Tetesi: Tundu Lissu kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha kupeperusha bendera ya CHADEMA

Tetesi: Tundu Lissu kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha kupeperusha bendera ya CHADEMA

Nyuma ya pazia moto unawaka Mkuu, wacha tuone
CDM ni lazima waumiliki mchakato wa kidemokrasia ili kumpata mperusha bendera ktk nafasi ya uraisi, kwa kuwa wanachama wote 11 waliojitokeza wana haki kikatiba. Wote Nyalandu, Mbowe, Lissu na wengineo waliobakia wana haki sawasawa, na hakuna aliye juu ya wenzake.

Ni jukumu la Kamati Kuu ya CDM kuendesha mchakato huu kwa haki pasipo kuangalia majina na hadhi ya mtia nia. Pia ni lazima watambue madhara hasi yaliyotokana na mchakato wa kumpata Mwenyekiti Taifa wa chama chao, hali iliyopelekea kukimomonyoa kwa kiasi kikubwa.

Nafiri pengine Mbowe kachukua fomu kama njia ya kukabiliana na "calculated & manipulated risks" endapo kutatokea pandikizi kuvuruga mchakato huu muhimu ktk chama chao. Watia nia wote waliojitokeza ni lazima wakubaliane na "technical reasons" zitakazopelekea kuwaengua 10 miongoni mwao, na hatimaye akatokea mteule mmoja kati yao kupitia vigezo vya kikatiba vya chama chao.
 
Hawa Chadema walizoea kufanya siasa za tumbo bora wapotee
 
Huu ni ushauri mzuri, lissu akiomba msamaha kwa Watanzania tutsmsamehe tu

Tunajua alikuwa anapata mgao kuwatetea Wazungu dhidi ya madini yetu
Aombe radhi tu
Kumbe Lissu alikuwa anaweza ku-sign mikataba ya uchimbaji wa madini eeeh?

Yaani waliouza madini yetu mko nao na mnakula nao kuku kwa mrija lakini kwa maslahi ya kisiasa mnaamua kupotosha ukweli pamoja na midigrii yenu!

Anyway,that is the choice of many elites of the land
 
Tumesema Rais Magufuli alipokuwa anapambana na Mabeberu kuwatafutia Watanzania mkataba bora wa madini lissu alikuwa anapenyezewa rupia ili kuwatetea Mabeberu

Wenye akili wanajua kilichokuwa kinafanyika,tafuta maandiko ya historia ya kupambania madini ya nchi yetu,miongoni mwa watu waliojitolea kunusuru madini ya nchi hii ni pamoja na Tundu,tatizo kubwa ni kwamba HATUSOMI,tunasikiliza ya kuambiwa!

Nyamongo na Bulyanhulu,ni baadhi ya maeneo ambayo watu walipoteza maisha yao,(waliuawa kwa kukataa kupisha uchimbaji huu mnaoita wizi leo)

Lissu ni miongoni mwa mawakili waliojitolea kuwatetea wananchi wa maeneo yale waliposhtakiwa na serikali kwa kukataa kuachia machimbo yao!

Msingi aliokuwa anausimamia Lissu hata kuitwa MSALITI ni wenye akili tu,wanaweza kumuelewa,lakini kama ni zile Division four za 45...HUWEZI KUELEWA...
 
Mbowe k-vant hajawai simamia jambo na likawa.anafanya mambo yake hovyo hovyo tu.
kikubwa muheshimiwa Lissu aombe radhi watanzania arudi nyumbani kumenoga aachane na siasa za kihuni za Mbowe.
kwanza Lissu anafaa kuwa balozi wa Tanzania nchini ubelgiji.Inshallah.
Kweli kabisa kabisa.
Lisu aachane na siasa za Mbowe za maslahi.

Kwanza Lisu na Mbowe wanaamini kwenye vitu viwili tofauti .
Lisu anaamni kwenye Ujamaa wa Kidemokrasia lakini Mbowe ni Bepari na Beberu anayeamini kwenye udikteta kwa vitendo huku akijifanya mliberali anayeongoza chama cha kidemokrsia.

Lisu aende ACT au CCM kwani ni vyama vyenye mifumo ya kijamaa na bahati nzuri zina viongozi wazalendo wa ukweli.
 
Hata yuda alikuwa mwanafunzi bora kabla hajamsaliti Yesu
Lissu alirubuniwa na Mabeberu kwa kujidanganya kuwa ni Mwanasheria ataweza kuwatetea Mabeberu wapore madini yetu kwa kupewa mamilion

Alikuwa anawapokea pale KIA wanaenda kujifungia ili watuhujumu

Back
Top Bottom