Tundu Lissu; Kila atiapo mguu nguvu kubwa inatumika ila mwishoni anashinda, hatujifunzi tu?

Tundu Lissu; Kila atiapo mguu nguvu kubwa inatumika ila mwishoni anashinda, hatujifunzi tu?

6. Mwaka 2020 aligombea urais akashindwa vibaya akaenda uhamisho akarudi kwa huruma ya Samia! Mbona umejisahaulisha hii makusudi!
Matokeo ya urais ,sheria inatamka ni lazima yatangazwe gazetini , tuoneshe gazeti lipi la kilasiku laserikali lilitsngaza au binafsi
 
Kibaraka kivipi? Hivi CCM bado mnaamini Watanzania tutawaamini na propaganda zenu mfu hizo?

Lissu anayetetea rasilimali za Taifa na nyie mnaozipora na kuziuza alafu hela mnakula wenyewe nani kibaraka? Tena nyie ni mashetani kabisa.
Waambie hawa wanajifanya hawajui nan ndo jambazi mkuu(kibaraka) nchini👿
 
Ukikosa elimu unaweza kuimbishwa nyimbo bila kujielewa. Nchi inapelekwa katika namna ambayo sio sawa na mnapiga makofi
Mkuu huyo lisu mwenyewe na wenzake wanagombana kila siku, unategemea nini!? Mimi sina chama, ila baadhi ya vyama vinaudhaifu mkubwa Sana.
 
. Aliamua kugombea urais wa TLS na serikali ikatumia nguvu kubwa kuhakikisha hawezi kuwa kiongozi wa TLS hadi kutumia polisi kumuweka ndani ili ashindwe kuwahi Arusha kushiriki lakini hatimae alishinda urais wa TLS na kuanzia hapo cheo hicho kikapata umaarufu
TLS ilikiwa haifamiki hadi TL alipogombea. Mshike mshike wake ilikuwa balaa. Vipenyo walipenyezwa na bado wakaangukia pua
 
Hana hela kweli, lakini hao jamaa wanaakiri Sana maana wamegundua jamaa japokua hana hela, ila anaushawishi wakutosha hivo ni rahisi kumtumia kutimiza marengo yao.
Ana hela gani yule bwana? Vibaraka kweli wanakuwa na uwezo, pesa, utajiri. Kama huna hivyo vitu unavurugaje nchi?

Hamna mtu ana invest kwa masikini atarajie matokeo
 
Nimejaribu kufuatilia harakati za Mwenyekiti Tundu Lissu na kugundua ambalo wengi hawalioni, kila ajiingizapo hashindwi na mwishoni anafanikiwa.

Mifano:
1. 2010 alipogombea ubunge Rais Kikwete alitumia kampeni ya nguvu kuwa tahadharisha watu kuwa ni bora kumchagua urais Dr Slaa kuliko kumpa ubunge Lissu na alishinda kwa kishindo kikubwa.

2. Aliamua kugombea urais wa TLS na serikali ikatumia nguvu kubwa kuhakikisha hawezi kuwa kiongozi wa TLS hadi kutumia polisi kumuweka ndani ili ashindwe kuwahi Arusha kushiriki lakini hatimae alishinda urais wa TLS na kuanzia hapo cheo hicho kikapata umaarufu.

3. Alipambana bungeni kuhusu mikataba ya Makinikia huku dhahabu ikiibiwa kwenda nje hadi akaitwa msaliti na apotezwe. Risasi 16 zikashindwa kumuondoa.

4. Ameamua kugombea Uenyekiti Chadema CCM na dola wametumia nguvu kubwa kuhakikisha kila kitu kifanyike asishinde nafasi hiyo. Lakini hatimaye katika uchaguzi huru akashinda.

5. Sasa hili la sasa ambalo ingawa Chadema hawaja mdhibitisha kuwa mgombea ila picha inasomeka hivyo, tayari hujuma dhidi yake zimeanza ikiwemo kumfungulia kesi nzito kuliko zote nchini yaani UHAINI.

Je, hatima ya Lissu itarejea palepale kuwa huwa anamaliza mshindi? Msimamo wa No reforms no election utafaulu?

Je, huyu kiumbe ni mteule wa Mungu na kuwa mapenzi ya Mungu huwa lazima yatimizwe?
Tumewahi kuyaona yaliyowapata huko nyuma marais wa Zambia na Senegal na hatima zao leo hii. Viongozi na wakuu wa polisi hali hii haiwatii hofu kupambana na mapenzi ya Mungu?
Yule ni mtu na nusu hakuna mtu yoyote kwenye hii nchi ambae anamfikia
 
Back
Top Bottom