Sikufahamu kuwa ukoo chini kiasi hiki katika uelewa wako.

Kumbe unajisemea tu mambo usiyo kuwa hata na chembe ndogo ya ufahamu juu yake; halafu unakija humu JF kupotosha watu kana kwamba wewe ndiye mjuaji mkuu.

Haya ndiyo matatizo makubwa tukiyo nayo katika hizi serikali zetu mbovu hizi. Watu wa aina yako, wasiojuwa kitu ndio mmeshikilia nafasi za maamuzi yanayo husu maisha ya wananchi. Kila jambo mnafanya nje ya sheria, kwa kujiapiza nyinyi mnajuwa kila kitu; kuliko sheria inavyo elekeza.
 
sawa mkuu mjuzi wa yote..
 
sawa mkuu mjuzi wa yote..
Hapana.
Mimi siyo "mjuzi wa yote", lakini ninapo ona upotoshaji wa maksudi kabisa kama unavyo fanya wewe, kamwe siwezi kuuacha uposhaji huo usimame.

Maelezo yako juu ya swala hili toka mwanzo ni wazi kabisa kuwa yanapotosha tu; hayaelezi uhalisia wenyewe ulivyo katika nchi hizo unazo zitolea mifano.
 
πŸ˜‚ hamtakuja kuelewa mpk damu imtoke kenge!.
 
πŸ˜‚ hamtakuja kuelewa mpk damu imtoke kenge!.
Sasa hii mipasho ni ya nini tena hapa!
Kisicho eleweka ni kitu gani kwenye mada hii inayo jadiliwa hapa. Kupotosha hakuwezi kamwe kuwa sehemu ya kuelewesha. Ni kinyume chake.
 
Out of nowhere, katika mgogoro wake na TIGO mh Lissu bila kupepesa macho, amesema anaenda kwenye mahakama ambazo zikitoa amri ya kukamatwa ndege basi zinakamatwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Lissu kuonesha mapenzi ya sio ya kawaida kwa ndege hizi. Itakumbukwa sababu ya ndege zetu kukamatwa kipindi cha nyuma ilikuwa baada ya Lissu kuuza 'password' kwa mabeberu.

Naomba serikali yangu, kwa moyo mkunjufu wampe ndege moja ili kuondoa migongano isiyo kuwa na ulazima.
 
Bilionea mtarajiwa Ndugu Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti Dr Tundu Lissu (Mbunge Mstaafu na Mgombea Urais 2020 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) aongezewe ulinzi kwa sasa. Watesi wasije wakamdhuru (tena).
 
TAL ni Daudi wa zama hizi. Wasomaji wa Biblia watakumbuka jinsi Mfalme Sauli alivyopambana sana kumpoteza Daudi. Ila matokeo yake ni yeye Mfalme Sauli ndiye alitangulia kufa akimwacha Daudi akila maisha.

Na Mwenyezi Mungu akamuinua Daudi hadi akaweza kuja kuwa Mfalme aliyeheshimiwa zaidi pale Israeli.
 
Na Michael Crifford ni kama Dr Kigwangalla aliyekuwa akiishambulia Simba SC original ambayo yeye ni Mwanachama mwenye haki zote za Msingi

Labda tujiuluze aliyevujisha Taarifa za Tukutuku na kumpelekea Mwakyembe ni nani?! 🐼

Jumaa Mubarak πŸ˜ƒπŸŒΉ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…