Tundu Lissu; Kila atiapo mguu nguvu kubwa inatumika ila mwishoni anashinda, hatujifunzi tu?

Chakaza

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
41,034
Reaction score
74,732
Nimejaribu kufuatilia harakati za Mwenyekiti Tundu Lissu na kugundua ambalo wengi hawalioni, kila ajiingizapo hashindwi na mwishoni anafanikiwa.

Mifano:
1. 2010 alipogombea ubunge Rais Kikwete alitumia kampeni ya nguvu kuwa tahadharisha watu kuwa ni bora kumchagua urais Dr Slaa kuliko kumpa ubunge Lissu na alishinda kwa kishindo kikubwa.

2. Aliamua kugombea urais wa TLS na serikali ikatumia nguvu kubwa kuhakikisha hawezi kuwa kiongozi wa TLS hadi kutumia polisi kumuweka ndani ili ashindwe kuwahi Arusha kushiriki lakini hatimae alishinda urais wa TLS na kuanzia hapo cheo hicho kikapata umaarufu.

3. Alipambana bungeni kuhusu mikataba ya Makinikia huku dhahabu ikiibiwa kwenda nje hadi akaitwa msaliti na apotezwe. Risasi 16 zikashindwa kumuondoa.

4. Ameamua kugombea Uenyekiti Chadema CCM na dola wametumia nguvu kubwa kuhakikisha kila kitu kifanyike asishinde nafasi hiyo. Lakini hatimaye katika uchaguzi huru akashinda.

5. Sasa hili la sasa ambalo ingawa Chadema hawaja mdhibitisha kuwa mgombea ila picha inasomeka hivyo, tayari hujuma dhidi yake zimeanza ikiwemo kumfungulia kesi nzito kuliko zote nchini yaani UHAINI.

Je, hatima ya Lissu itarejea palepale kuwa huwa anamaliza mshindi? Msimamo wa No reforms no election utafaulu?

Je, huyu kiumbe ni mteule wa Mungu na kuwa mapenzi ya Mungu huwa lazima yatimizwe?
Tumewahi kuyaona yaliyowapata huko nyuma marais wa Zambia na Senegal na hatima zao leo hii. Viongozi na wakuu wa polisi hali hii haiwatii hofu kupambana na mapenzi ya Mungu?
 
Jee tunakubaliana na mzee Warioba?
 
Attachments

  • 20250214_195258.jpg
    20250214_195258.jpg
    126.5 KB · Views: 39
6. Mwaka 2020 aligombea urais akashindwa vibaya akaenda uhamisho akarudi kwa huruma ya Samia! Mbona umejisahaulisha hii makusudi!
2020 wakati wa Magufuli hapakuwa na uchaguzi ila UCHAFUZI na kusudio baya dhidi yake lilifanyika ila ubalozi wa Germany ndio ulimuokoa na kumsindikiza hadi Airport. Au ulikuwa huko Nanjilinji hakuna mtandao wa kujua ya dunia?
 
Safari hii kutakua na uchaguzi ?
 
lisu ni kibaraka wa nchi za ulaya, na watamtumia huyu huyu kuhalibu amani ya Tanzania watanzania tujitambue hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania
Ukikosa elimu unaweza kuimbishwa nyimbo bila kujielewa. Nchi inapelekwa katika namna ambayo sio sawa na mnapiga makofi
 
Attachments

  • mzalendotv_online_1744611093736332.mp4
    2 MB
Nimejaribu kufuatilia harakati za Mwenyekiti Tundu Lissu na kugundua ambalo wengi hawalioni, kila ajiingizapo hashindwi na mwishoni anafanikiwa.

Mifano:
1. 2010 alipogombea ubunge Rais Kikwete alitumia kampeni ya nguvu kuwa tahadharisha watu kuwa ni bora kumchagua urais Dr Slaa kuliko kumpa ubunge Lissu na alishinda kwa kishindo kikubwa.

2. Aliamua kugombea urais wa TLS na serikali ikatumia nguvu kubwa kuhakikisha hawezi kuwa kiongozi wa TLS hadi kutumia polisi kumuweka ndani ili ashindwe kuwahi Arusha kushiriki lakini hatimae alishinda urais wa TLS na kuanzia hapo cheo hicho kikapata umaarufu.

3. Alipambana bungeni kuhusu mikataba ya Makinikia huku dhahabu ikiibiwa kwenda nje hadi akaitwa msaliti na apotezwe. Risasi 16 zikashindwa kumuondoa.

4. Ameamua kugombea Uenyekiti Chadema CCM na dola wametumia nguvu kubwa kuhakikisha kila kitu kifanyike asishinde nafasi hiyo. Lakini hatimaye katika uchaguzi huru akashinda.

5. Sasa hili la sasa ambalo ingawa Chadema hawaja mdhibitisha kuwa mgombea ila picha inasomeka hivyo, tayari hujuma dhidi yake zimeanza ikiwemo kumfungulia kesi nzito kuliko zote nchini yaani UHAINI.

Je, hatima ya Lissu itarejea palepale kuwa huwa anamaliza mshindi? Msimamo wa No reforms no election utafaulu?

Je, huyu kiumbe ni mteule wa Mungu na kuwa mapenzi ya Mungu huwa lazima yatimizwe?
Tumewahi kuyaona yaliyowapata huko nyuma marais wa Zambia na Senegal na hatima zao leo hii. Viongozi na wakuu wa polisi hali hii haiwatii hofu kupambana na mapenzi ya Mungu?
Mwenzenu ananyea ndoo,nyie mpo kwenye keyboard.. anyways,lissu anapaswa kufungiwa kwenye chumba chenye kiza kwa miaka kumi,asituvurugie nchi
 
lisu ni kibaraka wa nchi za ulaya, na watamtumia huyu huyu kuhalibu amani ya Tanzania watanzania tujitambue hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania
Kibaraka kivipi? Hivi CCM bado mnaamini Watanzania tutawaamini na propaganda zenu mfu hizo?

Lissu anayetetea rasilimali za Taifa na nyie mnaozipora na kuziuza alafu hela mnakula wenyewe nani kibaraka? Tena nyie ni mashetani kabisa.
 
Back
Top Bottom