T
Tatizo letu Watanzania ni kufikiria "AJIRA" zile za kufanya kazi kwa mtu, lampuni, kiwanda, ofisi nk ya mtumwingine na kungoja mshahara mwisho wa mwezi. Aliyetufundisha hili na kulipanda mioyono mwetu amefanikiwa sana. Hili wazo potofu halibagui - uwe msomi au uwe hukusoma au hata uwe na uelewa wa namna gani kupitia kisomo chako hicho bado utadai na kusema "hakuna ajira, watu hatueleweki mtaani" kama asemavyo Pangamalasy! Jamani ajira zipo ni suala la kujipanga na kuamua - nenda kauze mchicha, nyanya au ingia shamba ulime hata kanusu ekari. Hizo ndiyo ajira asemazo JPM.