitafakari!
 
So, TL atapata escort ya delegates kutoka IPU wakati anarudi hapa nchini na itakuwa very soon? Nice move.

Naamini hapo ulinzi wake utakuwa wa kiwango cha juu sana.


Subiri aje Musiba awatishe na hao wajumbe wa IPU kwamba wakikanyaga ardhi ya Tanzania tu wanauwa!

Kiburi kabla ya kufikwa na kifo ni hatari sana. Ngoja Tanzania isikie kibano cha kimataifa ndiyo tutaelewa jeuri ya kijamaa na ubabe wa kimaskini havina tija katika anga za Dunia ya sasa.
 
huyu sipuka hana akili hata kidogo yaani bado ana mawazo ya kitoto kwamba tanzania ni nchi huru
 
Kalamu1,
Mkuu ukifuatilia mijadala ya sasa ya bunge linaloendelea utagundua kwa ushabiki wa Ndugai na kuacha majukumu yake kama Spika ni ishara ya matatizo kwenye afya yake , sidhani kama ni mzima
 
Hii document haisemi chochote cha maana chenye nguvu kinachofanya watu kusherehekea. Inatumia indecisive keywords kama vile "Notes", "Is concerned", "Is troubled",

"Requests' wala haina statement inayosema "Resolved that ..."kuhitimisha tamko la kulitaka bunge la Tanzania lifanye nini kulingana na malalam9iko ya Lissu. Hata ombi la Lissu la kusindikizwa na kamati ndogo ya Kamati hiyo nalo halikuamriwa limeachwa linafloat tu.
 
Hii ni nzuri kama RECORD KEEPING, yaani kupeleka malalamiko yake IPU, ni kumbukumbu, iwapo mambo yatazidi kuharibika na itakuwa reference kwa IPU kuendeleza kuipigi kelele serekali ya TZ.

Kisu cha IPU hakina Makali yoyote ni sawa na NGO isiyo na uwezo, ila ina budget ya kuendesha mkusanyiko wa kubadilishana mawazo.

Lissu anajitayarisha vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
So, TL atapata escort ya delegates kutoka IPU wakati anarudi hapa nchini na itakuwa very soon? Nice move.

Naamini hapo ulinzi wake utakuwa wa kiwango cha juu sana.
Jee wataishi naye, shida sio kumsindikiza, huko hakumfaidii Lisu, bali kinaijengea Sifa na Per Diem Allowance wabunge wao na kuwapa publicly.

Lissu umaarufu wake umemtengenezea maadui na wafuasi wengi, maadui zake sio wa serekali tuu, hao ni washindani wake wa Jadi, lakini wale wa upinzani na waliokuwa na mrengo mmoja wa siasa, nao pia wanamuona ni tishio.

Pia kuna wafanyi biashara Lissu na chama chake wanawaona ni wafadhili wa ccm, na ndio wanao waangusha wasishike dola n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom