Tundu Lissu: Kuna biashara haramu ya utoaji wa vibali vya uagizaji wa Sukari nchini. Siku nikitaja majina mtashangaa

Tundu Lissu: Kuna biashara haramu ya utoaji wa vibali vya uagizaji wa Sukari nchini. Siku nikitaja majina mtashangaa

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema kuna mchezo haramu unafanyika kwenye utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nchini, na kama wahusika watabisha (watakanusha) tuhuma hizi basi atawataja hadharani.

"Kuna biashara inafanyika na mimi nitataja majina mtashangaa, kuna siku nitataja majina mtashangaa. Kuna watu wanapewa vibali anaambiwa hivi kwa kila kilo moja ya kibali cha kuagiza sukari nje lipa Tsh. 200. Tukikupa tani 30,000, ni kilo milioni 30, zidisha mara 200 ni Tsh. Bilioni 6."

"Mfanyabiashara analipa Bilioni 6 anapewa kibali cha kuagiza sukari, anaagiza sukari anakuja kuongeza yeye Tsh. 1000 juu, wewe unanunua sukari bei imeongezeka kwa Tsh. 1000 ya mfanyabiashara na 200 ya hii biashara ya huyu malkia na watu wake wa Ikulu."

Ameongeza "Kama kuna mtu anabisha anataka tutaje orodha ya viongozi wa kidini waliopewa vibali vya sukari, viongozi wa kidini, Shehe gani kwenye nchi hii ana duka la sukari, au askofu gani kwenye nchi hii ana duka la sukari? Anapewaje kibali cha kuagiza tani 35,000 za sukari afu yeye anaenda kuuza kwa wafanyabiashara anawaambia nipe mia mbili mia mbili kwa kilo, wakibisha na wabishe waone. "
.
 
Dadeki Ccm na machawa wake kwisha habari yao , kwa hili kwakweli atakaegundulika husika hata kwa kivuli chake bila kujali ni nani atupishe kwa namna yoyote ile ama yeye mwenyewe au Nguvu ya umma itemike ,tumechoka ,huozo huu mpaka lini?
 
Kwenye hili kaniboa sana i was expecting ataje majina bila kuogopa ili tudeal na wanaotuhujumu lakini nae ameishia kuwa kama bashite. Tishia nyau watu wazima eti ndio danganya toto ya maandamano yote plus kibali cha mhadhara unaishia kuambiwa wakibisha anawataja so ina maana anawaambia wasipobisha hatawataja.

Watu wameandamana plus kukaa juani kumsikiliza and this is all he had to say ??
Tulia wewe wajikune huone moto utawashwa
 
Mwashambwa mwashambwa AKA mke wa bashite nakuita tena mwashambwa mwashambwa AKA mke wa bashite njooo na huku majibwa Yako yashakwiba tena njoo uyatetee!
 
Lissu ni mtu muoga kuliko kunguru,tunataka nchi safi hivyo Lissu angewataja tujue,athibitishe kama kweli yeye ni jasiri.
Kwani wewe katika maisha yako umewahi kumtaja nani kwa ufisadi? Kwa maelezo tu hayo aliyosema wewe unaweza simama in mahali popote hata mtaani kwako tu ukayasema mbele za watu? Je umesahau orodha ya mafisadi aliowataja Lissu pale mwembe yanga akiwemo PM wa zamani? Kwa sasa hivi hakuna mpinzani mwenye ujasiri kumzidi huyo jamaa. Haogopi mtu huyo jamaa na anajiamini sn
 
Dadeki Ccm na machawa wake kwisha habari yao , kwa hili kwakweli atakaegundulika husika hata kwa kivuli chake bila kujali ni nani atupishe kwa namna yoyote ile ama yeye mwenyewe au Nguvu ya umma itemike ,tumechoka ,huozo huu mpaka lini?
😂 Wabongo bhana 🙌
 
Ameongeza "Kama kuna mtu anabisha anataka tutaje orodha ya viongozi wa kidini waliopewa vibali vya sukari, viongozi wa kidini, Shehe gani kwenye nchi hii ana duka la sukari, au askofu gani kwenye nchi hii ana duka la sukari? Anapewaje kibali cha kuagiza tani 35,000 za sukari afu yeye anaenda kuuza kwa wafanyabiashara anawaambia nipe mia mbili mia mbili kwa kilo, wakibisha na wabishe waone. "
Ndiyo nchi inayo oza hii, hata dini zinahusishwa kwenye uchafu.
 
Wajinga ndiyo waliwao.

Chadomo hawana sera wao wana porojo, kubwabwaja na kuhororoja bila mpango tu.

Hapo hakuna zaidi ya ufataani tu.
Umekuwa mpole sana siku hizi. Kuna sababu maalum inayo kufanya uwe na hali hii.

Na bado!
 
😂 Wabongo bhana 🙌
Inawezekana hakuna cha wabongo , haya yanapofikia nafikili sio watumishi wa umma katika ofisi za umma na wazalendo mbalimbali wanafurahia ujinga ,machawa tu ndo wanakubaliana na ujinga huu
 
Angewataja hao masheikh waagiza sukari tuwajue.
Hajasema hatawataja. Hata kwenye hayo maneno aliyonukuliwa kuyasema, amesema "atawataja" hata kama siyo leo.

Kuna muda na wakati mwafaka wa kufanya hivyo.

Kwanza usisahau, Lissu ni MWANASHERIA kwanza..., umelitazama hili?

Tayari taarifa muhimu inayo ambatana na kutaja imetolewa, na inaeleweka.

Na kusema kweli hii siyo habari mpya hata kidogo, kwa sababu ilikwisha andikwa kwenye vyombo vya habari.
Tofauti yake ni hiyo tozo ya Tsh 200, basi, na maudhui ya umuhimu wa kuifanya kazi hiyo - kuwapa wahusika pesa wasiyoistahili ya kuchafua siasa nchini.
 
Wazalendo wa nchi ,bila kujali upo mtaani au ofisi za umma mda wa kuunganisha nguvu ni huu kama hii kitu ni kweli, ikiwezekana hata kama kuna kivuli kimeshiriki lazima kiondoke ofisin, hii ni hatari kwa nchi kama ni kweli , kwamba watu wasio na vigezo wanapewa vibali vya kuagiza sukari , je afya za watumiaji wa sukari ambazo wenda kweli imeagizwa kinyemela kesho yao ni ipi maana sio madhala yanaweza onekana papo kwa papo.

Nasema madhara ,kwangu ,na watanzania wote tunaotumia sukari ukiachana na wengine ambao hawatumii tokana na sababu mbalimbali ikiwemo maradhi bila kujali dini ,au chama , maana wenda usalama wa sukari kama kweli wameagiza watu wasiohusika kwa mjibu wa sheria ,sasa tuna imani ipi kwamba iyo sukari ipo salama?

Kama ndinvyo wahusika katika sakata hili wanabakije salama kama kweli ni kweli ,haiwezekani
 
Nini kinafanya hoja za wapinzani zisitikise nchi? Watu wameshawazoea kwamba ni wa hivyo hivyo tu?
Watu gani sema wewe mwenyewe kama umejifungia kwenye kabati umefungiwa kama yule Diwani wa Dar aliefungiwa Tabata , watu wanatafuta kumbe yupo kula mema ya nchi kwa bibie mmoja
 
Back
Top Bottom