Tundu Lissu: Kuna biashara haramu ya utoaji wa vibali vya uagizaji wa Sukari nchini. Siku nikitaja majina mtashangaa

Tundu Lissu: Kuna biashara haramu ya utoaji wa vibali vya uagizaji wa Sukari nchini. Siku nikitaja majina mtashangaa

Vyombo vya habari havitangazi hoja zao vinachagua negatives tu ndiyo vinatangaza.
 
Wajinga ndiyo waliwao.

Chadomo hawana sera wao wana porojo, kubwabwaja na kuhororoja bila mpango tu.

Hapo hakuna zaidi ya ufataani tu.
Ajuza wa jumba jeupe ndio pekee mwenye akili kwenu nyie.
 

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema kuna mchezo haramu unafanyika kwenye utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nchini, na kama wahusika watabisha (watakanusha) tuhuma hizi basi atawataja hadharani.

"Kuna biashara inafanyika na mimi nitataja majina mtashangaa, kuna siku nitataja majina mtashangaa. Kuna watu wanapewa vibali anaambiwa hivi kwa kila kilo moja ya kibali cha kuagiza sukari nje lipa Tsh. 200. Tukikupa tani 30,000, ni kilo milioni 30, zidisha mara 200 ni Tsh. Bilioni 6."

"Mfanyabiashara analipa Bilioni 6 anapewa kibali cha kuagiza sukari, anaagiza sukari anakuja kuongeza yeye Tsh. 1000 juu, wewe unanunua sukari bei imeongezeka kwa Tsh. 1000 ya mfanyabiashara na 200 ya hii biashara ya huyu malkia na watu wake wa Ikulu."

Ameongeza "Kama kuna mtu anabisha anataka tutaje orodha ya viongozi wa kidini waliopewa vibali vya sukari, viongozi wa kidini, Shehe gani kwenye nchi hii ana duka la sukari, au askofu gani kwenye nchi hii ana duka la sukari? Anapewaje kibali cha kuagiza tani 35,000 za sukari afu yeye anaenda kuuza kwa wafanyabiashara anawaambia nipe mia mbili mia mbili kwa kilo, wakibisha na wabishe waone. "
Duuh
 
Ndio maana nchi haitakaa kamwe iweze kujitegemea kwa uzalishaji wa bidhaa maana kuna watu wao na familia zao biashara yao ni kuagiza bidhaa kutoka nje. Kwa mfano watahujumu kwa nguvu zote sekta ya sukari kuanzia mashamba hadi uanzishaji wa viwanda vya sukari. Hata wakijidai kuanzisha kiwanda ni kuzuga ili waendelee kuagiza kutoka nje. Kuna familia zingine ni wagizaji wa ngano wengine wa mchele, wengine magari. Unakuta familia kama hizo nyingi niza asili ya kiasia na ni shughuli yao toka enzi ya ukoloni. Kwa hivyo kuhujumu viwanda na kuhonga wapewe vibali kupambana na vikwazo kuagiza ni katika kuhakikisha wanaendelea na maisha yao. Inahitaji uongozi aina ya kimagufuli kukabiliana na watu wabinafsi wenye kulinda maslahi yao kwa gharama ya mma na taifa ambalo linahitahi maendeleo ya kweli ya kiuchumi kwa watu wake.
Upo sahihi. Hao waagizaji ndio wanaharibu kila kitu. Kuanzia ngano, mbolea, mafuta, mafuta ya kula, sabuni, sukari, mchele, madawa ya binadamu, nguo, vitenge e.t.c.


Uzalishaji wa viwanda vya ndani bado una safari ndefu.
 
Ajuza wa jumba jeupe ndio pekee mwenye akili kwenu nyie.
Chama cheye sera zinazoeleweka ni CCM pekee, ndicho kinachoongoza nchi.

Hivi wananchi wenye akili zao waichaguwe chadomo kwa lipi zaidi? Sera yao nini zaidi ya majungu?
 
Malikia wenu huyu anajifanya mvaa ushungi kumbe mwizi tu?

Ndio maana juzi kwenye kura za maoni za gazeti la mwananchi alipata kura 17% dhidi ya 59% za marehemu

Wanaomwelewa huyu bibi ni wale machawa wake tu

Kina Bashe ndio mabumunda kabisa yanajifanya yako busy kumbe ni mahuni tu
Wewe ndiye Tundu Lissu? Hapana. Bali wewe ni mfuasi wa yule hayati aliyetaka kumuua Tundu Lissu. Ila Mungu alivyo wa ajabu akafa yeye kabla ya Tundu Lissu. Crimea kaa mbali na mambo ya Lissu
 
Vilaza Mmeshapanik ....huyo haongeagi bila data hiyo KITU tunasemaga TAYARI!!

Stay tuned...hawako Bungeni ila Wako kwenye BUNGE LA WANANCHI
Anasubiri nini sasa kutaja? Au mpaka mabasha wake wa Brusssels wamruhusu?
 
Tundu Lissu atabali kila aina ya mipasho, Mzanzibari hajibu yule.

Mama Samia hapapariki kama mwendazake, yeye kimya tu. anaamini vitendo ndiyo vinatowa majibu.
 
Chama cheye sera zinazoeleweka ni CCM pekee, ndicho kinachoongoza nchi.

Hivi wananchi wenye akili zao waichaguwe chadomo kwa lipi zaidi? Sera yao nini zaidi ya majungu?
Majungu anayapika Bashite, eti ajuza ndiye anamtegemea kwenye ufitinishaji.
 
Tundu Lissu atabali kila aina ya mipasho, Mzanzibari hajibu yule.

Mama Samia hapapariki kama mwendazake, yeye kimya tu. anaamini vitendo ndiyo vinatowa majibu.
Tunajua kuwa mzanzibari, Sasa anawashwa na nini kuwafukuza wamasai nyumbani kwao!? Ili awakabidhi wajomba zake waarabu au!?
 
Lissu anaanza kuvaa vema viatu vya Dr. SLAA na Magufuli kwa mbaaaali sasa naanza kuona Lissu Mpya
Jiwe hakuwa mpenda demokrasia,
Pia kumbuka ya CAG Assad
 
Nini kinafanya hoja za wapinzani zisitikise nchi? Watu wameshawazoea kwamba ni wa hivyo hivyo tu?
Main stream media hazitangazi zinachagua vile negative tu.

Hata wenyewe CDM wanatatizo kubwa sana kwenye kusambaza taarifa zao.

Mikutano inaendelea nchi nzima lakini wao kwenye social media zao hawaziweki taarifa kwa wakati wanasubiri nyomi tu.

Nadhani CDM wanaupungufu wa strategists kwenye chama ndiyo maana wanafanya siasa kwa survival mode tu.

Kuna haja kubwa ya wao kubadilika ili wananchi wapate taarifa zao.
 
Back
Top Bottom