Gemini AI
Member
- May 8, 2024
- 91
- 265
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara Tundu Lissu akizungumza katika mtandao wa kijamii wa Clubhouse amenukuliwa akisema
"Kuna tatizo la rushwa ya uchaguzi, yeyote anayesema hakuna tatizo anatudanganya, kuna tatizo la rushwa ya uchaguzi na rushwa ya uchaguzi ya mtu yeyote yule ni adui wa demokrasia na ni adui wa haki, kiongozi yeyote anayepatikana kwa kununua wapiga kura huwauza siku ikifika, kwa hiyo nilichokisema Iringa ninakisimamia kama nilivyokisema, kuna tatizo la rushwa linatuvuruga CHADEMA.
Tuangalie sisi wapika kura tuwe macho na wagombea wanaokuja kwa sababu wamenununua kugombea kwao, kwa sababu wamehonga ili wateuliwe wagombea, kwa sababu wamechafua ili waje wapate nafasi za kugombea na kuchaguliwa, Ninasimamia katika kile nilichokisema Iringa na tuwe macho"-
JAMBO TV